Saikolojia Marufuku Kumfanya Mwanamke Akupende


Hebu tuweke vitu wazi. Ni vigumu kumtongoza mwanamke ambaye unampenda. Hata kama unajiamini kiasi gani, kuna wakati mwingine inatokea unashindwa kuelewa mbona wanawake wengine unaweza kuwatongoza lakini huyu mmoja anakushinda.

Yeah. Ni ukweli jambo hili linakuwa gumu kwa baadhi ya wanaume, lakini ukweli ni kuwa haifai kutokea kama hivi. Hii hutokea kwa sababu wanaume wengi wanachukua mtizamo wa kuwa kuapproach demu aina hii ni vigumu hivyo wanasahau kutumia mbinu zile rahisi ambazo zinaweza kumnasa mwanamke yeyote yule.

Ok. Kama umekuwa katika nyanja ya kudeti wanawake unafahamu ya kuwa kuna hatua za kutongoza mwanamke. Mwanzo unaanza na approach halafu ile inayofuata kawaida ni kuwashawishi wakupende. Na hatua zote hizi mbili ni tofauti kabisa na kumfanya mwanamke akupende.

Kama kweli una azma ya kuuteka moyo wa mwanamke wa ndoto yako, basi, ni lazima uifahamu mbinu ya saikolojia marufuku na jinsi ya kuitumia saikolojia marufuku kumfanya mwanamke akupende. Saikolojia marufuku ni mbinu ambayo imekuwa ikizua mijadala tofauti tofauti katika dunia ya kudate. Mbinu hii ya kutongoza ilianzishwa na baadhi ya guru flani ambao wamekuwa wakifanya tafiti katika sekta hii kwa muda.


Ok kupunguza stori ndefu, nataka nikuintroduce kwa hii mbinu.

Kutumia saikolojia marufuku kumfanya mwanamke akupende

Psss: Ijapokuwa mbinu hii huwekwa kama siri kwa baadhi ya watu, wanaume wengi wameanza kuitumia ili kufanikisha kuwavutia wanawake wanaowapenda.

1. Jifundishe jinsi ya  kuisimamia akili yake
Njia rahisi ya kuweza kuuteka moyo wa mwanamke ni kwa kuingia katika akili yake. Narudia. Kuitawala akili ya mwanamke inaweza kuleta mafanikio makubwa katika dunia ya kudeti wanawake. Kile unachotakiwa hapa ni kutumia majibu ya kumchanganya ili uweze kukikoroga kichwa cha mwanamke na kubadilisha mawazo yake kukuhusu. [Soma: Saikolojia kumfanya mwanamke akupende daima]

2. Jenga mchanganyo wa akili
Mchanganyiko wa akili kwa lugha rahisi inamaanisha kuikoroga akili ya mwanamke na mawazo yake. Tofauti na kuisimamia akili yake, mbinu hii haihusishi kuikontrol akili ya mwanamke kiukamilifu; inachanganya akili ya mwanamke pekee. Kimsingi, ukiendelea kuichanganya akili ya mwanamke mara kwa mara itafikia wakati flani mawazo yako kwake yataanza kuivamia akili yake. Atakuwa akiweka sehemu flani katika mawazo yake ambapo atakuwa akikuona. Kufanikisha mbinu hii vizuri, unafaa kubadilisha badilisha hisia zako ambazo zinaonyesha kumpenda na zile hisia nyingine ambazo umezihifadhi.  Mbinu hii ni silaha rahisi kwako kumchanganya akili yake kwa sababu atakuwa haelewi misimamo yako kwa uharaka.[Soma: Ingia akili ya mwanamke]

3. Jenga uwepo wa kudumu
Mbinu hii ni kumfanya mwanamke akuwaze mahala popote pale ambapo atakapoenda. Kiufupi mbinu hii ni kuingia katika akili ya mwanamke na kumfanya akuwaze wakati wake wote. Ukifanikiwa kuitumia mbinu hii ipasavyo utamfanya mwanamke akupende papo hapo. Uzuri wa kutumia mbinu hii ni kuwa unarahisishiwa kazi yako ya kumfanya mwanamke akupende. Atavutiwa na kupendezwa na wewe bila kutumia ujanja zaidi. [Soma: Kumfanya mwanamke akuwaze milele]

4. Yaangalie macho yake
Mbinu hii ni ya kawaida kama vile unaweza kumvutia mwanamke kwa kumuangalia macho yake ama pia kumboa. Katika saikolojia marufuku, mbinu hii inaweza kuleta utata kwani wakati mwingine inaweza kumfanya mwanamke asipendezwe na jinsi unavyowaangalia. 
Ujanja wa kutumia hapa kwanza unafaa kuanza na gumzo ambalo atajiskia huru na kuweza kumakinika na wewe, mfanye akijiskie yuko karibu na wewe. Halafu sasa ndio unaweza kutumia mbinu hii ya kumwangalia.[Soma: Njia tofauti za kuteka atenshen ya mwanamke kwa kutumia macho]

5. Tumia saikolojia mjeuko
Ushawahi kugundua ya kuwa wanawake wanapenda kusema kitu ambacho ni tofauti na kile wanachomaanisha? Wanaficha hisia zao kwa kumaanisha tofauti? Well, hii ni sababu wanawake wamebugia kwa kutumia saikolojia mjeuko. Mwanzo kutumia saikolojia mjeuko kama mbinu moja wapo ya saikolojia marufuku hufanya kazi vizuri sana. So iwapo umejikuta katika situation ambapo una ugomvi ama kutoelewana na mwanamke kwa jambo flani mbona usijaribu kukubali kushindwa na ufuate kile anachotaka? Ijapokuwa hii itamaanisha umeacha kupigania kuhusu jambo ambalo liko sawa, utamweka na fikra za kuwa anaweza kufanya kile anachotaka kwako iwapo atakubali kutoka na wewe.  Hii ni njia ambayo unaweza kuitumia kiurahisi kumfanya mwanamke akakupenda, bila hata kutokwa na jasho.

ILANI: Kutumia mbinu ya saikolojia marufuku inafaa kutumiwa na umakini wa hali ya juu. Hii inamaana ya kuwa mbinu hii ukiitumia kupita kiasi inaweza kuwa hatari ama inaweza ikakujeukia.


1 comment:

  1. Mimi na tatizo la kukosa mameno ya kumwambia machina ninetaka kumtongoza nipeni mwongozo

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.