Zijue Hatua Za Kumfanya Mwanamke Akutamani


Ungehisi vipi kama kila unapoamka asubuhi mwanamke unayemjua anakuwa wa kwanza kukutumia jumbe za kimahaba na kukuambia, "Jana sikulala, nilikuwa nakufikiria wewe"?

Ama je, kila ukikutana na huyu mwanamke anakwambia, "bebi usiende, nataka muda mwingi na wewe. Nakumiss sana"?Ni raha iliyoje hii?

Sasa fikiria ungekuwa na uwezo wa kufanyia hivi mwanamke yeyote yule unayekumbana naye! Ni nishati ya ajabu!

Uzuri hapa Nesi Mapenzi hatukosi kuja na ujanja mpya. Fuata mbinu hizi hakika 3 ambazo zitamfanya mwanamke yeyote akutamani.

#1 Kuwa wingu lisilofahamika.
Hii inamaana ya kuwa usikuwe na yeye wakati wote. Kama mmepanga kukutana na yeye ili muongee kwa saa limoja, hakikisha umekaa na yeye muda wa nusu saa halafu utoe kisababu cha kujiondoa katikati ya maongezi yenu. Hii itamfanya kuachwa kwenye mataa na kutaka kujiuliza maswali kama mungekuwa naye saa zima mngeongea nini. Hii itamfanya yeye kukufikiria kwa urahisi. Lile ambalo mmeliacha kati kati litakuwa likimzunguka akilini mwake. [Soma: SMS 47 za mapenzi za kumnyegeza mwanamke]

#2 Uwe usukani.
Mwanamke yeyote, uwe uko na mahusiano naye au la, hakikisha kuwa wewe ndiye unayeamua mambo yote mtakayoyafanya mkiwa pamoja. Kama ni kuchagua sehemu ya kukaa, sehemu ya kula, sehemu ya kutoka ama chochote kile ambacho mnachotaka kufanya, wewe ndiye utakuwa ukiamua bila kumwachia nafasi yeyote ile. Huu ujanja utamfanya yeye kutofanya jambo lolote bila kukufikiria wewe. Yaani atakuwa hawezi kujiamulia mwenyewe hadi wewe uwe karibu yake. Hii moja kwa moja itakuwa njia rahisi ya kwake kukufikiria wakati wote ule atakapokuwa akifanya shughli zake. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke atambue uwepo wako]

#3 Kuwa mtu wa mwisho akilini mwake.
Utafiti umegundua ya kuwa kile kitu ambacho mtu hufikiria cha mwisho ndicho kitakachomjia ndotoni mwake. Na kama usiku wake umemuendea vizuri bila tatizo, basi asubuhi yake kitu hicho hicho kitakuwa bado kinamjia akilini. Mbinu hii inaweza kutumika vizuri kama utahakikisha ya kuwa wewe ndiye mtu wa mwisho kabisa ambaye anaongea naye...yaani unaweza kumpigia simu nyakati zake za kulala. Hii itamfanya yeye kuweza kukuota na kuchangia  kukufikiria siku ya pili. Hii ni njia nyingine rahisi ambayo itamfanya yeyote kukufikiria mara kwa mara.

Niamini, ukitumia mbinu hizi tatu vizuri, mwanamke yeyote atakuwa akikufikiria wewe mara kwa mara na inafanya kazi asilimia 100 bila shaka yeyote ile.
[Soma: Jinsi ya kurespond baada ya mwanamke kukukataa]1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.