Mbinu Nzuri Ya Kutongoza Kwa Wale Wanaoanza Kujifunza


Katika maoni ambayo tuliyaweka kwa app yetu ya Nesi Mapenzi, tuliuliza iwapo kutongoza mwanamke ni rahisi au vigumu. Na majibu mmetupatia. Kulingana na maoni yenu, 36% wamesema kutongoza ni vigumu, 13% wamesema  ni rahisi, wengine 38% wameonelea kuwa kutongoza kunategemea na mtu ilhali  11% wamesema hawajui. [Download: App ya Nesi Mapenzi]

Sisi hapa Nesi Mapenzi tunaamini ya kuwa kutongoza ni rahisi. Tena ni rahisi sana. Kile kitu ambacho unafaa ufanye ni kuondoa uoga. Uoga ndio unaofanya wengi kuona ya kuwa kutongoza ni kazi ngumu na nzito.


Uoga unaletwa na dhana ya kuwa ukimuapproach mwanamke atakuona wewe hufai na pia anaweza kukuona wewe ni mdhaifu kwake. Jambo hili ndio chanzo cha woga huu wote. Pindi ukianza kufikiria zaidi kumhusu mwanamke unayetaka kumuaproach ndipo unazidi kujiongezea dhana nyingi ambazo zinaongeza woga. Kuna njia rahisi ya kuiondoa hii dhana ya kuwa mwanamke atakuona wewe hufai. Ni mbinu rahisi ambayo imekuwa ikitumiwa na wengi bila wao kujua. Hata wewe labda ushawahi kuitumia mbinu hii. Inaitwa kushusha hadhi.

Mbinu hii ni rahisi kuitumia kwa mwanamke na pia kwa yeyote yule. Nina uhakika ya kuwa labda hata wewe ushawahi kuitumia. Inaweza kuwa umeitumia mahali popote pale. Uzuri wa mbinu hii ya kushusha mtu hadhi hufanya kazi kila wakati.


Mfano mzuri ni huu:-


Mara ngapi ushawahi kukutana na watu wanao ombaomba pesa barabarani, nje ya maduka na  ukawapuuza?

Hii ndio kushusha mtu hadhi. Akili yako unaifunga ili usimwonee huruma mtu kama yule anayeombaomba pesa. Pindi utakapoanza kufikiria shida anazozipitia nyumbani mwake, njaa, ama ugonjwa alionao, basi bila shaka utampa pesa na zaidi unaweza kumpeleka hospitali ama kumtafutia makaazi ya kuishi.

Lakini kwa kuwa umemshusha hadhi hauoni shida zake.

Mbinu io hio pia unaweza kuitumia kwa mwanamke ili uweza kumtongoza kwa urahisi. So, mbona usimshushe hadhi mwanamke ili usione kuwa ni mrembo, anavutia ama atakukataa?

Anyway, somo hili linapatikana kwa upana ndani ya kitabu chetu cha Kutongoza Mwanamke: Kuanzia Hadharani Hadi Kitandani.

Turudi kwa mada yetu...
Narudia, jambo la kwanza nataka uelewe ya kwamba kutongoza mwanamke si kazi ngumu, ni kama vile kuendesha baiskeli ama vile kuogelea. Mara ya kwanza unaweza kuona ni jambo gumu lakini ukifaulu mara ya kwanza basi hutoweza kushindwa kamwe. Wale marafiki zako ambao hakupiti mwanamke kabla hawajawatongoza walianza pale ulipo sasa, lakini baada ya muda wamekuwa mabingwa wa kutongoza.

Kabla hujaifahamu sanaa ya kutongoza naamini ya kuwa wewe ni mtu unayejiamini. Kujiamini wewe mwenyewe ni jambo muhimu ambalo linahitajika muda ili uweze kufanikisha kutongoza. Kama bado hujajijenga ili ujiamini wewe binafsi basi itakuwa vigumu kiasi kutekeleza swala la jinsi ya kutongoza. [Soma: Kwa nini wanawake wanakataa kusimama ukiwaaproach]

Jinsi ya kutongoza mwanamke kwa uharaka

Haya hapa ni baadhi ya mambo ya kutumia ili uweze kumtongoza mwanamke kirahisi

1. Mpe kipaombele, atenshen

Ushamtambulisha kuwa huyu ndie unayemzimia. Utafanya nini mpaka akunotice?
Kile cha kufanya hapa ni kumuangalia machoni mpaka aone aibu ya kukuangalia. Pia unaweza kucheza na mbinu ya kumuangalia halafu akitaka kukuangalia wewe unaangalia kando halafu unamuangalia papo hapo. Kufanya hivi kutakuwa kunavuta atenshen yake kutaka kujua mbona unapenda kumuangalia mara kwa mara.


NB: Usitumie mbinu hii mara kwa mara kwani unaweza kumuogopesha ama kukuona punguani. [Soma: Njia tofauti za kuteka atenshen ya mwanamke kwa kutumia macho]


2. Mguse kibahati mbaya

Iwapo huyo ambaye unamzimia ni mtu mnajuana, unaweza kumshika ama kugongana naye kibahati mbaya. Hii italeta atenshen kwenu wawili na utachukua nafasi ya kumuomba msamaha. Labda anaweza kukuuliza maswali ambapo unaweza kuendeleza na gumzo. Mfano unatembea halafu ukamgonga akaangusha vitabu vyake, ukamwambia samahani halafu akakujibu alikuwa anaenda kusoma maktabani, wewe ukamjibu kuwa ulikuwa umetoka huko sababu kuna joto jingi so unaelekea kusoma kwa uwanja. Halafu unamwomba kama anaweza kwenda na wewe kusoma pamoja. [Soma: Utajuaje kama mwanamke anakupenda?]


Iwapo humjui, kile unachotakiwa kufanya unaweza kumshika ama kugongana naye kibahati mbaya lakini usiongee kitu chochote. Mpe tabasamu halafu ujiondoe. Hii itamfanya kujiuliza maswali ya kwa nini umemfanya hivyo na anaweza kutaka kukujua zaidi ama kuuliza marafiki zake kukuhusu.


3. Ukiwa unaongea na yeye mpe dokezo kuhusu maisha yako

Iwapo umefaulu kuweza kupata kikao chake na chako, hakikisha wakati unapoongea mdokezee mambo mazuri ya kutoka kwako lakini usimuelezee kila kitu kukuhusu. Mfano unaweza kuwambia kuwa wewe ni msanii lakini usijieleze ni msanii wa aina gani. Kufanya hivi kutampa kiu cha kutaka kuongea na wewe siku nyingine ili kutaka kujua zaidi kukuhusu.
Pia wakati wa maongezi yenu hakikisha una nakili maneno yote ambayo huyo unayemzimia anapenda. Hii inaweza kuibua mada zaidi na zaidi wakati mtakapokutana mara nyingine.


4. Msogelee karibu na pale alipo

Wakati unapoongea na yeye kuwa jasiri wa kukaa karibu na pale alipo. Weka uoga kando na uonyeshe ujasiri wako wa kuongea na yeye akiwa karibu yako. Kufanya hivi utakuwa unaonyesha kuwa wewe unajiamini na kuwa hautikisiki. Wanawake hupenda sana kuona mwanaume jasiri hivyo ukitumia mbinu hii kuna uwezekano mkubwa wa yeye kukupenda. [Soma: Mfanye mwanamke akutamani]


5. Leta tenshen ya kimapenzi

Njia nyingine ya kutongoza mwanamke unaweza kujaribu kufanya kumshika viganja vyake wakati unapoongea. Hapa kutaleta msisimko wa kimapenzi kati yenu. Mfano ikiwa unaongea na unayemzimia, unaweza kumuangalia kucha zake na kumwambia kuwa unazipenda. Atakuuliza kwa nini? Wewe mjibu kuwa kuna kitu ambacho kimekuvutia ambacho hujakielewa. Kama ataingiliana na huu mtego basi fanya kuushika mkono wake na kuanza kucheza na viganja vyake mkononi mwako. Pia unaweza kutumia mbinu ya kuleta ucheshi halafu mara moja au nyingine uwe unamgusa au kumdara mapajani au mkononi kuashiria kuwa jambo fulani linawachekesha. Hii moja kwa moja italeta tenshen ya kemia kati yenu.

NB: Kumbuka ya kuwa hii mbinu unaitumia kumfanya mwanamke akupende zaidi na wala haimaanishi ya kuwa itakusaidia kumpata kingono. [Soma: Fahamu hatua za kuleta tenshen ya kimapenzi kwa mwanamke]


6. Mwangalie machoni

Hii ni mbinu ambayo imekuwa ikielezwa mara kwa mara ya kuwa lazima umuangalie mwanamke machoni wakati unajifunza jinsi ya kutongoza. Baadhi ya umuhimu wake ni:


 • Unaweka atenshen yote kwa kitu kimoja, yaani unamwangalia umpendaye pasipo na kutatizwa na maswala mengine
 • Inakupa mawazo ya haraka ya kufikiria wakati unapoongea
 • Unamfanya yule unayeongea naye kukuona uko serious na mambo unayoongea.
 • Kunapunguza wasiwasi
 • Kunajenga tenshen ya kimapenzi kati yenu

Mwisho: Ukihakikisha ya kuwa umefuata mbinu hizi kwa umakini, basi itakuwa rahisi kwako kuhakikisha ya kuwa umeweza kuteka hisia za yeyote yule ambaye umemzimia. Hapo ndipo unaweza kufunguka na kumwambia kuwa umemzimia na ungependa kuwa nayeye kama mpenzi wako. Kama bado unatashwishi ama uoga basi kuna kazi nzito inakungojea. [Soma: Toa woga wa kuapproach mwanamke haraka na hizi mbinu]

15 comments:

 1. je kama unayetaka kumtongoza unataka uwe nae ana kwa ana

  ReplyDelete
 2. Huwa nkimuapproach msichana pindi TU nkimaliza introduction naishiwa na maneno kabisa Kisha napoteza atensheni na msichana..nisaidie

  ReplyDelete
 3. Jaman nashidwa nianzeje nisaidie

  ReplyDelete
 4. Eeeeh hapo kwanza nichek 🤣🤣🤣

  ReplyDelete
 5. Maneno tano muhimu ya kumtongoza mrembo

  ReplyDelete
 6. Poa bro kwa kunisaidia☺☺☺☺

  ReplyDelete
 7. weeeeee wacha nijaribu

  ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.