Mwanamke 'Wife Material' Utamtambua Na Tabia Zipi? -Ishara 13 Tunazo


Itatimia wakati flani ambapo utahitajika kuoa. Na kuoa huwa kuna harakati zake. Mtu hafai kuingia katika mpango wa ndoa bila ya kutambua yule ambaye ataona naye.

Ikija katika maswala ya kuoa, utaskia wengi wakitumia maneno kama `wife material` ama `mke bora`. So utamtambuaje mwanamke ambaye ni wife material/mke bora?

Kuna baadhi ya vigezo ambavyo watu huangalia na kutambua kama mwanamke ni wife material au la. Na muhimu zaidi huangalia tabia na matendo ya mtu.

Kosa ambalo wengi hufanya ni kuwa wanakimbilia kuoa mwanamke bila ya hata kusoma tabia za wanawake hao ndio unapata wakati mwingine ndoa za baadhi ya watu zinakuwa na shida miaka michache baada ya kuoana.

Eric Omondi akiwa na wife material wake Carol

Katika somo la leo hapa Nesi Mapenzi, tumekuja na tabia ambazo zitamtambua mwanamke ambaye ni wife material kwa urahisi sana.

Zama nasi!

Tabia za mwanamke ambaye ni wa kuoa (wife material)

1. Anakusikiliza wakati unaongea.
Ijapokuwa hili linaonekana swala dogo, ikija kwa kuchagua mwanamke lina umuhimu mkubwa. Mwanamke ambaye anakusikiliza wakati unapoongea ni ishara kuonyesha kuwa anakuheshimu. Na heshima ndio msingi wa ndoa.

2. Anaingiliana na wengine kiurahisi.
Mwanamke wife material ni yule ambaye ni rahisi kwake kuingiliana na watu wengine bila tatizo. Hakasirishwi na mambo madogo madogo ambayo wengine wanaweza kumfanyia. Badala yake yuko tayari kukumbana na chochote ambacho atapitia akiwa anajumuika na wengine.

3. Anakushughulikia iwapo umekuwa mgonjwa.
Angalia mwanamke ambaye unadeti naye kwa sasa. Iwapo anataka starehe pekee na hashughuliki na wewe kama umekuwa mgonjwa huyo si wife material. [Soma: Tambua kama girlfriend wako anakupenda]

4. Ana tabia za kimama.
Mwanamke unayedeti kama anapenda watoto wa wengine na kuwajali ni ishara nzuri kuwa atakuwa na hulka nzuri za kimama. Hivyo iwapo anapenda watoto wa wengine, wako atawapenda zaidi.

5. Anakuwa na uamuzi huru.
Wakati unatafuta mwanamke wa kuoa, hakikisha mwanamke huyu anakuwa na uamuzi wake binasfi. Usikubali kuoa mwanamke ambaye kila kitu ambacho anataka kufanya lazima akuulize wewe.

6. Haabudu pesa.
Mwanamke wife material ni yule ambaye hana tamaa ya pesa. Ndoa huwa zina changamoto zake. Hivyo kama mwanamke uliye naye amezoea pesa basi ule wakati pesa zitatoweka naye pia atakutoka.

7. Anawapenda marafiki zako.
Mwanamke aina hii huwa anawathamini sana marafiki zako. Hii ni muhimu kwa kuwa anajua thamani ya marafiki zako. [Soma: Jinsi ya kupata mwanamke kirahisi]

8. Anakusaidia ufanikiwe maishani.
Sifa nyingine za mwanamke ambaye ni wife material ni kuwa yuko tayari kukujenga kimawazo ili uweze kufanikiwa kimaisha. Ukiona mwanamke hata hajui kazi unayofanya achana naye huyo hakufai.

9. Anaficha udhaifu wako.
Kila mtu anakuwa na udhaifu wake kwa njia moja au nyingine. Hivyo mwanamke ambaye ni wife material akiutambua udhaifu wako hawezi kukutenga bali atafanya kila juhudi kuhakikisha unakabiliana na udhaifu huo hadi unafaulu.

10. Yuko tayari kuvumbua mapya chumbani.
Ikija katika maswala ya chumbani, mwanamke ambaye ni wife material yuko tayari kuvumbua mambo mapya. Kama kifo cha mende kimewachosha mnaweza kujaribu daudi msalabani bila tatizo. [Nunua: Kitabu cha Staili 365 Za Kufanya Mapenzi]

11. Anaelewana na mamako.
Mwanamke wife material ni yule ambaye ukimpeleka kumtembelea mama yako anaelewana na yeye na wanakuwa marafiki. Ukiona anamkashifu mama yako kuwa hampendi basi huyo hakufai.

12. Familia yako inampenda.
Ukiona ya kuwa kila mtu katika familia yako hakosi kumtaja mwanamke huyu mara kwa mara kwa nia nzuri, basi huyo amepitishwa na familia na ni wife material tayari.

13. Anaheshimu ndoto zako.
Mwanamke wife material ni yule ambaye yuko tayari kukusaidia kutimiza ndoto zako. Kama ana uwezo wa kusaidia kufanikisha kile ambacho unatamani kukitimiza maishani basi mwanamke aina hii ni wa kuoa.

Upo!!

Hizi ni baadhi ya tabia za wife material lakini kuna tabia nyingine nyingi ambazo unaweza kuongeza ili uweze kumtambua yule ambaye anakufaa. [Soma: Maneno ambayo mwanamke angependa umwambie]No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.