Maneno 14 Ambayo Mwanamke Anatamani Umwambie


Ikija katika maswala ya kuwavutia wanawake, kile kitu ambacho utamtamkia kitakusaidia pakubwa katika azma yako ya kumuwini.

Hakuna ujanja wowote ambayo unatumika bali ni maneno yako. Wanawake ni viumbe ambao ni wasikilivu ilhali wanaume ni viumbe waangalifu, hivyo matumizi yako ya maneno ni silaha nzito ambayo umebarikiwa nayo.


Ok. Ikija katika usikilizi, kila mwanamke huwa tofauti. So itabidi umsome mwanamke kwanza na uyafahamu mambo gani anapenda ili ikija wakati wa kumtamkia maneno itakuwa rahisi kwako kumteka kihisia. Tumeandaa orodha ya maneno ambayo ukiyatumia yapasavyo yatakusaidia kumzuzua mwanamke yoyote awe rafiki yako ama mpenzi wako. Zama nasi.

#1 Yuko smarti. Hapa hauwezi kukosea wakati utakapomwambia kuwa anapendeza. Unachohitajika ni kumtamkia maneno kama haya wakati ufaao. Unaweza kumweleza sehemu ambayo unaona yuko smarti na utakuwa unamfurahisha wakati wote.

#2 Unapenda jazba na msukumo wake. Kama umeona kuwa mwanamke aina hii ana ari na msukumo wa kufanikisha jambo flani basi unapaswa kumpongeza. Kama hana msukumo wowote katika maisha halafu umsifie atashangaa unamsifia na nini. So hakikisha kuwa unampa sifa aina hii kulingana na msukumo wake wa kutimiza jambo fulani katika maisha yake.

#3 Unapenda vyenye anavyoishi. Hapa unamsifia maisha yake yote. Hii ina maana kubwa katika kila kitu cha maisha yake. Wakati unapomtamkia maneno kama haya hakikisha kuwa unakuwa serious na kile ambacho unatamka.

#4 Kuwa yeye ni muhimu kwako. Kama unajaribu kumuonyesha mwanamke kuwa unamweka kipao mbele katika maisha yako unapaswa umwambie kuwa yeye ni muhimu katika maisha yako. Haya ni matamshi mazito ambayo utamfurahisha na kutamani kuwa na wewe milele.

#5 Yeye ni tofauti na wengine. Kila mwanamke anatamani kuwa spesho. Wanatamani kuwa tofauti na wanawake wengine wale wote. So msifie mwanamke na umwambie kuwa yeye ni tofauti, hakuna mwanamke mwengine ambaye anaweza kufikia kiwango chake. Utafaulu kumuwini.

#6 Unajali maslahi yake. Wanaume wengi mara nyingi huwa wanashindwa kutamka maneno haya mbele ya mwanamke japo kuwa ni matamshi rahisi ya kusema. Hapa si lazima uingie ndani ueleze sababu zako zote. Kumtamkia maneno kama haya yanatosha kwa mwanamke.

#7 Ni mrembo zaidi ya maumbile. Hapa unatuma ujumbe wakumwambia kuwa yeye kando ya kuwa ni mrembo kimwili, pia ni mrembo ndani yake. Mweleze kinjia ambayo hakutaleta kana kwamba ni mrembo kimaumbile pekee.

#8 Anakusisimua bila hata kujaribu chochote.  Hii ni silaha nzito unapaswa kuitumia kwa kuwa wanawake wengi hupenda kuskia matamshi kama haya. Wanawake wana hisia ndani zao so ukimtamkia maneno kama haya watahisi kujishasha/sifu hivyo wataskia vizuri ndani yao.

#9 Kama anataka kuongea uko tayari kumsikiliza. Hii inaweza kuonekana kama ni mambo ya friend zone lakini ukweli ni kuwa wanawake hupenda kusikilizwa na wapenzi wao. Hii inamaana kuwa uko tayari kutenga nafasi yako spesheli ili uongee naye. Atajihisi tofauti.

#10 Utakuwa karibu naye kwa shida na raha. Mwanamke anataka utumishi kutoka kwako. Kama una upendo ndani yako kwake, basi atahisi usalama, kukamilika na kupendwa. Hivyo baada ya kusoma hii post spesheli tulioiandika hapa Nesi Mapenzi, unapaswa kumtamkia maneno haya mpenzi wako.

#11 Unataka kusapoti ndoto zake. Wanawake huwa na ndoto zao katika maisha. Hivyo ukionyesha usaidizi wako kwake kutamfanya akuthamini na kukupenda zaidi. Usisahau swala hili muhimu katika mapenzi.

#12 Unamshukuru kwa kila kitu. Kuwa katika relationship lazima pia uwe unaeleza hisia zako kwa mpenzi wako. Na njia moja ya kufanya hivi ni kwa kumshukuru mpenzi wako kwa kila jambo ambalo ameweza kukufanyia katika maisha yako.

#13 Unataka ushauri wake. Wanawake pia hupenda maoni yao yasikilizwe kuhusiana na jambo fulani. So usichelewe kumuuliza ushauri mpenzi wako hata kama ni jambo dogo. Hilo hilo dogo litamfanya kuona unathamini uwepo wake.

#14 Mwambie kuwa una plan nzuri ya nyinyi wawili. Wanawake wangependa kuona kuwa wapenzi wao wanapanga mambo ya usoni katika maisha wakiwa wamehusishwa. Hili ni jambo muhimu ambalo wanawake wangependa kusikia wapenzi wao wakiwatamkia.

Ok. Upo!? Haya ndio baadhi ya mambo ambayo wanawake wanatamani kuskia kutoka kwa wapenzi wao hivyo unapaswa kuchangamka sahizi na kutafuta maneno ambayo yanawiana na mpenzi wako sahizi.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.