Jinsi Ya Kuzungumza Na Mwanamke Ili Umvutie


Kuongea na mwanamke ni rahisi. Unaweza kuongea na mwanamke yeyote ambaye unamjua ama uliekutana naye mara ya kwanza.


Lakini tatizo ni pale ambapo utahitajika kumfanya mwanamke avutiwe nawe. Hapa ndipo ustadi unahitajika ili ufanikishe mpango mzima. Si kila mwanaume anaweza kufanya maongezi mazuri hadi mwanamke avutiwe. Uzuri ni kuwa hapa Nesi Mapenzi tumekuletea mbinu ambazo unaweza kufanikisha mpango huu.

Hii hapa ndio njia rahisi ya kuongea na mwanamke ambayo itakusaidia kupata ujuzi kadri muda unaposongea.

#1 Usijaze mazungumzo yenu kwa kumsifu sana.
Kuna makumi ya wanaume katika nyanja hii ambao wanapenda sana kutumia maneno ya kumsifu mwanamke kama wameishiwa na maneno wakati wanapoongea nao. Wanaume wengine hufanya hivyo ili kudhihirisha kwa mwanamke kuwa wamevutiwa nao. Lakini makosa ni kuwa, kutumia maneno ya kumsifu mwanamke hayaongezi sana wala hayafanyi mengi kumsaidia mwanamke. Kwa hivyo, weka maneno ya kusifu kando, na uanze kuongea mambo mengine ambayo yatamvutia pia. Kama hutafanya lolote kando na kumwambia kuwa umemzimia kwa urembo wake au macho yake, utakuwa umejiweka level moja na wanaume wengine ambao wanatumia mitindo io kwa hio.
Kumbuka: wewe unawezekana kuwa si mwanaume wa kwanza ambaye umevutiwa naye. Mwanzo, kuna uwezekano mkubwa kuwa wanaume wote wanamuona kuwa anavutia. Hii inamaanisha kuwa kumsifu wewe kwake haitakuwa jambo geni kwake. [Soma: Jifunze jinsi ya kukutana na mwanamke mpya]

#2 Usijikite sana kuonyesha ya kuwa unamwona anavutia.
Kusistiza, ni kuwa haufai kuweka akili yako ijikite kuwa unamwona mwanamke unayeongea naye kuwa anavutia kupindukia. Ukijisahau tu ukianza kumfikiria vile ana urembo na kuvutia, utakuwa unajipa presha ambayo haitakuwa na manufaa yeyote kwa mazungumzo yenu. Kuna njia rahisi ya kuepuka jambo hili ambayo ni kuidanganya akili yako kuwa huyo mwanamke unayeongea naye hana urembo wowote ule. Presha ikishuka katika mwili wako, utajiona umepata fursa rahisi ya kuweza kujieleza ukiwa pamoja na mwanamke yeyote yule.[Soma: Jinsi ya kuwaambia aina tofauti tofauti ya wanawake uwatoe out]

#3 Tafuta mambo ambayo munagawa kimaisha.
Ok, haitakuwa jambo gumu vile mkianza kuongea mambo ambayo mnagawa ama intrest ambazo mnashare. Mwanzo kama mtaanza kuongea mambo ambayo mnagawa katika maisha, itakuwa ni njia rahisi ya wewe kuweza kupata namba yake ya simu ili kuweza kumshawishi kumtoa date.

Kumbuka: mwanamke akigundua kuwa mnashare intrest moja, hapo hapo atataka kuutumia muda wake zaidi mkiwa pamoja ili mpate kuzungumza intrest mnazoshare. Hivyo basi, fanya utafiti wa kina na ujaribu kuvumbua jinsi na njia utakayoitumia ili muweze kujumuika pamoja.[Soma: Makosa wanaume hufanya kwa mwanamke]No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.