Jinsi Ya Kumshawishi Mwanamke Mtandaoni

Kama kuna sehemu moja hapa duniani ambayo unaweza kujiachilia na kuwa wewe mwenyewe na kupata wanawake wakupende, bila shaka hio sehemu ni mtandaoni.
Hii ndio sababu kuu ya wanaume wengi kujiingiza katika Internet ili kujaribu mizare yao ya kuwavutia na kuwashawishi wanawake sikuhizi. Habari njema ni kwamba wanaume wengi hufanikiwa katika azma yao. Kuingia katika mitandao ya kijamii na kujaribu kuwashawishi wanawake inaweza kuwa jambo gumu kiasi na wakati mwingine likawa ni rahisi. Wengine hutumia fursa ya kutumia mitandao kama mazoezi ya washawishi mademu huku wengine wakifanikiwa kupata wachumba ambao wanakuwa nao katika maisha yao ya kawaida. Well, kama hujawahi kutongoza mwanamke online, ama unapata vigumu kutongoza then hapo chini kuna mbinu mwafaka ambayo itakuwezesha wewe kumtongoza yeyote yule katika mitandao ya kijamii kiurahisi.

1. Mtongoze
Kama maisha ya kawaida, kumtongoza mwanamke akiwa online ni lazima kama ibada. Itakuwa bora zaidi ukichanganya mitindo spesho ya kutongoza mara kwa mara, Mnyeshee kwa kumsifu siku moja halafu unakuwa mfidhuli siku nyingine. Jambo muhimu hapa ni utambue kuwa lazima unafaa kumfanya awe ametulia wakati unapochat nayeye. Pia lazima awe anajiskie yuko huru kabisa wakati mnapoongea. Hii itahakikisha kuwa anapenda na kufurahia kutaka kukujua zaidi na labda siku moja atatamani muweze kukutana ana kwa ana.

2. Tafuta maneno ya kwako
Usithubutu kutafuta mistari ya papo kwa papo kwani kawaida haifaulu katika mitandao. Kile unachohitajika kufanya ni kuhakikisha umepanga conversation yenu vizuri ili isiweze kukwama mbeleni. Pia hakikisha kuwa unaingiza maneno ambayo yataleta hisia za kucheka na furaha. Hii itamfanya amakinike zaidi na wewe.

3. Mfanye Acheke
Ok najua si kila mtu ana talanta ya kumfanya mwanamke yeyote acheke kama vile mzee Majuto lakini unafaa angalau utumie maujanja uliozaliwa nayo ili kumfanya mwanamke acheke. Nasema hivi kwa sababu wanawake wengi kawaida hupenda wanaume wacheshi. Ukitumia mbinu hii utamfanya akiwa offline ama online, fikra zake zitakuwa kwako.

4. Usimwambie kila kitu chako
Ukiwa unachat na mwanamke online, hakikisha humwambii kila kitu chako kwa wakati mmoja. Hakikisha ya kuwa kama mnachat unamfungulia moyo wako pole pole. Hii itamfanya yeye kuwa na shauku ya kutaka kukujua zaidi. Ukiweka baadhi za siri zako kikapuni, lazma ataingiwa na tamaa ya maswali hivyo kutaka kuongea na wewe zaidi na zaidi.

5. Kutana na yeye uso kwa uso.
Mwisho wa siku -baada ya kumtongoza na kumjua nje na ndani -unafaa kumuuliza kama atatoka out na wewe. Kumbuka hii ni level nyingine kubwa sana katika chat ya online hivyo kabla hujamuagiza mukutane uso kwa uso, lazima ujipange vilivyo. [Soma: Mitandao ya kutongoza mwanamke unayofaa kuijua kabla hujaoa]

Jinsi Ya Kumshawishi Mwanamke Mtandaoni Jinsi Ya Kumshawishi Mwanamke Mtandaoni Reviewed by Admin on 8:04 PM Rating: 5

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.