Mpenzi Wangu Hajibu SMS zangu, Jifundishe Kwa Nini Anafanya Hivyo


Jambo hili hutokea katika mahusiano. Aidha inaweza kuwa ni mwanamke au mwanaume anafanya hivi. Wapenzi wengi hupenda mara moja au nyingine kunyamaza au kukataa kujibu sms za wapenzi wao wakiwa na sababu zao wenyewe. Hapa Nesi Mapenzi kwa kawaida haipiti wiki bila kupata jumbe za kutaka kusaidia mtu kujua sababu za kwa nini hawajibiwi sms na wapenzi wao.


Leo tumeamua kuandika chapisho ambalo linaweza kuwapa wengi majibu ya haraka kujua kwa nini wapenzi wao hukataa kujibu sms zao.

So ukimuuliza unayemchumbia kwa nini amekataa kujibu sms zako kwa siku ya pili anaweza kukudanganya kuwa alipoteza simu, ama haikuwa na moto ama ilikuwa imepelekwa kwa fundi. Anaweza kukupatia sababu nyingi mpaka ukaingiliana, lakini kuna nyingine ambazo anakuficha, na zinaweza kuwa kama zifuatazo:

NB: Sababu hizi zinaweza kutumiwa kutatua swali hili la kutojibu SMS kwa mwanaume na pia kwa mwanamke.

#1 Mambo mengine hutokea.
Well, ukiona hajakujibu siku tatu mfululizo, usiwe na wasiwasi. Labda kazini kwake amekuwa busy sana. Labda alikuwa mngonjwa na alilazwa hospitali ama majanga mengine yalimtokea. Maisha huwa na changamoto zake wakati mwingine.

#2 Alijaribu kuwa mkarimu.
Wakati mwingine unaweza kukutana na wanawake ambao hawawezi kukuambia ‘sitaki’ mbele yako. Hivyo ule wakati ambapo ulimwomba namba yake ya simu hakuridhika na wewe, lakini alikupatia tu kwa ukarimu. Kisha baada ya siku mbili tatu umekuwa ukimtumia meseji na alikuwa akikujibu. Ukiona amekuzimia na hataki kukujibu, labda hii ndio sababu yake.

#3 Amepoteza hamu.
Labda umekuwa ukiwasiliana na yeye kwa wiki ama mwezi sasa. Lakini tangu mawasiliano yako ya mwisho ambayo ulipayuka maneno ya kuudhi, alipoteza hamu na wewe na ameamua kukunyamazia. [Soma: Tambua ishara za mwanamke anayekuchukia]

#4 Anatarajia kuwa utapata fununu.
Wanawake wanakuwa na tabia tofauti tofauti. Wengine watakuja mbele yako na kukuambia wamechoka na wewe na wengine wanaweza kutumia mbinu ya kunyamaza kupitisha ujumbe wao. Wakati mwingine ukimwona mwanamke amekunyamazia basi atakuwa anakutumia ujumbe wa kuwa hakutaki amechoka na wewe na anataka kuwa huru.

#5 Hayuko singo.
Mwanamke yeyote anaweza kukupatia namba yake ya simu, lakini hii haimaanishi kuwa yuko singo. Amekupatia hio namba lakini labda kuna wengine kama wewe ambao wako katika msururu wa wanaume aliowapa namba. Wakati wako ukiisha anakuzima tu. [Soma: Mambo ambayo mwanamke huangalia kwa mwanaume kabla kumpenda]

#6 Umeanza kuwa fala.
Wanaume wengine huwa mafala. Wakipewa nafasi na mwanamke badala ya kutumia nafasi hii vizuri wanaanza kubabaika na kuona kama dunia yote imepotea na amebakia yeye na huyu mwanamke. Utamwona anatuma meseji zaidi ya kumi mara moja bila ya kutoa nafasi ya kujibiwa. Anaanza kuingia kwa mitandao na kuanza kulike kila kitu chake na kucomment hata sehemu ambazo hazifai kwa profile yake. Mwisho wa siku utamwogopesha na atakuzima tu. Upo! [Soma: Makosa ambayo wanaume huwafanyia wanawake]


Je, imeanza kuingia kwa akili? Je, umepata sababu ambayo inakufanya mpenzi wako akuzime na asiweze kuwasiliana na wewe aidha kwa njia ya sms ama kwa simu? Na je, uko tayari kumfanya arudi aanze kuwasiliana na wewe? [Soma: Hatua za kufanya wakati mpenzi wako hataki kujibu sms zako]

1 comment:

  1. Ni fanye Nini Ndio boyfriend wangu anipigie simu tena

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.