Mambo 15 Mwanamke Huangalia Kabla Kukupenda - Mtizamo Kutoka Kwa Wanawake


Hebu tuseme ukweli, kuna wakati mwingine ambao wanaume wanashindwa kuwaelewa wanawake. Unaweza ukamwaproach mwanamke huku ukijua wazi hutatoboa lakini unashangazwa mwanamke kama huyo anakukubali fasta.

Na wakati mwingine utaapproach mwanamke ambaye unaamini kuwa ni rahisi kabisa kumtongoza lakini ukirusha nyavu badala ya kushika samaki inanasa mawe (sitaki kusema kinachotokea wakati mwanamke anakuzima mbele ya hadhira)

...halafu sasa kuna wale marafiki zetu ambao kila wakati wao wakitongoza wanakataliwa. (inauma sana)

Mapenzi ya mwanaume na mwanamke

Well, usitie shaka tena coz hivi karibuni kama Nesi Mapenzi tumekuwa tukitafiti kwa kuuliza wanawake ni mambo gani ambayo yanawavutia sana kutoka kwa wanaume na mambo ambayo yanaweza kuwafanya wafall in love na wanaume na haya ndio mambo ambayo waliyazungumzia sana:

#1 Kuvalia nadhifu
Kulingana na wanawake ni kuwa mwanaume anapaswa kuvalia nadhifu kila wakati. Hii ni muhimu kwa mwanaume kwa kuwa huwezi kujua ni wapi au lini unaweza kukutana na mwanamke wa ndoto yako. Ni jambo muhimu la kuzingatia lakini masikitiko ni kuwa ni wanaume wachache ambao huwa wanaona umuhimu ikija katika hili swala. Ok. ni hivi, kuanzia sasa hadi milele hakikisha kuwa unavalia kisafi na kinadhifu wakati wote, jipulize marashi na utumie bidhaa zote za wanaume ambazo zitakupamba.

#2 Kuwa na msimamo
Jambo ambalo wanawake wanachukizwa kutoka kwa wanaume ni kuona mwanaume ambaye hana msimamo thabiti. Mara leo anasema hivi mara siku nyingine yuko hivi. Well, hapa siongei kuhusu mwanaume ambaye mambo yake hayajulikani (mysterious) La. Naongea kuhusu wale wanaume ambao hawawezi kuwa na misimamo yao wenyewe. Akili zao haziwezi kujitegemea, hawezi kusema jambo mpaka aulize ushauri kwa wenzake ama kwa marafiki zake. So kama wewe ni mwanaume ambaye una tabia kama hizi ziache kuanzia sasa. Nataka ujeuke. Ukiwa na tabia kama hii hutatoboa katika kutongoza mwanamke.

#3 Mwanaume mwenye kuvutia
Mwanaume ambaye anajua kuvutia wanawake ni silaha nzito katika sanaa ya kutongoza. Wanawake wanapenda mwanaume yeyote ambaye ana chembechembe za kusisimua wanawake. Na mwanaume kama huyu ni yule ambaye ana uwezo wa kutumia miondoko ya mwili ipasavyo, wale ambao wanajua kutumia sanaa ya kubanta, na wale wanaojua kuzungumza maneno ya kunata. Upo? [Soma: Mbinu za kufuata uonyeshe kuwa una ushawishi]

#4 Mwili mzuri/shepu
Kama vile ambavyo ungependa mwanamke mwenye shepu na figa, pia wanawake wanapenda wanaume wenye shepu. So utafanyaje kama wewe una shepu la duara? Ingia gym, fanya mazoezi ya kukimbia angalau dakika 30 kila siku. Hii itakufanya uwe na toni nzuri kwa mwili wako. Si mimi ndio nimesema hivi, ni maneno kutoka vinywa vya wanawake. Anza mazoezi pindi utakapomaliza kusoma hii post.

#5 Kuwa na sanaa ya ucheshi
Mwanamke anaweza kujua iwapo mwanaume anachembechembe za ucheshi au la wakati ambapo anaongea naye. Ni hivyo tu ambavyo unahitajika kuwa navyo wakati kama unataka kumfurahisha mwanamke. Kila wanawake wanajua kwamba mwanaume ambaye ni mcheshi huwa anavutia sana haswa ikija katika maswala ya kudeti na wakati wanapochat nao kupitia kwa simu. Hivyo jambo lako la kufanya ni hakikisha ya kuwa wakati unapoongea na mwanamke unamchekesha. Usijilazimishe kama wewe si mcheshi. Mwanamke anaweza kucheka kwa mizaha ambayo hata haichekeshi kama umemsoma mambo anayoyapenda.

#6 Mwanaume ambaye halazimishi mambo
Mwanaume ambaye hulazimisha mambo huwa ni wanaume wanaochukiza zaidi ikija katika mchezo wa kudeti. Mwanaume wa kulazimisha ni yule ambaye anakubali kushindwa ili kuzuia mgogoro na mtu ambaye amemshinda kihadhi. Wewe kama mwanaume haupaswi kujidhalilisha mbele ya yeyote yule, hata kama ni marafiki zako. Kuwa na misimamo yako mwenyewe katika maisha yako. Kama unaona kuwa unakosewa una haki ya kupaza sauti yako usikike  balada ya kukasirika ama kusinyaa.

#7 Kazi nzuri na hela ndefu
Ok. Haya si maoni yangu. Ni mambo ambayo yametamkwa kutoka kwa vinywa vya wanawake. Lakini ngoja tuseme ukweli...pesa ni muhimu ikija katika maswala ya mapenzi. Ni hivi! Wewe hupenda wanawake warembo zaidi kuliko wanawake wabovu. Kweli? Hivyo hivyo wanawake hupenda wanaume ambao ni matajiri zaidi kuwaliko wale maskini. Kuwa tajiri na kuendesha gari la kifahari ni advantage kwako (usitie wasiwasi, haya ni maoni ya wanawake tu. hapa Nesi Mapenzi tushalizungumzia tatizo hili mara kwa mara, pesa si muhimu katika kutongoza, ushapu wako ndio muhimu)

#8 Mwanaume ambaye anaheshimiwa na wengine
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawaheshimu, lakini pia wanapenda kuwa na wanaume ambao wanaheshimiwa na wengine. Kama kuna mtu hakuheshima, hayo ni makosa yako? Kama ni yako basi hakikisha kuwa unatatua. Lakini kama si makosa yako basi si lazima ujihusishe nao. Simama wima na utetee haki yako ya kuheshimiwa na kila mtu. Tumeelewana?

#9 Mwanaume anayejiamini
Kuwa na confidence ni muhimu kwa kila mwanaume. Ni nguvu ya kuzimu ambayo kila mtu utakayekutana naye atakuonea gere. Mwanaume anayejiamini huwavutia wanawake kwa kuwa anajiamini yeye mwenyewe pamoja na uwezo wake wa kuyaona mambo jinsi yalivyo ulimwenguni. [Soma: Hatua za kujiamini]

#10 Mwanaume anayeonekana vizuri
Huku ni kuanzia kule kujiweka kimwili. Vile ambavyo unasimama kama mwanaume. Je mapozi yako yakoje? Je unavalia nguo kulingana na mwili wako? Wakati unapoongea unazungumza na ishara zipi? Haya yote ni baadhi ya mambo ambayo  ni muhimu na yanayowafanya wanawake wakutambue kama wewe ni mwanaume bora wa kumchumbia au la.

#11 Mwanaume anayejua kuzungumza
Kama tu vile kujua jinsi ya kutumia ucheshi katika mazungumzo yako, kujua jinsi ya kuzungumza na mwanamke kwa kutumia Sanaa ya Mazungumzo kama vile banta, miondoko ya mwili na kuchanganya Programu ya Isimu Ubongo ni muhimu zaidi kwa kuwa kutamfanya mwanamke kujiskia huru zaidi akiwa na wewe na ni mambo ambayo mwanamke anatamani kutoka kwa mwanaume yeyote. Sanaa zote hizi ziko kwa kitabu cha Kutongoza Mwanamke: Kuanzia Hadharani Hadi Kitandani

#12 Tabia ya kuheshimu
Kuwa na tabia ya kuheshimu wengine vile inavyotakikana. Wanawake wote wazuri hawawapendi wanaume ambao wanapenda kuwachukulia vibaya wengine. Usiwe mbaya kwa watu walioko chini yako bila ya kuwa na sababu yeyote. Ukiheshimu wengine nao pia watakuheshimu. Wanawake huwaona wanaume wenye tabia ya kuwaheshimu wengine kuwa wanaweza kuwa wazazi wazuri. So hakikisha kuwa unatabia nzuri wakati wote.

#13 Kuwa mwanaume alpha
Wanawake wazuri huwa kwa mikono mwa wanaume bora. Hakuna mwanamke atataka kuwa na mwanaume mwoga, asiyejiamini, asiyeheshimu wengine. Itakuwa ushawahi kugundua kitu flani, kwa kawaida huwa kuna mwanaume mmoja katika kikundi flani ambapo yeye anadeti wanawake warembo zaidi ilhali wenzake wanadeti wanawake wa kawaida. Wanaume kama hawa ndio huitwa alpha. [Soma: Hatua za kujijeuza Alpha]

#14 Mfanye ajihisi huru
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawafanya wajihisi huru wakiwa nao. Hii ni kulingana na usemi kutoka kwa wanawake. Hivyo kama wewe unakuwa na tabia za maswali yasioisha, ukali, woga ama kutojiamini basi utamfanya mwanamke ashindwe kujiskia comfortable akiwa na wewe. Jambo la kuhakikisha ni kuwa unautoa wasiwasi wowote ambao unaweza kujitokeza wakati unapoongea na yeye.

#15 Mwanaume mwenye usambamba/ compatibility
Ok. Tatizo kuu linajitokeza hapa. Mara nyingi mwanaume anaweza kumpendeza mwanamke kwa kila kitu lakini mwanamke anaweza asikubali mwitikio wako kwa kuwa hamna uwiano ulio sawa. Mwanamke anaweza kukukataa kwa sababu zake binafsi. Kama unataka kufanikiwa na hili basi hakikisha kuwa unakuwa mkweli, makinika na interests zake na usome mambo anayopenda na kuchukia. Kama ataona kuwa kuna uwiano ndani yenu, basi ni rahisi kwa yeye kukukubali.

Mwisho ni kuwa haya ni maoni ambayo yametoka kwa vinywa vya wanawake, hivyo kama kuna moja kati ya haya maoni 15 tuliyoyaorodhesha unayakosa, basi ni muhimu uanze kazi sasa hivi.

Mafanikio Kwako.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.