Sababu 5 Za Kutongoza Wanawake Ufuoni Mwa Bahari


Ok. Inaweza kuonekana jambo la kufurahisha, lakini katika Nesi Mapenzi, tunaona ya kuwa ufuoni mwa bahari ni sehemu moja nzuri zaidi ya kukutana na wanawake wapya. Kama unaishi karibu na ufuo wa bahari halafu hujajishughulisha kutafuta mchumba huko basi ni wakati wako wa kufikiria mara ya pili: Tumia muda wako vizuri kwa kumakinika na kuapproach wanawake sehemu hizo na utakuja kugundua kwa nini tunasema kuwa beach ni sehemu moja muhimu ya kuapproach wanawake.


Na kwa kusistiza msimamo wetu, tumekuja na sababu zifuatazo:

1. Kunafurahisha
Hakuna njia mbili kuhusiana na swala hili: Ufuo wa bahari huwa ni sehemu inayofurahisha. So wakati ambapo unaanza kuongea na mwanamke katika ufuo wa bahari, nafasi kuu zaidi ni kuwa tayari anaenjoy muda wake katika sehemu hio. Hii inamaanisha hakutakuwa na haja za kuziondoa hisia zozote hasi. Atakuwa anafuraha, mcheshi, anajienjoy, na pia itakuwa rahisi kwake kukusikiliza kwa urahisi kwa sababu muda wote amejawa na furaha. Katika ufuo wa bahari ni rahisi sana ukilinganisha na maktabani, gym ama hata katika mkahawa. So tumia hii nafasi inayojitokeza.

2. Unakuwa mchangamfu
Ok. mtakubaliana nami ya kuwa hakuna mtu atajipeleka kwa ufuo wa bahari kama hana kitu cha kufanya. Kwa kawaida mtu akienda beach huwa lengo lake kuu ni kuogelea, hujumuika na marafiki zake, kucheza mpira, kukimbia ama jambo lolote lile ilimradi tu aonekane yuko mchangamfu na shughli flani. Kumhusisha mwanamke katika shughli zako ni njia muhimu na ya kwanza kuchukua ili uweze kumfahamu zaidi. Bora zaidi ni kama unafanya beach party, unaweza kumualika kwa marafiki zako. Cha zaidi ni kuwa wakati ambapo unaonekana mchangamfu, pia unaonekana bora, jambo ambalo ni muhimu.

3. Ni sehemu ambayo wanawake hupenda
Kila mtu anajua ya kuwa sehemu za ufuo wa bahari kuna wanawake wengi zaidi kuliko sehemu zozote zile ambazo zinajulikana. Kama unataka kukutana na wanawake basi ni lazima uende katika zile sehemu ambazo wanapatikana. So bila kupoteza wakati wako unafaa utembelee sehemu hizi haswa beach ambayo uko karibu nayo uweze kutangamana na wanawake tofauti tofauti.

Halafu alama muhimu hapa ni kuwa katika beach kwa kawaida wanawake huwa wamevalia bikini na vinguo vya kuogelea. So kama unatafuta sehemu ya kutafuta wanawake, hata si jambo la kutumia ubongo. Hivyo basi mbona hujaenda kwa beach tayari?

4. Hisia zako zinakuwa juu
Uko mchangamfu, unaangazwa na jua la ufuoni na unajienjoy. Kuna nafasi gani nyingine unangojea upewe ili uongee na wanawake? Sehemu kama hii unapaswa uonyeshe hisia za juu, ujihisi bingwa na kufurahia wakati unapoongea na wanawake. Kama wewe ni mwanaume ambaye unapenda beach halafu unapenda maji, hakuna njia mbili za kuchagua, lazima uende baharini na uanze kukutana na wanawake wapya, sehemu ambayo itainua hisia zako.


5. Ni romantic
Labda maswala ya romantiki huna lakini yeye akawa nayo. Huu hapa ni uzuri wa romantic ambazo zinajikuza kutokana na mapenzi ya baharini: ni kuwa neno 'Nimefurahi kukutana na wewe" litajeuka kuwa "nataka kukujua zaidi" hadi likawa "nakumbuka ule wakati tulipokutana mara ya kwanza...".

Hakuna sehemu nyingine yeyote ile ambayo unaweza kuwa na nafasi ya kuupiga jeki uhusiano wako na mwanamke ambaye umekutana naye kidharura isipokuwa katika ufuo wa bahari. [Soma: Siri za kumvutia mwanamke]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.