Siri 4 Zinazofichwa Za Jinsi Ya Kumvutia Mwanamke


Kuna mbinu nyingine za kumvutia mwanamke ambazo haziwekwi hadharani kwa kila mtu kuzijua. Na hata kama ulikuwa ukizijua ni kuwa ulikuwa hutambua manufaa yake kwako hivyo ulikuwa ukizitumia vibaya. Mfano leo kama ungekuwa unazijua mbinu zote mwafaka za kumfanya mwanamke atamani kila kitu kutoka kwako si ingekuwa balaa?


Post ya leo tumeamua kukuandalia mbinu ambazo ukizitumia vizuri bila shaka itakuwa ufunguo wa kwako kuweza kulazwa na mwanamke yeyote yule.

Zama nami!

Siri za kumfanya mwanamke akupende

1. Kuwa na hadhi ya juu kijamii
Ushawahi kugundua vile watu matajiri na watu wenye hadhi ya juu huwa na maongezi na swaga ambazo huonyesha mamlaka? Watu aina hii huonyesha dhamana na hadhi ya juu kiasi cha kuwa hawaogopi kuonyesha hisia zao kwa mwanamke wala kuingiwa na wasiwasi wa kuwa wanaweza kukataliwa.

Wakati mwanamke anapokutana na mwanaume mara ya kwanza, hapo hapo hutoa uamuzi akilini mwake iwapo atalala na yeye au la. Kiujumla, haswa kwa wanawake warembo, huwa na nadhari iliyojengwa akilini mwao kwa vitu wanavyothamini. Vile ambavyo atakavyokukufikiria ndivyo atakavyokuchukulia kama thamani yake kwako. 

Kiufupi ni kuwa, wanawake huvutiwa na wanaume ambao wamepita thamani yao ambayo wamejiwekea. Hapa ndipo unapofaa kutumua nguvu za kijamii kukuongezea hadhi yako katika jamii.

Kuna njia tofauti tofauti za kufanilisha hivi. Njia rahisi ni kuhakikisha ya kuwa watu wanakuzungumzia na kuongea kuhusu mambo ambayo umefanikiwa kufanya ama kutimiza. [Soma: Jinsi ya kuipandisha hadhi yako kwa mwanamke]

2. Ujuzi wa kuwasiliana
Ok. Ushaongea na mwanamke kwa njia ya kumridhisha bila kuchekwa. Kila kitu kinaenda sambamba mpaka inafikia mahali flani unaishiwa na maneno ya kumwambia.

Ghafla, unamwona akikuangalia kwa matumaini, akitaka uendeleze na gumzo lakini unashindwa. Unabakia ukijiuma midomo na kujikuna kichwa huku ukimwona mwanamke aina hii akikutoka viganjani mwako na kuchukuliwa na mwanaume mwingine aliekaa pembeni. Situation kama hii inaumiza bila shaka.

Sababu kuu ambayo inawafanya wanaume wengi washindwe kuongea na wanawake ni kuwa wanaishiwa na mawazo ya kuongea. Ni muhimu kukumbuka ya kuwa katika mchezo wa kutongoza maongezi yako ni kama bango la mauzo kwa mwanamke. Hii ni kumaanisha kuwa kando na kuwa unajua kile ambacho unaongea, unafaa ujue jinsi ya kumudu na kuendeleza mazungumzo mazima.

Wakati unapomsuka mwanamke una muda mchache kabisa wakujifanyia mauzo. Hivyo ni muhimu zaidi upange hoja zako vile ipasavyo ili mwanamke akitoka hapo asiweze kukusahau kiurahisi. Na kufanikiwa kuujua ujuzi kama huu hauwezi kuja na siku moja, lazima ufanye mazoezi ya mara kwa mara mpaka ujeuke gwiji.

Kuongea na watu tofauti tofauti kutakusaidia kujenga confidence ambayo itakurahisishia kuongea na mwanamke wakati ambapo utakumbana naye. [Soma: Jinsi ya kuongeza ujuzi wa kuwasiliana]

3.Kuidhibiti miondoko ya mwili
Kulingana na utafiti wa kisayansi, binadamu huwasiliana asilimia 93 wakitumia miili yao na asilimia 7 kwa kutumia maneno. Ni muhimu kumakinika na kuelewa miondoko yako yote wakati ambapo unazungumza na yeyote yule.
Jitenge na tabia ya kuikunja mikono yako ama kujikunja kunja kwa sababu hio ni ishara ya kumwambia mwanamke akuondokee ukae pekeako. Na ukiendelea na tabia kama hii itakiwa kitu cha kwanza ambacho atakinotice wakati mumetoka deti.

Badala yake, tumia miondoko ya mwili ambayo inafahamika na kila mtu. Mfano ni kuegemea mbele wakati ambapo unaongea, kuifumbua mikono yako na pia kuweka pozi ambalo linaashiria kupumzika. [Soma: Matumizi tofauti ya miondoko ya mwili]

4. Kufanikiwa kiubora
Si jambo la kushangaza kwa wanawake kuwaona wanaume ambao wana ubora flani katika nyaja kama vile muziki, michezo, sanaa nk kuvutia kwa hali ya juu. Wanaume aina hii huwa wamejikuza na stadi zao kiasi cha kuwa wamebobea kwayo.

Ok tunajua ya kuwa ni kweli hauwezi kuwa mtajika kama vile Emmanuel Adebayor, lakini unaweza kutajika kwa maswala madogo madogo katika fani flani unayoipenda. Labda wewe ni bingwa mtajika katika gemu ya karata ama labda wewe ni kapteni wa timu yako ya raga nk.

Kulingana na shauku yako yeyote unayopenda, unaweza kumjulisha mwanamke kimtindo flani bila kujifanya kana kwamba unajipa sifa kujipendekezea. [Soma: Mambo hupaswi kumwambia mwanamke]


La mwisho ni kuwa hizi ni baadhi ya mbinu ambazo unafaa kuzijua na kutimiza kama unatumaini kuwa na mafanikio ya juu kwa mwanamke.


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.
##valentine ##valentine