Tambua Kama Mwanamke Anakupenda Kwa Kuangalia Miguu Yake


Hebu fikiria situation ambayo unaongea na mwanamke mrembo. Unamskiliza kila kitu anachozungumza... Unamwangalia jinsi vile midomo yake inavyojishepu wakati anapoongea maneno flani, na kumakinika na umbile lake kila wakati anapotaja maneno fulani na pozi tamu.

Fikiria sahizi unatatizwa kumakinika na vile anavyounembua mwili wake... vile anavyokaa... na jinsi anavyokunywa kinywaji chake mbele yako...

Lakini haya yote yakiendelea, unaongea na yeye bila kusitasita wala kubabaika, bila kuonyesha ishara yeyote ya kuwa umbo lake linakuchanganya akili. [Soma: Jinsi ya kuzungumza na mwanamke]

Utakuwa unadhania ya kuwa unaelewa kila kitu ambacho anatamka kutoka kwa mdomo wake. Kama unaamini hivyo, basi fahamu ya kuwa unajidanganya.

Wanaume wengi hudhania ya kuwa wanaweza kuelewa maneno yote ambayo yanatamkwa na wanawake. Lakini ukweli ni kuwa ni chini ya asilimia 20% ambayo wanawake wanasema ambayo wanaume wanaweza kuelewa.


Ok twaweza kusema kiujumla kuwa wanawake ni kama viumbe ambao wanatoka katika sayari nyingine kwa mtazamo wa mwanaume yeyote.

Lakini kuweza kuwaelewa wanawake angalau kwa asilimia 50% utafanyaje?

Soma miondoko yake ya mwili aka body language:
1. Jinsi wanavyojitandaza
2. Vile mapozi yao yako
3. Jinsi 'wanavyoitumia' miili yao kwa ujumla

Kwa mwanaume yeyote ambaye yuko serious kutaka kutongoza mwanamke yeyote, lazima awe na ujuzi wa kuisoma miondoko muhimu ya mwanamke ambayo inaashiria iwapo amevutiwa kwako au la.

Katika kufafanua zaidi, post hii tumeiandaa specially kuonyesha iwapo mwanamke anakupenda au la kwa kuangalia sehemu moja kuu kutoka kwake....

Zama nami...

Kuangalia miguu ya mwanamke kama anakupenda au la

Ni rahisi kudhibiti vile sura yako unataka ionekane. Kwa kutumia uso unaweza kuleta mitazamo tofauti kabisa na vile ambavyo unajihisi. Sura yako inaweza kushawishi kwa kudanganya, kutabasamu mbele ya kamera nk. Hata hivyo, kadri unaposongea mbali na uso wako, inazidi kuwa vigumu kuudhibiti mwili wako kwa ujumla.

Hii ni kumaanisha kuwa miguu (nyayo) ni kiungo muhimu cha kutumika kung'amua maswala ya kuvutiwa kimapenzi katika mwili wako mzima.

Halafu uzuri wake ni kuwa ni rahisi kuichambua. Kimsingi ni kuwa kila mtu hutumia miguu yake kuelekeza kitu ambacho anapendezwa nacho. So, iwapo unadhania ya kuwa unazungumza mazungumzo yanayovutia na mtu kwa kuwa anatabasamu na kucheka...

...halafu uje ugundue ya kuwa miguu yake hailengi kwako bali kwa mlango wa nje ...utajua ya kuwa hautakikani hapo.

Binadamu hutumia miguu yao kama vile wanavyotumia mabango ya ishara kuelekeza kitu ambacho wanataka. Sheria hii unaweza kuitumia vizuri katika maswala ya kudeti na kutangamana na wengine.

Wataka kujua kama mwanamke amevutiwa na kupendezwa kwako?
Fanya kuiangalia miguu yake mnapoongea. Miguu ambayo inalenga upande wako ni ishara dhabiti kuwa anapendezwa na wewe (kama hatakuwa akiisongeza mara kwa mara)

Vile vile, kama mguu wake ama miguu yake inalenga kwingine ama atakuwa akichezacheza na viwiko vyake vya mguu ni ishara ya kuwa hajapendezwa nawe, ama anataka kuondoka hapo mara moja.

Upo!? [Soma: Siri zilizofichwa jinsi ya kumvutia mwanamke]No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.