Mbinu 5 Tofauti Za Kumwomba Mwanamke Namba Ya Simu


Je ushawahi kujaribu kumwomba mwanamke namba yake ya simu ukashindwa?


Je umejaribu kutumia mbinu uliyojifunza kuomba namba ya mwanamke lakini hukufaulu? Ama ulifaulu lakini mwanamke amekataa kujibu sms zako?

Mbinu 5 Tofauti Za Kumwomba Mwanamke Namba Ya Simu

Well, tumekuja na mbinu mwafaka ambazo zitakufanya wewe upate namba ya mwanamke haraka na aweze kujibu texts zako siku ya pili ambapo utaamua kumtumia meseji.

Wanaume wengi huingiwa na woga ikifikia wakati wa kuomba namba kutoka kwa wanawake. Haufai kuogopa na jambo hili. Mwanzo nataka nikuonyeshe njia za kumwomba mwanamke namba na pia nikuonyeshe umuhimu wa mbinu moja muhimu kati ya hizi. [Soma: Makosa unayoyafanya kwa SMS ambayo wanawake hukucheka]

Mbinu za kumwomba mwanamke namba ya simu.



Hizi ni hatua tano ambazo zitakurahisishia kazi yako ili upewe namba kutoka kwa mwanamke haraka sana.


1. Wajua nataka kwenda, lakini nilikuwa nataka kukujua zaidi.  Waonaje nikupigie simu kesho?

Makinika hapa ya kuwa sijasema "nitakupigia simu siku flani" bali nimesema "kesho". Mwambie utampigia simu halafu umuulize umpigie saa ngapi. Njia hii inakupa nafasi ya kujui iwapo amevutiwa na wewe au anakupotezea wakati. [Soma: Hatua za kupata girl friend mpya]

2. "Hey, wajua nataka kwenda lakini nataka kuendeleza maongezi yetu. Waonaje tukutane siku ya ____saa ____?"

Kuweka deti ya siku maalum ni njia nzuri ya kuomba namba kutoka kwa mwanamke. Fahamu ya kuwa umeweka deti yenu sehemu maalum. Hivyo anaweza kuamua kama mtakutana ama kutafuta sehemu nyingine mwafaka. Usitumie maneno kama "wakati mwingine" kwani itaonyesha dalili ya kutojiamini ama kuonesha woga kiasi flani. [Soma: Hatua za kumteka nyara mwanamke kimapenzi]


Hizi hapa ni njia za moja kwa moja za kuomba nambari ya mwanamke:


3. "Hivi unatumia simu aina gani?" Atakujibu "Mbona wauliza?" Mjibu "Sababu nlikuwa nataka unipatie namba yako."



4. Mpatie simu yako halafu umwambie "Nataka kwenda lakini waonaje kesho tuendeleze gumzo letu?"


Hii mbinu ya mwisho ni nzuri ya kutumia kumwomba mwanamke namba yake kwa sababu unakwepa kutumia maneno kama: "Naomba namba yako ya simu" [Soma: Jinsi ya kutongoza kimwili]


Hili ni jambo kubwa sana kwa kuwa kawaida mwanamke huandamwa na wanaume wengi asiowapenda ambao wanamuuliza namba zake. Hivyo pindi utakapotumia maneno "Naomba namba yako ya simu" anaweza kukufananisha na wanaume wale wa kawaida asiowapenda ambao kila wakati wanapenda kumwomba namba yake ya simu.

Lakini pindi ambapo utampatia simu yako utakuwa umeashiria mambo mawili: Kwanza atakuwa ameelewa jambo ambalo unataka kutoka kwake bila kutumia maneno "Naomba namba yako ya simu" [Soma: Ishara za kuonyesha kama mwanamke amevutiwa kwako]

Pili ni kuwa unajenga dhana ya uaminifu kwa akili yake. Kumpatia simu yako mwanamke kunaleta dhana ya uaminifu ambayo ni jambo muhimu kwake. Simu yako ni kifaa chako binafsi na ni faragha yako, lakini pindi ambapo utamruhusu mwanamke kuishika kutaonyesha ya kuwe wewe si mtu mfiche. Mwanzo kulingana na utafiti uliofanywa na wanasaikolojia ni kuwa kupatia simu yako kwa mwingine ni ishara ya uaminifu.


Pia kupatiana simu yako ni kuonyesha kutaka mwenzako akuamini zaidi. So waonaje wewe uitumie mbinu hii ya kuomba namba ya simu kwa njia ya urahisi? [Soma: Mitandao maarufu Afrika ya kupata wachumba papo hapo]





2 comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.
##valentine ##valentine