Makosa 5 Ya SMS Ambayo Unamfanya Mwanamke Akucheke


Kila mtu hutumia SMS kila siku kuwasiliana.

Kama inavyotambulika ni kuwa ni rahisi sana kutumia jumbe fupi kuwasiliana na mwingine kupitisha ujumbe. Lakini je huo ujumbe unaoutuma unachukuliwa vipi na unayemtumia?


Katika swala la kutongoza ama kumSMS mwanamke, wanaume wengine wanafanya makosa makubwa wakati wanapochat bila wao kujua. Jambo ambalo nimeamua kuliweka wazi. 

(Kwa bahati mbaya ni kuwa makosa haya yanafanywa na wanaume kila wakati)

1. SMS za kujisifu
Kosa hili nishawahi kulizungumzia mara kwa mara kwa blog hii, na ni wanaume wengi sana wanapenda kulifanya. Najua waelewa nazungumza kuhusu nini. Kuongea stori za kirare (na 85% ya ufala) ambazo unajaribu kumwonyesha mwanamke jinsi ulivyo burudi, kumwonyesha kuwa una marafiki wazuri ambao wanaweza kukufanyia chochote kile utakacho, na kuwa huwa unatembea sehemu tofauti tofauti za kifahari kwa kuwa umefanikiwa na una umuhimu mkubwa katika jamii.

Kwa maneno ya urahisi ni kuwa unajaribu kadri iwezekanavyo kumpendeza mwanamke.

Mwanamke wako mwenye hadhi atayaringa macho yake na kucheka kimoyo akianza kuhisi kama unafanya hivyo kumpendeza. Kwa nini? Kwa sababu unajaribu kutumia mbinu hio kumfanya akupende. Ni wakati wako wa kuacha kutumia mwanamke meseji kama hizi.

2. Kuwa na mapepe
Kumualika mtoke deti pamoja kabla ya kutumia mbinu ya kumtongoza ili akukubali. Hakuna njia nyingine nzuri zaidi ya hii kudhihirisha kuwa wewe:
(a) una experience ndogo ya kutangamana na kuwajua wanawake (b) hauna ladha ya maana kuchagua wanawake

(PssS: Kama kujuana kwenu kulikuwa kwa nishati, unaweza kuipuuza hii)

3. Kupumbazika kwake
Unamtumia mamia ya text za ucheshi, unamsuka, unamwelezea stori za ovyo ovyo za abunuwasi na nyingine, na unazidi kumtumia sms za 'kumvutia' zaidi --mpaka inafikia mahali flani unamboa na anaanza kukupuuza.

So imekuwaje mpaka ameanza kukupuuza? Umempandisha mzuka wa kukupenda halafu ukapoesha kila kitu.

Wanawake wanadhania ya kuwa mwanaume ambaye anaonyesha interest kwao halafu hataki watoke deti pamoja huwa ni mwoga wa kuchukua hatua ya mbele.

4. Kuharibu tenshen
Unafafanua jokes zako kuhakikishia ya kuwa anaelewa kile unachomaanisha. Unajihisi haujiskii vizuri kama hujibu texts zake, kwa sababu hutaki aone kama unampuuza. Kama anakataa na kitu flani, unanyenyekea na kukubaliana na kila atakachosema.

Hii inaonyesha ya kuwa wewe si mwanaume dhabiti, kwa sababu hauwezi kuhimili tenshen, na mbaya zaidi ni kuwa unaogopa kumpoteza.

5. Mambo yakienda mrama
Wakati ambapo amekataa ama kusimama kureply text zako, unaanza kutoa kucha zako za ujinga na ''kumweka sehemu anayostahili''

Unaanza kumwambia jinsi alivyo mbovu, anatisha, ni zuzu ama mpotezea watu wakati, ama ni mwanamke mwenye hadhi ya chini na unaweza kufanya zaidi. (Kwa mwanamke atakuwa akifikiria, ''Ha ha, haukuwa unasema hivyo dakika mbili zilizopita ulipodhania una nafasi kwangu'')

Okay...

Najua kuwa text zako ni za level ya juu wakati unapomtext mwanamke, na naamini hauwezi kufanya makosa tuliyoyaeleza hapo juu. Lakini tukiwa waadilifu ni kuwa tunaweza kukubali kufanya kosa moja au lingine katika haya.


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.