Sababu 3 Kuu Ambazo Zinakufanya Ushindwe Kumtoa Mwanamke Deti


Acha tuwe waadilifu kiasi...

Baadhi ya wengine wetu  wanashindwa kupata deti na mwanamke.

Baadhi ya wengine wetu wanaweza kupata deti mara ya kwanza lakini wanashindwa kupata deti ya pili.

Wengi wanadhania ya kuwa si makosa yao - eti ni makosa ya mwanamke mwenyewe.

"Nilimwita tukatoka deti mara ya kwanza, nilipomwambia tutoke deti ya pili alikataa. Sijui tatizo liko wapi"

So tatizo huwa linajitokeza wapi?


Kulingana na tafiti tulioufanya katika blog hii, tumekuja na sababu tatu kuu ambazo zinachangia wengi kushindwa kutoka deti na mwanamke mara ya kwanza au mara ya pili.

#1. Haujitayarishi kutengeneza deti ya pili wakati ambapo deti ya kwanza bado haijakamilika. Pia itakuwa hujamsisimua vizuri kuhusu wakati ambapo mtakutana tena katika deti ya pili.

Ok mpango mzima huwa hivi, iwapo unataka deti ya pili na mwanamke itendeke, lazima umwelezee na mapema kuhusu deti yenu ya pili. Pia iwapo unataka deti ya pili na mwanamke lazima umsisimue kuhusu deti yenu ya pili, mfano unaweza kumdokezea kuhusu mambo ambayo unatarajia kumfanyia mtakapo kutana mara ya pili nk.

#2. Itakuwa haujitahidi kuwa wewe mwenyewe. Itakuwa unababaika na kuwa na wasiwasi wa kutaka kuhakikisha ya kuwa husambaratishi deti yako naye, jambo ambapo linafanya deti yako na mwanamke kuharibika.

Kwa kawaida mwanamke hupenda mwanaume ambayo yuko wazi, mwenye nishati na pia hisia. Hivyo ni rahisi sana kwa mwanamke kutambua iwapo mwanaume ameingiwa na wasiwasi ama uoga.

#3. Hausikilizi kile ambacho anasema. Tatizo hili humkumba mwanaume wakati ambapo anajaribu kufikiria sana kuhusu mambo ambayo anataka kumuuliza ama kumjibu mwanamke ili kutafuta vitu mnavyohusiana pamoja badala ya kumakinika na kumsikiliza mambo ambayo anayasema.

Ok... kwa kifupi ni kuwa hizi sababu tulizozieleza hapo juu huchangia kwa mwanaume kushindwa kuzuia deti kwa mara ya kwanza kwa mwanamke au kwa mara ya pili.

Kama umetoka deti na mwanamke kwa mara ya kwanza, sioni tatizo la kwako kushindwa kutoka naye deti mara ya pili, tatu, nne na hata ya tano na mwanamke unayemfukuzia.

Kile unachopaswa kuzingatia ni kuangalia vile ambavyo unawatendea katika deti, ujanja wako wa kutumia mbinu kadha wa kadha za kuwashawishi, na cha msingi ni vile ambayo utamakinika kutaka kujua vitu ambavyo mwanamke anataka katika deti.

Upo!?

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.