Dalili Za Kuonyesha Kama Imefika Kumkiss Mpenzi Wako


Lazima uwe mjanja wa kusoma ishara zote kabla hujachukua hatua ya kujaribu kum kiss ama kumla dende mpenzi wako.

Ukijifanya fala wa kuchukua hatua ya haraka kumkiss mpenzi wako kwa mara ya kwanza bila kusoma ishara dhabiti inaweza kukuletea aibu, ama zaidi kukufanya upungukwe na kujiamini kwako wakati mwingine ambao mtakutana tena.

So utafanyaje usipate aibu ama kupungukiwa na kujiamini?


Jambo la msingi ni kuwa lazima nyote wawili muwe mumevutiana aidha kimapenzi ama kuna kemia ya kimahaba ambayo imejijenga kati yenu. [Soma: Njia tatu za kujenga tenshen ya kimapenzi]

Ok. Kuna wengine wangepinga msimamo wangu wa hapo juu ya kuwa si lazima kuwe na mvuto wa kimapenzi kati yenu... Jibu langu ni rahisi. "Unless nyote wawili mumekutana kwa kilabu ama sehemu nyingine na nyote wawili mumeathirika kwa kubugia bia nyingi, haitakuwa jambo zuri kama utachukua hatua ya kumkiss yeyote...mwanzo kumkiss mtu ambaye humjui vizuri kunaweza kuwa matatizo chungu nzima"

So ina haja gani ya wewe kumkiss mtu ambaye humjui? Mbona usimkiss mtu ambaye tayari umemzoea na ambaye kuna tenshen ya kimapenzi kati yenu?

Hoja hii ndio imenifanya nije na:

Dalili za kuonyesha kama imetimia kumla dende mpenzi wako

1. Kabla siku yenu ya kukiss iwadie lazima muwe mumekumbatiana mara kwa mara, mumeweza kugusana na kutomasana sehemu tofauti tofauti hasa kwa mikono, shingo, viganja ama sehemu yeyote ile ambayo nyote wawili mumeona ni sawa. Iwapo hamjawahi kufanya hatua hata moja kama hii, ni bora zaidi usijaribu kuchukua hatua ya kukiss kwani itakujeukia wewe mwenyewe. [Soma: Hatua za kumpapasa mwanamke kiujanja na akukubali papo hapo]

2. Kabla hatua ya kukiss haijawaidia, kwa kawaida inatoa wakati ambapo nyinyi wawili mnakaribiana kimwili kuliko kawaida yenu. Mara nyingi wapenzi wawili huanza kugusana mikono, viganja, mgongo au wakati mwingine miguu.

3. Wakati ukifika nyinyi wawili mtakuwa mkiangaliana sana kwa macho huku mkipuuzia mazingira ambayo yamewazunguka. Hatua kama hii ikifika usipoteze muda zaidi. [Soma: Njia za kumshawishi mwanamke kwa kutumia macho]

4. Wakati mwingine ghafla maongezi yenu yanasimama halafu mnaanza kuangaliana machoni kwa muda mrefu kuliko kawaida. Ijapokuwa maongezi yenu yatakuwa yamesimama, hamtaona jambo lolote la kutatanisha bali mtakuwa mnaskia raha na mnavutiana zaidi.

5. Wakati huo mtakuwa mnajiskia mko na raha, na mnaweza kuwa mnacheka sana ama mnatabasamuiana nyote wawili. Ukiona hatua kama hii mpenzi wako anatabasabu na wewe unatabasamu, unaweza kuchukua hatua ya pili ambayo tumeieleza hapo juu.

6. Dalili dhahiri ya kuonyesha kuwa hufai kupoteza hata sekunde moja zaidi ni pale ambapo mpenzi wako ataanza kuonyesha dalili za wazi za kuanza kujilamba midomo yake huku akiiweka unyevu. Pia ukiona akianza kuuma midomo yake huku akiiviringa kwa mitindo flani ni ishara ya kukuambia: "wapoteza muda wangu, nataka unile dende sasa hivi"

7. Mwisho ni kuwa vichwa vyenu vitapinda upande wa kulia huku mkisogeleana. Tenshen ya kimapenzi itakuwa imejijenga kati yenu huku ikikoroga akili na miili yenu. Na mwisho ni ile hatua ya kuyeyusha kiu ambacho kimekuwa kikikuandama tangu siku ulipoweka nuru ya kumwona uliyempenda.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.