Formula Za Kumtumia Mwanamke SMS ili Aweze Kukujibu


Kupokea jibu kutoka kwa mwanamke wakati mwingine si rahisi. Wanawake ni viumbe ambao hawatabiriki kirahisi. Anaweza akajibu jumbe zako na mara ghafla unapata kuona amekujeukia na hajibu meseji zako tena. Mara nyingi ukiona hatua kama hii fahamu ya kuwa amepoteza hamu na wewe na itakuwa vigumu kwake kuweza kuongea na wewe tena.


Nakumbuka hivi juzi kabla janga hili la Corona Virus na  karantini kutujia, niliweza kupewa namba na mwanamke niliyekutana naye mtaani. Kama kawaida nilijua ya kuwa itakuwa rahisi kwangu kuweza kumteka mwanamke huyu bila wasiwasi.

Baada ya siku mbili ya kutumiana jumbe kwa chat, niliona amepunguza mazungumzo yake na mwisho kabisa akaacha kuchat na mimi. Ilikuwa pigo kwangu kwa kuwa haijakuwa jambo la kawaida kuweza kushindwa kuchat na mwanamke.

Lakini uzuri juzi, wakati karantini imeanza na kila mtu amelazimishwa kukaa nyumbani kwa wale ambao hawana mishe mijini, alianza kunijibu yeye mwenyewe.

So, kwa kuwa nimepitia jambo hili kwa mara yangu ya kwanza, leo pamoja na paneli yetu ya Nesi Mapenzi tumekuja na formula ambazo kwa kawaida tunazitumia kuanzisha mazungumzo na mwanamke ambaye amekupatia namba yake ya simu.

Ok, formula za kumtongoa mwanamke kupitia kwa SMS ni gani?

Na unapaswa kumuandikia nini?

Zama nami...

#1 Mbinu ya jadi.
Hii ni formula ambayo inapaswa kuwa kwa viganja vya kila mwanaume kila wakati anapopewa namba na mwanamke. Si lazima uandike mambo mengi. Wewe anza hivi; “Hi, ni *JINA LAKO HAPA* kutoka *SEHEMU MLIPOKUTANA*. Nilienjoy kukutana na kuongea na wewe leo”.

SMS hii inaonekana sahili lakini inatuma ujumbe mzito wa kuwa unavutiwa na yeye na uko interested na mambo yake.

#2 Msuko.
Kuanza kumtumia jumbe mwanamke mara ya kwanza pia unaweza kutumia maneno ya kutongoza bila wasiwasi. Matumizi ya SMS hizi hufanya kazi vizuri haswa wakati ambapo umekuwa ukimtongoza ulipokutana na yeye. So akikupa namba yake, si vibaya kama utaendelea na mwendo uo huo. [Soma: Jinsi ya kutongoza kirafiki]

Mfano unaweza kumtumia jumbe rahisi ambayo itaanza hivi; “Hi, ni *JINA LAKO HAPA*. Unamkumbuka yule mwanaume aliyekuwa akishinda akikuangalia sana leo.”

Hii ni jumbe ambayo inaweka lengo lake dhahiri hivyo itakuwa rahisi kwako kutimiza ajenda yako bila wasiwasi.

#3 Ujanja.
Huu ni ujumbe ambao unatumia mizaha na ucheshi. Mara nyingi unapokutana na mwanamke, unawezapata ya kuwa unatumia mbinu za ucheshi zaidi wakati unapomtongoza. Mwisho unajipata umezama ndani na unaonekana kama staa wa vichekesho. Hivyo akikupa namba yake ya simu, ingekuwa ni bora kuanza na ucheshi. [Soma: Jinsi ya kumchekesha mwanamke]

Katika kumtumia jumbe, unaweza kuanza kijanja kama hivi; “Hii ni meseji automatic kutoka kwa *JINA LAKO HAPA*. Jibu NDIO iwapo unataka kupokea meseji mbeleni. Jiba LA kusitisha mawasiliano yoyote ya mbeleni na *JINA LAKO HAPA*

Meseji kama hii ni nzuri kwa kuwa itakupa uhakikisho wa kuwa mawasiliano yenu yataendelea ama yatakatika. Hivyo mbinu hii ina umuhimu wake.

#4 Kumsifia.
Hapa unaweza kumsifia kwa jambo lolote lile ambalo unaona linaweza kumfaa. Unaweza kumwambia mwanamke ni mrembo, lakini ukimsifia mwanamke kuwa ni mjanja, mchangamfu ama mwenye msimamo itakuwa bora zaidi kwa kuwa ataona ya kuwa umemakinika na yeye.

So unaweza kumwambia maneno kama yafuatayo; Hi, ni *JINA LAKO HAPA*. Sikuweza kuvumilia nifike nyumbani nikutumie hii meseji. Nimependezwa na uchangamfu wako.

Hii ni muhimu kwa kuwa wanawake wamezoea kusifiwa kiumbo hivyo ukimsifia kihulka yake basi utakuwa umeuteka moyo wake rahisi na atakuwa makini na wewe zaidi. [Soma: Mbinu za kumpagawisha mwanamke]

#5 Muendelezo.
Wakati mwingine ukiwa unazungumza na mwanamke mkiwa pamoja, mazungumzo yenu yanaweza yasimalizike na badala yake anakupa namba yake ya simu. Hivyo ukipata namba yake unaweza kuendeleza na pale ambapo muliachia mazungumzo.

Mfano unaweza mtumia jumbe kama; “Hi, ni *JINA LAKO HAPA* Je ulienda kuangalia ile game ama?” Ama unaweza kusema “Niliangalia kile kitu ambacho ulisema awali na siamini ulijuaje.”

Hii ni mbinu rahisi kwa kuwa inakupa nafasi ya kuanzisha mazungumzo na yeye bila tatizo.


Hizi ni baadhi ya formula unaweza kuanzisha mazungumzo na mwanamke na ukiona amekujibu basi kuna uwezekano mazungumzo yenu yakaendelea bila wasiwasi. Unaweza kuboresha SMS zako kwa kutumia mbinu tofauti tofauti kulingana na vile ambavyo unaona itakusaidia.


1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.