Kutongoza Kutumia Mwili (Body Language) - Mambo Muhimu


Ushawahi wakati fulani kujihisi ya kuwa wanawake wanaongea lugha tofauti na vile unavyofikiria? Kama ushawahi kuwa na hayo mawazo, jua ya kuwa ni ukweli. Kulingana na wanasaikolojia, asilimia 90 ya mawasiliano tunayotumia huwa ni ya ishara...kumaanisha ya kuwa miili yetu huchangia pakubwa katika mawasiliano.

Hii ina maana ya kuwa kama hujui kutumia ishara vizuri kutaharibu mawasiliano yako na wanawake. Bila kupoteza wakati acha nikudokezee mambo muhimu ili uwe na ujuzi wa kutumia maongezi ya ishara vizuri.


Ufahamu mwili wako vizuri.
Kwanza unafaa kuelewa miondoko wa mwili wako wakati ambapo unaongea. (wanaume na wanawake hutumia hii mbinu). Ikiwa unadhani unafahamu kila kitu ambacho mwili wako hufanya wakati unapoongea basi unajidanganya.

Kama vile samaki hajitambui kama yuko ndani ya maji, vile vile mwili wa binadamu hukua hivyo hivyo. Anza kujifunza kumakinika na vidole vyako wakati unapoongea na mtu ama wakati umesimama.

Unajihisi unatetemeka, kuingiwa na baridi, kuanza kucheza na vidole, kushika nyuma ya shingo, kukunja mikono, kuchezea na simu yako wakati ambapo unaongea ama kufanya kitu ambacho kinaonyesha unashughli flani?

Iwapo ni hivyo, fahamu ya kuwa kwa mwanamke atatabiri jambo tofauti. Ataona kama wewe unawasiwasi, ama kuona kama hauna interest kwake ama zaidi kuona kuwa haujiskii uko salama na yeye.

Kwa hivyo lazima ujifunze kuufahamu mwili wako na kuelewa kila kitu ambacho unafanya wakati ambapo utakuwa ukiongea na mwanamke.

Maongezi ya mwili huashiria kuwepo kwako
Hivi ulikuwa wafahamu ya kuwa wanawake huangalia miondoko ya mwili wako zaidi ili kuangalia kama uko hapo na yeye ama unawaza kwingine?
Kwa wanaume, mara nyingi hawatilii maanani kuwepo kwa akili ya mwanamke wakati wanapoongea. Hivyo kwao ni msamiati ambao haufahamiki sana.

Kwa wanawake, wao hupenda sana kuona ya kuwa yule wanayezungumza naye anamsikiliza kwa makini. Mara nyingi wanaume wanapoongea na mwanamke wanasahau swala hili ambalo inafikia wakati fulani mwanamke analoose interest na yeye.

Kama unataka kuuteka moyo wa mwanamke kiurahisi basi lazima uwe na umakini kwa kila kitu atakachokuwa akifanya na kuongea.

Hizi ni baadhi ya hatua utakazofanya ili kuhakikisha kuwa unaonyesha dalili za kuwepo kwako katika maongezi yako na mwanamke.

1. Mwangalie macho yake
Kumuamgalia macho yake wakati anapoongea ni ishara kubwa ya kuonyesha ya kuwa unamakinika na kila kitu anachoongea hivyo kuona ya kuwa akili yako umeimakinisha kumsikiliza yeye. Hii itakusaidia wewe pia usimwangalie sehemu yake ya matiti ama sehemu nyingine.

2. Msikilize
Kumsikiliza kutakupa atenshen ya kuelewa kila kitu anachoongea na kufanya maongezi yenu yakueleweka. Pia itakupa usukani wa kupeleka vile maongezi yenu yanafaa kuenda. Mfano akiongea kuhusu mambo anapenda, unamuuliza aeleze kwa undani mambo anayoyapenda.

3. Kumtomasa kimpango
Hapa bora usiingiwe na tamaa chafu. Kufanikisha hivi unaweza kuanza kwa kushika simu yake, mkufu, kipuli ama chochote ambacho alochovaa. Hivi kwake kutaashiria ya kuwa unajiskia huru ukiwa naye hapo ulipo.

Mwanaume ambaye anajiamini hawezi kubabaika wala kuogopa iwapo ataanza kumtomasa mwanamke ilimradi asizue hisia ambazo ataonekana yeye kuwa na pepo la ngono.
No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.