Hatua 3 Muhimu Ambazo Zitatoa Uoga Wa Kuaproach Mwanamke


Ushawahi kupatikana katika situation ambayo unampenda mwanamke flani umekutana naye sehemu flani lakini unashindwa kumfuata umweleze hisia zako?

Tatizo hapa kama kawaida huwa ni uoga ambao unakujia kwa ghafla bila wewe kuweza kukontrol.


Wakati mwingine kuapproch mwanamke ni kazi nyingine ngumu sana. Enyewe unaweza ukaaproach mwanamke halafu akakuaibisha kwa kukukataa kweupe mbele za watu. Inaweza kuwa katika klabu, supermarket, kituo cha mabasi nk. Ukiweka dhana ya kuwa ukiapproach mwanamke flani atakukataa, uoga ndio huanza na hapo, na ni vigumu kwako kuweza kutoboa kuongea na mwanamke aina hii.

So utafanyaje mpaka uuondoe huo woga wa kuapproach mwanamke?

Kuuondoa woga wa kuapproach mwanamke ni rahisi sana. Kuna mbinu rahisi ambazo unaweza kuzitumia kutuliza neva zako na kukupatia nafasi nzuri ya kuuteka moyo wa mwanamke unayemzimia. 

Zama nami.

Hatua za kuondoa uoga wa kuaproach mwanamke

1. Kuwa na mawazo yanayokufaa
Kuwa na mawazo yanayokufaa yanasaidia sana kuondoa uoga kwa akili yako. Mfano iwapo unaaproach mwanamke huku ukiwa na mawazo kama "Manisha huyu mwanamke ni mzuri zaidi ya Beyonce. Najua nikimuapproach atanikataa, hata nihifadhi masomo yote ya Sanaa ya Kutongoza bado atanikataa." Ukiwa umeweka akilini mwako kuwa hauwezi kutoboa kuapproach mwanamke basi elewa ya kuwa hutoweza kweli.

Ok. Mbona usiwe na mawazo chanya? Mfano weka katika akili yako mawazo kama vile " Duh! Huyu mwanamke ni nomaaa, leo najiskia kutangamana na watu, najua nikimfuata hapa kwangu hawezi kukataa."

Jikumbushe ya kuwa huyu mwanamke si mwisho wa dunia. Hata kama atakataa mwitiko wako kuna milioni ya wanaweke wengine kama yeye ambao wanatafuta nafasi ya kufukuziwa. 

Pia elewa ya kuwa kukataliwa na mwanamke mara ya kwanza hakumaanishi kuwa ni mwisho wa safari. Na hata kama akikataa mara ya pili ama mara ya tatu kuna wengine ambao unaweza kuwaaproach bila wasiwasi wowote.

2. Ongeza ujuzi wako wa kuongea na wanawake
Kuna ule msemo wa kizungu unaosema 'practise make perfect'. Ukitaka kuwa bingwa wa kufanya jambo flani lazima basi ufanye mazoezi ya mara kwa mara. So mazoezi utayafanya vipi?

#Ongea na wanawake. Ongea na wanawake sehemu yeyote ile, kuanzia madukani, sokoni, shuleni, kazini, sehemu yeyote ile ongea na wanawake. Mwanamke ni mwanamke hata kama ni yule ambaye amekuvutia. Kuongea na wanawake kunakupa confidence ambayo unaweza kuitumia mbeleni wakati ambapo utakuwa unamtongoza yule ambaye umempenda. [Soma: Hatua za moja kwa moja za jinsi ya kuapproach mwanamke]

#Anza kwa kujenga msingi. Iwapo unaaproach mwanamke, haswa yule ambaye hujawahi kukutana naye, usimuulize maswali ambayo yatamlenga yeye binafsi.
Usijaribu kumuuliza jina lake papo kwa hapo, unalohitajika ni kuanza na maswala ambayo hayamlengi yeye. Mfano kama umekutana naye kwa klabu unaweza kuzungumza kuhusu nyimbo ambazo zinachezwa ama kumuuliza kuhusu kinywaji anachopenda. Kama umekutana naye barabarani unaweza kuongea maswala ya kuhusu hali ya anga, wakati ambapo basi litakapokuja ama habari zinazohusiana nayo.

Baada ya kueleza haya yote sasa unaweza kujitambulisha halafu ndio umuulize jina lake. Ukitumia hii njia atajiskia huru zaidi kuliko kama utachukua hatua ya kumuuliza jina lake papo kwa hapo.

#Makinika na mambo anayopenda. Kumakinika na vitu ambavyo mtu anapenda hufanya maongezi yakuwe marefu. Kwa kawaida watu hupenda kuongea vitu ambavyo wanapenda. So kama unaongea na mwanamke halafu akakutajia kuwa anapenda wanyama, wewe unafaa kupanua mawazo yako na kujaribu kumuuliza ziada. Mfano unaweza kumuuliza mnyama gani anapenda zaidi, kama angepewa nafasi ya kufuga mnyama angechagua yupi nk. [Soma: Maswali mazuri ya kumuuliza mwanamke]

Maongezi yako na yeye yataendelea iwapo ameonyesha kupendezwa. So iwapo unaona unataka kuanzisha mada ambayo itaonesha kumboa basi ni hatua ya kwako kujeuza gumzo zima.

#Kumsifia. Wanawake hupenda kusifiwa. Wanawake wanapitia hatua ndefu ya kujipodoa kabla hawajatoka out. Wanachukua muda wao mwingi kujiangalia kwa vioo, nguo ambazo zitalingana na siku, mitindo yao ya nywele na kadhalika.

Hivyo basi kama umeugundua mwonekano wa mwanamke mbona usimpongeze? Kumwambia maneno kama "leo nimependa mwonekano wako" ama kumwambia "leo umetoklezea" kutafanya kazi kubwa kwako. Kumpongeza mwanamke kwa kitu alichofanya kutamfanya kujiskia mrembo na kuona ya kuwa umekuvutia. Hii itaongeza nafasi yako zaidi kupendwa na wanawake.

Ijapokuwa kumsifia mwanamke ni jambo zuri, kutategemea na wakati ama sehemu ambayo unampongeza mwanamke huyo. Mfano iwapo unaongea na mwanamke kwa mara ya kwanza huwezi kumwambia "una matiti ya kupendeza." Huku kutamfanya mwanamke kutojiskia huru na wewe ama kukuona wewe kama fala.

3. Jifunze kwa watu wenye ujuzi
Kujifunza kutoka kwa watu kunaweza kuwa njia nzuri ya kujifunza kutokuwa na woga wakati wa kuapproch mwanamke. Hii ni kuanzia kuuliza marafiki zako, wale unaofanya nao kazi, unaosoma nao na pia unaweza kupata ujuzi kutoka kwa vipindi vya runinga. [Soma: Leonardo DiCaprio akitufunza silaha 3 kuu kwa mwanamke]

Pia unaweza kujaribu kuuliza baadhi ya marafiki zako wanawake. Mfano unaweza kuwauliza kama "wanawake wanapenda njia gani ya kutongozwa" ama "mambo gani ambayo yanamuudhi mwanamke wakati wa kuongea"

Kwa wanawake wengine wanaweza kutojiskia huru kukujibu lakini ukimpata yule ambaye yuko huru anaweka kukuambia kila kitu kuanzia A hadi Z.

Kumalizia ni kuwa kuwa na woga wa kuapproach mwanamke ni jambo ambalo wengi hupitia na ukifanya mazoezi ya mara kwa mara basi changamoto hii unaweza kuikabili kwa njia ya rahisi.
5 comments:

 1. Kusema kweli mi mwenyew hadi muda huu niko na miaka 28 lakini kitu kilicho ni shinda ni ule ujasiri wa kumsimamisha mwanamke na kumtongoza hapa kusema kweli napaona pagumu sana
  Na wapo wanawake ambao wanataka kuanzisha mahusiano nami lkn nashindwa kuwa na njia sahihi ya kuanzisha mazungumzo ya aina yeyote na wao kila ninapofika karibu kuwaongelesha moyo unasita na kukata shauri

  ReplyDelete
  Replies
  1. Lakini na wewe ukifuata hizi mbinu tumezielekeza basi itakuwa rahisi kwako kumpata mwanamke haraka sana

   Delete
 2. Ashanteni sana kwa shauri, ningependa kujua nimefaulu kuongea naye akanipa namba, pale kwa message ni topic gani nafaa kuongea naye ili asikatae kureply.

  ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.