Jinsi Ya Kumwinda Mwanamke Kwa Baa, Klabu


Kuapproach mwanamke na kuanza kuongea naye katika baa ama klabu ni tofauti kabisa ukilinganisha na kumchukua mwanamke katika mkahawa, supermarket, vituo vya basi nk. Katika bar ama klabu itakubidi uanze approach ya kutumia macho kwa sababu ya kelele nyingi ambazo hutokea katika sehemu hizo.


Ok, kabla hujazifahamu hizi hatua lazima uwe unavijua vipengele kadhaa ambavyo vitakusaidia wewe kuapproach mwanamke aina hii bila wasiwasi. Hii nikuanzia kujiamini, jinsi ya kuzungumza naye, mambo ya kuepuka wakati uko naye nk (Tushaeleza katika post za awali)

Hatua za kufanya kumchukua mwanamke katika klabu, baa

1. Anza kwa kumuangalia macho
Hii ni hatua muhimu hapa. Mwangalie machoni mwake mpaka akugundue kuwa unamuangalia. Ukiona naye ameanza kukuagalia, wewe unafaa uweke tabasamu halafu uangalie kando. Hapa utakuwa umemtumia ujumbe wa kuwa umependezwa naye. Kama pia yeye amependezwa na wewe atatabasamu. Anaweza kutumia njia nyingine za kukuonyesha kuwa amependezwa na wewe kv kushika nywele zake. Kushika nywele ni njia rahisi ya kuonyesha kuwa mwanamke amependezwa nawe. Lazima ujue na kuzifahamu mbinu nyingine ambazo anaweza kutumia kukuonyesha kuwa amependezwa nawewe. [Soma: Mbinu ambazo wanawake huonyesha kama wamempenda mwanaume]

2. Anza kumuandama
Baada ya sekunde kumi ya kumtabasamia, anza kumuapproach pale yuko. Usikimbilie uende ukae naye ubavuni mwake, la, unafaa uanze kwa kumsogelea karibu naye. Usiwe na pupa. Chukua hatua moja baada ya nyingine. Kuchua hatua ya pole pole kumuapproach hadi pale alipokaa. Usisahau kuweka tabasamu lako wakati ambapo unamuapproach. Pia wakati ambapo unamfuata usimwangalie usoni la sivyo anaweza kukuchukulia wewe kama tishio kwake. Ni vizuri kumuapproach kwa upande wake. [Soma: Kutoa uoga wa kuapproach mwanamke]

Iwapo atakuwa ana marafiki zake, si rahisi kwake kukunotice. Hivyo unafaa kumwambia ya kuwa huna muda mwingine wa kukaa kwani unataka kwenda mahali flani. Kumwambia hivi kutamfanya yeye kukupa atenshen yake kwako ili asipoteze muda wowote ule.

3. Teka hisia za marafiki zake
Kama tujuavyo ni vigumu sana kwa mwanamke kuenda baa ama klabu akiwa pekeake. Lazima atakuwa ameandamana na marafiki zake. Kama umepatikana katika hali kama hii basi itakubidi uanze kwa kuteka hisia za kikundi kizima. Iwapo kuna mwanaume kikundini, jitambulishe kwao na pia ujaribu kufanya utafiti iwapo huyo mwanamke unayemfukuzia ana boyfriend hapo au la. Pia kama kuna 'malkia' kikundini usisahau kumfanya rafiki yako. [Soma: Jinsi ya kukutana na wanawake wapya]

4. Muibe kutoka kwa marafiki zake
Baada ya kujitambulisha kikundini na kujuana nao, tafuta kisababu cha kutoka na windo lako. Hapa unaweza kutoa kisababu kama "Nilikuwa nataka kumchukua rafiki yenu kuna kitu nataka kuongea naye. Sitokaa naye sana ntamrudisha sasa hivi. Kuna tatizo?"

Njia nyingine ya kumteka mwanamke kama huyu ni kuwakaribisha kikundi kizima katika himaya yako, pale ambapo ulikuwa umekaa awali. Hapa unaweza kutoa kisababu cha kuwaambia kuwa hio sehemu ina kelele ama inakaa ndogo hivyo muende sehemu tofauti. Wakikubali utakuwa sasa wewe ndio umekuwa kiongozi wao hivyo itakuwa rahisi kwako kuanza mazungumzo na kuomba namba ya simu kiurahisi.

Amini usiamini ukitumia mbinu hizi nimeziorodhesha na baadhi ya ujanja ambao tumeweza kuchapisha katika nakala zetu za awali, hakuna kitu kitakushinda. Unaweza kufanya chochote kile mbele ya mwanamke bila kuingiwa na woga wala wasiwasi.


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.