Jinsi Ya Kuapproach Mwanamke Ambaye Humjui


Wengi husema kuwa kuaproach mwanamke ambao hawawajui ni vigumu kwao. Ndio maana utapata wanaume wengi wanapenda kuunganishiwa wanawake na marafiki zao. Wengine hata hujaribu kutongoza wanawake ambao wamewazoea lakini tayari wako na wachumba.


Hapa Nesi Mapenzi tunaamini kuwa mwanamke yeyote yule ni rahisi kumtongoza. Aidha unamjua ama humjui.

Hizi hapa ni mbinu ambazo unapaswa kufuata ili uweze kumuaproach mwanamke usiyemjua kwa urahisi.

#1 Mwangalie.
Tuseme sahizi uko na marafiki zako ama uko pekeako katika sehemu ambayo ina watu wengi halafu huyo mwanamke unataka kumuaproach yuko karibu na wewe ama sehemu mbali kidogo na wewe. Kile unachohitajika sasa ni umuangalie ili ufanye kumuonyesha kama unajaribu kumuangalia yeye. Jaribu kujifanya unamwuangalia kisirisiri, halafu akijaribu kukuangalia tu unajifanya unashughli nyingine ama unaongea na marafiki zako. Hii itamsisimua kutaka kujua kwa nini unamuangalia hivyo itamfanya na yeye kukuangalia mara kwa mara kama utakuwa ukimwangalia.[Soma: Jinsi ya kumvutia mwanamke]

#2 Mwangalie machoni.
Kila wakati akikuangalia, wewe muangalie halafu papo hapo uangalie kando kikondoo. Endelea kumuangalia kimtindo huo mara kwa mara, na wakati mwingine, mwangalie nusu sekunde, uangalie kando halafu hapo hapo muangalie tena (nadhani hapo umenipata). Ukifanya hivyo utakuwa automatiacally unamsisimua kihisia. Lakini kama umejaribu njia hii yote halafu hakuonyesha dalili ya kuingiliana basi itakuwa hajakupenda ama kuridhika na wewe.

#3 Jifanye kutoeleweka.

Kama uko na marafiki zako, muangalie mara kwa mara, lakini jifanye kama unasumbuliwa na jambo fulani ambalo linakufanya wewe usielewe kile ambacho marafiki zako wanaongea. Hii itamfanya yule mwanamke kufikiria kuwa ameingia kwa akili yako hivyo ataona ya kuwa yeye ndiye chanzo kikuu kinachokuzuia wewe kumakinika na yale ambayo marafiki zako wanaongea. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akupe nambay yake ya simu]

#4 Mwonyeshe tabasamu.
Bila kupoteza wakati, hii itakuwa ufunguo wa kwako kufungua mlango wako wa kuongea naye kwani atenshen yote yake itakuwa imekuja kwako hivyo lile unalohitajika la kufanya ni kumwonyesha tabasamu. Fanya kusmile kiasi tu ili kuonyesha kuwa wewe umekuwa intrested na yeye muda huyu wote.

ONYO: Usijaribu kuweka smile kubwa kwani itaweza kuleta maana nyingine haswa kwa mwanamke ambaye humfahamu kabisa.
Hatua hizi hapa juu lazima zote ziwiiane, yaani lazima zifanye kazi. Iwapo katika hatua yoyote hapo juu utamwona mwanamke anakupotezea, basi jua na mapema kuwa hujamridhisha na kile unachohitaji kufanya ni kukimbia tu.


1 comment:

  1. Nimependa Sana hili dalasa liko powa sana sana jamani

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.