Hatua 8 Mtu Hupitia Baada Ya Kuachwa Na Mpenzi Wake


Kuachwa baada ya kuingia katika mahusiano ni jambo ambalo hutokea mara kwa mara. Lakini wengi hawajui kuwa kila mara ukivunjwa moyo na mpenzi wako kuna hatua ambazo lazima uzipitie kabla ya kurudi kuwa kawaida. Leo tumeandika hatua ambazo mtu hupitia wakati ambapo ameachwa na mpenzi wake.


Hizi ni hatua mtu hupitia akiachwa na mpenzi wake.

#1 Mshtuko.
Ok, kumekuwa na ishara kuwa mpenzi wako yuko karibu kukuacha lakini bado unapuuza. Kisha siku moja akakutokea na kukuangalia usoni mwako na kukuambia kuwa wewe na yeye mambo yenu yameisha. Hapo ndipo unakuwa na mshtuko wa mara ya kwanza.

#2 Kukataa.
Hii hatua huja baada ya mshtuko wa kuwa umeachwa. Lakini kuna kitu ndani yako ambacho kinakwambia kuwa labda amekasirika tu, atarudi.  Unampigia simu, unamtumia sms ukimwomba msamaha huku ukiwa na matumaini ya kuwa atarudiana na wewe. [Soma: Sababu ambazo wanawake huwakataa wanaume]

#3 Kujitenga.
Kwa kuwa unaona hataki kujibu meseji zako ama anakataa kuwasiliana na wewe, unaamua kujitenga na dunia. Unafuta namba zake zote za simu. Unajificha nyumbani hutaki mtu yeyote awasiliane na wewe. Unajitenga na uhalisia.

#4 Pupa.
Hii hatua huja baada ya kujitenga. Utakuwa umejitenga kwa muda mrefu kisha ghafla unaingiwa na mawazo ya kuwa mwema. Ulipokuwa na yeye katika mahusiano haukuwa unamjali, lakini sahizi unakuja na mbinu mpya za kujaribu juu chini kuhakikisha anakuona kuwa umebadilika na hautakuwa na tabia kama za zamani. [Soma: Makosa ambayo wanaume huwafanyia wanawake]

#5 Hasira.
Hata baada ya kuonyesha kuwa umebadilika unaona bado mambo hayajabadilika. Hatua hii huja na hasira nyingi za kujutia kwa nini ulikuwa na mahusiano na mtu huyo. Hatua hii unamchukia mtu huyu kiasi cha kuwa unamfaninisha na shetani ama adui. Chuki na hasira zisizoisha.

#6 Huzuni.
Baada ya hasira, hatua inayokuja unakumbuka kuwa kweli ulikuwa unampenda. Kila mahali ukienda unaona sura yake mbele yako. Unajiona kuwa bila yeye maisha yako hayana maana. Unajiona kuwa hufai katika dunia hii kwa kuwa umemkosa yule mtu ambaye ulikuwa unampenda zaidi hapa ulimwenguni.

#7 Unajirudisha nyuma.
Well, ameenda na sioni dalili zozote za yeye kurudiana na mimi. Shida iko wapi? Sijakufa, na kuna wengine wengi ambao wananiona kuwa mimi nafaa. Dunia haitaisha leo. Hii ndio hatua ambao unajikuta unatangamana na wengine ili kujionyesha kuwa kama aliniacha bado naweza kuwa na wengine wengi...lakini mwisho wa siku bado utaona kuwa ulikuwa unajirudia nyuma tu.

#8 Kujikubali.
Hii ndio hatua ya mwisho ambayo mtu hupitia akiachwa na mpenzi wake. Nayo ni kujikubali. Maisha yanasonga mbele. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akuone kuwa wewe ndie kila kitu kwake]

Je sasa hivi uko katika hatua gani? Ama unakumbuka hatua hizi ulipoachwa? Kwa wale ambao bado hawajapatikana kuachwa, fahamu kuwa hizi ndizo hatua ambazo utazipitia.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.