Jinsi Ya Kuuhepa Mtego Wa Kuwa Rafiki Na Mwanamke Unayempenda

Kama kuna kitu ambacho wanaume wanachukia ama kuogopa ikija katika maswala ya mahusiano ni kuona yule mwanamke unayempenda amejeuka rafiki yako badala ya mpenzi wako. Hii inajitokeza wakati mwanamume anaposhindwa kutumia mbinu mwafaka ambazo zitamwezesha yeye kutofautisha kati ya rafiki na mpenzi. Hii inadhihirika wakati ambapo mwanamume anakuwa rafiki wa mwanamke sana kupiti kiasi, inafikia level ambayo mwanamke anakuona wewe kama mtu ambaye akikumbwa na tatizo basi anakufikiria wewe. Wanaume wengi ikifikia hatua kama hii wanashindwa kujitatua na wanaishia kuwaona wanawake wanaowapenda kuchukuliwa na waume wengine huku wao wakiwa wameachwa katikati bila kujua la kufanya.
Ok. Kama wewe ni mmoja wa wanaume ambao wameachwa katika sehemu ya urafiki (friend zone) basi fahamu kuwa kuna habari njema. Tatizo lako limetatuliwa kwa njia rahisi.

1. Kuwa rafiki yake lakini tofauti na marafiki zake wengine

Msiongee vitu vya kijinga kwa masaa mengi ama mkae mnaongea kuhusu matatizo yake anayokumbana nayo maishani. Mnafaa kuongea vitu kama sinema, sehemu anazotembea, vitu ambavyo anapanga kufanya wikendi nk. Ongea vitu ambavyo vinahusiana na kudate. Hapo utafanya kuwe na msisimko kati yenu juu ya hewa.

2. Jaribu kuongea naye mkiwa pekeenu
Kama yuko na marafiki zake wengine, unaweza kuongea na yeye ama ukaamua kutoongea kabisa manake hauwezi kumrushia matamu akiwa pamoja na kundi zima la marafiki.
Mkiwa wawili unaweza kujaribu kutumia maujanja wa kumsuka bila yeye kutambua halafu kama kumekuja mtu wa tatu fanya kujeuza stori fasta. Hii itamuacha yeye kujiuliza kama kweli ulikuwa unafanya mzaha ama uko serious.
Hii itampa fikra za kuwa wewe unapenda zaidi kuongea na yeye mkiwa wawili pekee. Mwonyeshe dhahiri kuwa unapenda company yenu zaidi mkiwa wawili. Lakini chunga usithubutu kumwambia kuwa unampenda ama wataka kumtoa out.

3. Msifu wakati ambapo inahitajika
Kama amependeza usisahau kuchukua nafasi ya kumsifu. Pia unaweza kutumia ujanja wa kuchungulia kifua chake halafu kama amekuona ukimuangalia, fanya kutabasamu, mwombe msamaha halafu umwambie kuwa ulikuwa umeshindwa kujizuia. Jaribu kuongea na maneno ya ucheshi wa mapenzi na kutoa maoni ya mapenzi. Amini usiamini ataanza kukufikiria tofauti na utakuwa ukijinasua pole pole kutoka friend zone.[Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke apagawe kwako]

4. Mshike na mchukulie kama ni girlfriend wako
Lakini fanya na heshima. Unaweza kumshika mkono wakati mnavuka barabara na pia kumfungulia mlango kwa nyinyi wawili. Mfanye ajihisi yeye kama malkia na ataanza kupenda ateshen yako. Akiwa na marafiki wengine usimwonyeshe dalili hizi. Mfanye aelewe kwamba hii inatokea kama mko wawili pekee.

5. Mfanye ajihisi kuwa yeye specially
Mtuze kwa kumletea zawadi ndogo ndogo na binafsi mfano waweza kumletea ushanga nk lakini hakikisha kuwa umemwambia kuwa iwe siri kati yenu. Ukifanya iwe siri yenu utakuwa automatically unafungua mlango wa mapenzi na ataanza kukufikiria na mtizamo mwingine. Utakuwa mnajenga kemia kati yenu.

7. Muulize kama anataka kutoka out halafu ubadilishe stori fasta

Kama unaongea na yeye unaweza kumwambia kuwa unataka kumtoa lunch ama kwa mkahawa. Lakini kabla hajajibu fanya kumjeuzia topic nyingine ili abaki ajiuliza kama ulikuwa unafanya mizaha au la. Hivi itakuwa ikondoa tenshen ambayo itakuwa imejitokeza wakati wa kuuliza swali kama hilo.
[Soma: Dalili 7 za kuonyesha kuwa mwanamke anakupenda]
Hii ndio njia rahisi ya kutumia na mara kwa mara utaona kuwa amevutiwa na wewe. Baada ya muda flani unaweza kuchukua hatua ya kumuuliza kama angetoka date na wewe na hapo hawezi kukataa.
Jinsi Ya Kuuhepa Mtego Wa Kuwa Rafiki Na Mwanamke Unayempenda Jinsi Ya Kuuhepa Mtego Wa Kuwa Rafiki Na Mwanamke Unayempenda Reviewed by Ibrahim Morowa on 10:34 AM Rating: 5

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.