Hatua 7 Za Kufuata Iwapo Mpenzi Wako Anakataa Kujibu SMS Zako


Tumetangulia awali kwa kuorodhesha baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa yamechangia hadi mwanamke amekuacha. Na tukatoa baadhi ya sababu ni kuwa labda mwanamke huyu alikuwa hajakupenda ama amechoka na wewe. Pia tukaeleza kuwa inaweza kuwa tayari yuko na mwingine. Ingia hapa uzione sababu zote ambazo tulizieleza ambazo zinaweza kuwa chanzo cha mpenzi wako kutojibu jumbe zako. [Soma: Sababu ambazo zinamfanya mpenzi wako asijibu meseji zako]


Kufikia sasa naamini sababu ushazijua. Je, bado una tamaa ya kurudiana naye? Je, mahusiano yenu baada ya kugundua sababu za yeye kutojibu jumbe zako yatadumu? Kama unaona umuhimu wa kuendelea uhusiano wenu basi endelea kusoma chapisho hili. Kama unaona hakuna umuhimu wa penzi lenu kuendelea basi itakubidi utafute mchumba mpya. [Soma: Jinsi ya kupata mpenzi mpya]

Well. Hebu tujaribu uwezo wetu wa kuhakikisha kuwa mwanamke huyu anarudi nyuma na kuanza tena kukutumia jumbe. Hizi ni baadhi ya mbinu ambazo unapaswa kufuata ili kumfanya ajibu meseji zako bila kinyongo.

Psss! Mbinu hizi zinaweza kutumika kwa aidha mwanaume ama mwanamke.

#1 Ngojea kwanza.
Ni kawaida kuwa na hamaki za kutaka mpenzi wako aanze kukujibu meseji zako kwa haraka lakini usiwe na pupa. Ngojea. Kama amekataa kukujibu achana naye. Usipanic. Wewe la kufanya ni kutoonekana kama una mahitaji mengi kwake. Kama umekuwa ukimtumia jumbe nyingi ni wakati wako kusitisha.

#2 Kuwa mtulivu.
Kwa kuwa hauko tayari kumuacha mwanamke kama huyu kukuacha hivi hivi, lazima utajaribu kutia bidii angalau kumtumia jumbe kwa mara nyingine. Ok, hii inaeleweka. Na ni vizuri baada ya kuacha kumtumia jumbe kama wiki moja hivi unapaswa kumjulia hali ujue anaendelea vipi.

#3 Usimuulize maswali.
Akikujibu jumbe yako usianze kumuuliza maswali. Maswali yatamfanya aweke ukuta ambao utashindwa kuubomoa. Maswali ya mbona hukujibu meseji zangu huu muda wote hayafai. Anza na mazungumzo ya wastani, mfano unaeleza mambo ambayo umeyafanya wiki nzima na umepata kujua mbinu flani ya ‘kufanya kitu’ na ungependa kumuonyesha. [Soma: Maswali mazuri ya kumuuliza mwanamke]

#4 Unaweza ukamtext kwa kuzungumza chochote.
Meseji nzuri ni ile ya habari ya asubuhi, leo umeshindaje, usiku mwema, unafanya nini sahizi nk. Hapa unapaswa kuna na mtindo mpya kabisa wa mazungumzo. Kumbuka lengo letu hapa ni kumfanya ajibu meseji zako. Na ukiona kuwa anakujibu basi kuna matumaini kuwa mbeleni mamb yatakuwa shwari.

#5 Tafuta wakati mzuri wa kumtumia meseji.
Wakati mzuri wa kumtumia mpenzi wako meseji ni ule wakati ambao hayuko busy. Mfano nyakati nzuri ni kama saa tatu usiku. Ukimtumia sms wakati yuko chuoni ama kazini basi anaweza kuiona meseji yako na kuipuuza. So unapaswa ujipange vizuri hapa. [Soma: Sheria za kufuata unapomtumia meseji unayemzimia]

#6 Tambua ishara za kuwa hataki mawasiliano yako.
Kuna njia ambazo utajua kama mwanamke hataki mawasiliano yako. Mara nyingi hutumia mbinu ya kukujibu ‘ndio’ na ‘hapana’. Pia utajiona kuwa wewe ndie unayeuliza maswali mengi na yeye anajibu tu. Ukiona hivyo ujue hakuna matumaini. Hapo anakwambia kifioa kuwa hakutaki.

#7 Endelea na maisha yako.
Usijitie presha bure. Kama mbinu hizi tulizozieleza hapo juu na bado unaona kuwa hajibu kama vile ulikuwa unatarijia, basi ni wakati mzuri wa wewe kuvunganya virago na kusimamisha uhusiano wenu. Kuna wanawake wengi ambao wako single na wanahitaji kuchumbiwa.


Kwa sasa naamini kuwa uko tayari kujaribu na kupambana na hali hii. Mafanikio kwako.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.