Maswali Mazuri ya Kumuuliza Mwanamke


Tumekuwa tukipokea request nyingi kutoka kwa mashabiki wetu wa Nesi Mapenzi wakitaka kufundishwa jinsi ya kumuuliza maswali mwanamke. Tumejizatiti mara kwa mara kuja na machapisho tofauti tofauti ambayo yanakuwa na maswali mazuri ya kumuuliza mwanamke.


Ingawaje bado wengi hawaridhiki na maswali hayo ama wanataka maswali ya ziada, sisi hufanya kadri iwezavyo kuja na maswali ambayo yanakuwa na manufaa mengi haswa wakati unapojenga mazungumzo.


Baadhi ya maswali yenyewe ni kama yafuatayo.

#1 Kawaida unafanya nini siku za wikendi?
Hili ni swali ambalo unaweza kumuuliza mwanamke yeyote ili kuzua mjadala zaidi. Iwapo ashaeleza katika profile  yake haswa kwa mtandao, basi unaweza kulijeuza swali hilo na kumuuliza zaidi kuhusu mambo anayoyafanya wikendi. Mfano kama ameeleza kuwa wikendi yeye hupenda kupika basi unamuuliza ni chakula gani na kadhalika. Hivi utamfanya akuelezi mengi na mengi huku ukimakinika kwa kuchukua yote ambayo atakutajia ili baadae utumie hio nafasi kuuliza maswali zaidi. Pia unaweza kutumia hii nafasi uangalie vitu ambavyo vinafanana na mnavipenda nyote wawili. [Soma: Njia tofauti tofauti za kutongoza kwa kutumia macho]

#2 Ushawahi kukutana na mwanaume yeyote kwa mtandao ambaye humpendi?
Hili ni swali muhimu kumuuliza mwanamke kwani litakusaidia wewe kujitenga na kujitofautisha na wanaume wengine wanaopatikana kwa mtandao wa kijamii. Kumuuliza swali hili litamfanya kufungua roho yake kwako kwani ataona ya kwamba wewe unaelewa tofauti na changamoto ambazo zinapatikana kwa wanawake kutoka kwa wanaume. Hii kwa muda mfupi utamwona mwanamke kama huyu akiingiwa na ari ya kutaka kukujua zaidi na zaidi.[Soma: Maswali machafu ya kumuuliza mwanamke mtandaoni mpaka apandwe na nyege]

#3 Je wapenda date zinazofanyika online?
Hapa lazima utumie ujanja wakati wa kuuliza swali kama hili. Jaribu kutumia mbinu ya kujeuza jeuza na kuchezea maneno ilimradi uzue maswala mengi ambayo yatazunguka katika hili swali. Mfano baada ya kumuuliza unaweza kuuliza maswali kama nani, wapi, ilikuwaje, halafu nk ili kufanya maongezi yenyewe yawe na mnato wake.
Jaribu kumakinika kadri uwezavyo na unukuu mambo ambayo tayari amepitia ili kujaribu kufananisha na yako.

#4 Vitu gani unavyopenda na kuchukia?
Fanya kumuuliza hili swali ili upate kuyajua mambo yake . Hii itakuwasaidia wewe kuweka mipaka kwa mambo ambayo yanaweza kumkwaza ama kumfurahisha.[Soma: Mchezo utakaotumia kumshawishi mwanamke atoke deti na wewe bila kukataa]

KUMBUKA: Kulingana na utafiti ni kuwa ndoa nyingi ambazo zinatokana na mitandao ya kijamii hufanikiwa zaidi kuliko ndoa nyingine zozote zile.
Pia fahamu ya kwamba maswali manne hapo juu yanaweza kubadilishwa ili yatumike kulingana na changamoto unazoziona wewe. [Soma: Orodha ya mitandao maarufu ya kutongoza]


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.