Mbinu Ya Kutumia Kumwomba Deti Mwanamke Na Akubali Fasta


Imebainika ya kuwa asilimia kubwa ya wanaume hawatumii njia mwafaka ya kutongoza mwanamke. Kulingana na utafiti uliofanywa na mtandao wa askmen.com, imebainika ya kuwa wanaume wengi hutumia njia ambazo mwishowe zinawajeukia ikija maswala ya mahusiano. Hili swala zima lilinitia wasiwasi na niliamua mimi na jopo langu(post humu ndani kabla ziandikwe huwa zimefanyiwa majaribio kadhaa) kuandika mada ambazo zina msururu wa mafundisho ya jinsi ya kumshawishi mwanamke kwa njia rahisi isiokuwa na changamoto.

Leo nimeamua kugusia swala la mbinu mwafaka ambazo unahitaji kutumia ili kumuuliza demu yeyote atoko out na wewe.
Owk kwa haraka hebu tuorodheshe baadhi ya sheria ambazo lazima uwe nazo.

1. Pozi lako unaloweka lazima lionyeshe dalili ya kujiamini
Wanaume wengi hujikatia tiketi ya bure ya kukataliwa kila wanapo approach mwanamke kwa mara yao ya kwanza kwa sababu wanakosa jambo muhimu nalo ni kuwa na pozi la kumridhisha mwanamke. Haya ni baadhi ya mambo unayofaa kufanya na kujiepusha wakati unaweka mapozi yako.

Usijaribu:
1. Kuangalia chini wakati mnapoongea
2. Kuifunga miguu au mikono yako
3. Kuyainamisha ama kukunja mabega yako
4. Kuingiwa na wasiwasi wa kutulia pahali pamoja

Fanya:
1. Angalia mbele
2. Weka shingo yako sambamba , usilaze kichwa
3. Mabega yaweke nyuma ya kiuno, yalaze chini
4. Kifua kiweke mbele

Kufanya hivi kutakupa confidence na kutakupa nafasi ya kupumua vizuri hivyo kupunguza wasiwasi wowote ambao unaweza kujitokeza wakati unaongea na mwanamke. Pia hakikisha umechukua nafasi kubwa kwa kujitandaza iwapo umekaa kwa kiti. Hii itadhihirisha ya kuwa pale umekaa unajiamini inavyohitajika. Kama umekaa katika sehemu ya watu wengi hakikisha kuwa wewe ndie umechukua nafasi kubwa zaidi kuliko wenzako.[Soma: Jinsi ya kuongeza kujiamini kwako kwa mwanamke]

2. Nguo ndizo zinazomtambulisha mwanamume
Si lazima uvalie masuti ndio uweze umuuliza mwanamke atoke date na wewe. Na pia simaanishi kuwa uvalie nguo ambazo hazina mvuto. Unachohitaji kufanya ni kuvalia nguo ambazo zinaleweka na safi. Valia nguo ambazo zinakutambulisha wewe na ambazo hazitakusumbua. Valia nguo ambazo zitakuwa handsome guy.

3.  Eye contact
Wakati umeapproach mwanamke hakikisha kuwa kile ambacho unamuuliza ama kumwambia kiwe unamwambia uso kwa uso. Kumtongoza mwanamke ama kutaka umtoe out lazima umwambie ukiwa unamuangalia macho yake. Hii itamfanya yeye kuingiwa na aibu na itakuwa ni vigumu kwake yeye kukataa kwa rahisi.

4. Usifananishe upole wa mwanamke kuwa ni upendo
Wanaume wengi hukosea na kufananisha upole wa mwanamke kuwa unaashiria mapenzi. Ukiona mwanamke akikupa tabasamu ama akismile ukiongea kitu hakumaanishi kuwa amekupenda. Hivyo kama wataka kuhakikisha kuwa mwanamke awe ni rafiki yako au la kama anakupenda fanya kumuuliza kama anaweza kutoka out na wewe. Akiuliza kama ni deti jibu ndio bila kusitasita.[Soma: Hatua za kufanya kama mwanamke hataki kujibu text zako]

5.  Approach yako iweke simple
Wakati unapoapproach mwanamke kumuuliza kama anataka deti hakikisha kuwa wewe ni wewe. Usianze kwa kutumia mambo mengi kama kutumia ucheshi, mizaha ama kutumia mbinu ambazo huna uzoefu nazo. Hii ni kwa sababu pindi mwanamke atakapogundua kuwa unajifanya mtu mwingine, anaweza kukupuuza kwa urahisi. Hivyo ni bora zaidi kutumia mbinu zako za kuapproach demu ambazo tayari umezifanyia mazoezi na kuwa umeziamini.

Je, utamuuliza vipi ili akubali kutoka deti na wewe?
Rahisi sana. Mfano mmoja ni kama unamtongoza jirani yako mwanzo unamchunguza mambo anayopenda. Kama anapenda kuangalia movie unawezakumuapproach kumuuliza kama ashawahi kuangalia movie flani. Akisema hajaiona basi unaweza kuchukua nafasi ya kumwambia hio movie uko nayo lakini bado hujapata nafasi ya kuiangalia, je ungependa tuiangalie pamoja?
Hapa ni mchezo wa maneno ndio unaohitaji kutumia.[Soma: Jinsi ya kuapproach demu ambaye humjui]

6. Siku yenyewe
Kabla ya kumpeleka sehemu uliopanga kumtoa deti hakikisha kuwa sehemu uliopanga kumpeleka unaifahamu vyema. Hii kutaondoa aibu ndogo ndogo ambazo zinaweza kujitokeza. Kama umeamua kumtoa deti mwanamke sehemu ambayo hujawahi kuenda hakikisha umejipeleka sehemu ho siku moja kabla deti yenyewe ili ujitamblize na mazingara ya sehemu hio.
Wakati mko pamoja katika deti yenu. Usianze kuongeamengi kujihusu wewe. Kuwa simple na umakinike kwa kila neno ambalo nitatoka kinywani mwa mwanamke uliyemtongoza.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.