Hatua Za Kujijeuza Kuwa Mwanaume Alpha


Mwanaume Alpha inamaanisha mwanaume ambaye kila mwanaume anatamani kuwa kama yeye na kila mwanamke anatamani kuwa naye. Kulingana na mtandao wa Business Insider, hawa wanaume wanachulikuwa kama ‘wanaume wa kweli’ kwa sababu wanafanikiwa katika kila nyanja ya maisha: kuanzia kudeti hadi kibiashara. Karibu kila mwanaume anataka kujua jinsi ya kuwa Mwanaume Alpha ili aweze kuwawini wanawake kiurahisi. Watu wengi wanadhania kuwa Wanaume Alpha ni kipawa ambacho mtu anazaliwa nacho, lakini ukweli ni kuwa inaweza kuwa rahisi kwa wewe kujeuka kuwa Mwanaume Alpha kirahisi sana. Lakini pia fahamu hauwezi kujeuka Mwanaume Alpha na siku moja, kuna hatua kadhaa ambazo unapaswa kuzifuata ili uweze kufanikiwa mwishowe.


Jambo la kwanza ambalo ni muhimu na ni lazima kulifuata ni kuwa na confidence. Hili ni jambo la kwanza ambalo unahitaji kulikumbuka, na jambo nilingine ni kuwa mwonekano wako, elimu yako na fedha unazomiliki hazitakusaidia ili ujeuke Mwanaume Alpha. Wanaume Alpha karibu wote huwa hawana woga wa kuapproach mwanamke. As long as uko na confidence, utapata watu wakikuheshimu kirahisi. Kwa bahati mbaya, ni vigumu kuiga confidence, jambo ambalo wanaume wengi wanashindwa kujeuka kuwa Wanaume Alpha wa kikweli. Pia kama wewe unatabia ya kujishukushuku, hautaweza kuwa na njia ambayo unaweza kuwavutia wanawake aina yeyote ile ama kuweza kudeti mwanamke nyakati za usoni.

Kama unataka usaidizi wa kuongeza confidence yako, basi unahitaji kumakinika kwa kuangalia hio sehemu. Mfano waweza kununua nguo za fasheni na ubadilishe hairstlye ya nywele zako ili upate ile sura ya mwonekano wa mafanikio. Hii ni njia hakika ambayo itakusaidia kuonekana na mafanikio na confidence baada ya muda flani. Halafu fikiria mambo ambayo umebarikiwa nayo kuanzia kimwili na kiakili halafu umakinike kwa kukuza mambo hayo ili uweze kuyatumia wakati unapotangamana katika jamii. Mfano kama unakipawa cha kuchekesha watu basi tumia kipawa hicho kuongeza nafasi yako ya kuwa Mwanaume Alpha, vivyo hivyo kama umebarikiwa kuwa mrefu tumia kipawa hicho kadri uwezavyo.

Sasa, inapaswa kueleweka vyema kuwa ufidhuli na confidence/kujiamini ni mambo mawili tofauti. Watu wengi wanadhania kuwa Wanaume Alpha hua wanapenda sana kupiga makelele katika klabu na kupenda kupigana na wengine kabla usiku uishe. La, haya yote si kweli. Ijapokuwa wanawake hutafuta wanaume ambao watawalinda, pia hawamakiniki ama kushughulika na wanaume ambao wanakasirika haraka. So badala ya kujigamba kujihusu wewe mwenyewe kila wakati na kuongea sana, ni bora zaidi ujiamini wewe mwenyewe ndani ya mwili wako.

Bila kubahatisha, kujijeuza hadi kuwa Mwanaume Alpha kunaweza kukuletea manufaa mengi katika maisha yako tofauti tofauti, ikiwemo maisha ya kudeti. Upande wa kutongoza utakuwa rahisi, na zile mbinu zote za kutongoza ambazo tumeziandika katika blog yetu ya Nesi Mapenzi zitakuwa rahisi kuzitimiza.

Ijapokuwa inaweza kuchukua muda mpaka uzijue na kuzielewa mbinu hizi vizuri, kila mtu anaweza kuzisoma na na kuzielewa kama anataka kuwa na damu ya Mwanaume Alpha ndani yake.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.