Mambo 9 Ya Kuzingatia Ili Umpate Mpenzi Wako Uliyetabiriwa (Soulmate)


Watu wengi huchukua miaka yao yote kutafuta yule mchumba ambaye atamfaa maishani. Tatizo ni kuwa wanaambulia kwa mtu ambaye wanawazoza kimaisha na mwisho wanajutia kwa nini wamejiingiza kwa mahusiano hayo. Lakini wengi wanasahau ya kuwa mpenzi ambaye anakufaa (soulmate) ni rahisi kumpata kama utazingatia maswala fulani.
Kwanza lazima ufahamu ya kuwa kila mtu hapa duniani huwa kawaida ana mpenzi anayemfaa, ni vile tu mara nyingi kuna mambo ambayo tunayapuuza hivyo inakuwa vigumu kumpata mpenzi kama huyu.

Mara nyingi tunamakinika na wapenzi ambao tunaona wazi kuwa hawatufai lakini kwa kuwa unaamini mapenzi si mteremko, inakubidi uingie katika mahusiano na mtu ambaye hakufai.

Lakini leo tumekuja na mambo ya kuzingatia ambayo yatakuwezesha hadi ukutane na mpenzi uliyetabiriwa kuwa naye.

Zama nami!

#1 Kuwa wewe mwenyewe bila kuiga tabia za wengine.
Kitu cha kwanza ni kuwa kama unataka mwenza wako, basi lazima uwe na hulka ambazo zinaendana na wewe. Usijaribu kuiga mambo ambayo hayaambatani na tabia zako. Ukifanya kosa la kuwa mwigo, basi mahusiano ambayo utayaingia na yeyote yule yatakuwa na tatizo kwa kuwa haukuonyesha uasilia wako tangu mwanzoni. [Soma: Mambo mwanamke huangalia kabla kukupenda]

#2 Jaribu kudeti na watu tofauti tofauti.
Hii nayo ni muhimu kwa kuwa utakuwa unachunguza tabia za kila ambaye utakuwa unadeti naye. Kufanya hivi kutakupa taswira ya mpenzi ambaye unamwona anakufaa na bila shaka mwisho utaangukia kwa yule ambaye atakuwa mpenzi wako wa kweli.

#3 Ishi maisha ambayo unayatamani.
Ukiwa unatamani upishi, kuparty, kuogelea, kuingia kwa maktaba ama chochote kile basi ni bora zaidi uanze kuyafurahia maisha hayo. Hii ni muhimu kwa kuwa utakapokuwa unayatimiza maisha yako kwa kufanya mambo kama haya, unaweza siku moja ukakumbana na mchumba ambaye umetabiriwa kuwa naye.

#4 Jaribu mambo mapya.
Kama unapata tatizo la kupata mwenza ambaye atakufurahisha, basi unafaa ujiulize iwapo sehemu unazotembea ama mambo unayofanya yanachangia katika masaibu yako. [Soma: Zijue sababu zinazofanya mtu kupenda]

Ukiona ni hivyo basi itakubidi ujaribu mkondo mpya. Iwapo ulikuwa wewe ni mtu wa klabu basi acha uanze kutembea ufuoni mwa bahari ama tembelea sehemu tofauti za burudani kando na zile ambazo umezizoea. Hii itakupa nafasi ya kukutana na watu wengine wapya ambao wanaweza kuwa na hulka tofauti hivyo kumpata yule ambaye anakufaa maishani.

#5 Kubali kubadilika.
Labda mambo ambayo yanatuzuia sisi kupata wachumba wanaotufaa ni kwa sababu hatukubali kubadilisha mitazamo yetu. Hivyo ni bora kuibadilisha misimamo yetu ya mambo fulani ili tuweze angalau kupata wapenzi wanaotufaa. Na kubadilisha mitazamo yetu ni rahisi sana. Mfano ikiwa ulikuwa unapenda kuwa na mchumba ambaye ni mrefu basi tafuta wale wafupi. Ama ulikuwa ulikuwa unapenda weusi tafuta weupe…unanielewa hapo? [Soma: Zijue sababu zinazofanya mtu kuchepuka]

#6 Usiache nafasi ikuponyoke.
Wengi wetu wanakwamia hapa. Labda ni mwanamke umemuona ana hulka zote ambazo unazipenda lakini unaogopa kumuapproach. Unaishiwa kujutia kwa nini hukuchukua nafasi ya kumuapproach mwanamke huyo pindi anapopotea kwa macho yako.

Pia kwa wanawake vivyo hivyo. Hupaswi kuacha nafasi hii ikuponyoke. Mfano rafiki yako anajaribu kukuunganisha na rafiki yake mwingine halafu unakataa…labda unayemkataa ndie aliyetabiriwa kuwa na wewe.

#7 Endelea kutafuta. Usitulie hadi ule wakati utakuwa na furaha.
Kama mahusiano ambayo uko nayo sahizi hayakufurahishi, inamaanisha ya kuwa mpenzi uliye naye si yule uliyetabiriwa. Hivyo usisite na hapo. Endelea kumtafuta maana ipo siku utampata tu kama utazingatia masharti yetu.

#8 Deti mtu ambaye anakuelewa.
Kama tulivyoeleza katika hoja yetu ya #2, hakikisha ya kuwa yule ambaye unatoka naye deti anakuelewa. Kama hamuelewani basi mahusiano yenu hayana maana. Mfano kama mizaha yako haielewi, kama kuna hoja ambazo hazipendi na wewe unazipenda ama chochote ambacho anakipinga kutoka kwako, basi huyo hakufai na unapaswa uvunje uhusiano huo haraka iwezekanavyo.

#9 Lazima uwe na kemia na yule unayemdeti.
Hili ni jambo la maana katika zote. Ishara ya kwanza ya kuzingatia kwa yule ambaye ametabiriwa kuwa wako kawaida huwa kuna kemia kati yenu. Wazungu huiita ‘chemistry’. Chemia hii hutambulika kirahisi kuanzia moyo kwenda mbio, tumbo joto, malaika kusimama na ishara nyingine nyingi. Kama huyo unayemzimia haonyeshi ishara zozote kati ya hizi tatu nimeziorodhesha basi hakufai. Huyo hawezi kuwa mbashiriwa wako…upo!

Kazi kwako sasa. Tegea chapisho jipya kutoka hapa hapa blog ya Nesi Mapenzi.


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.