Hatua Za Kumkiss Mwanamke Kwa Mara Ya Kwanza


Kumkiss mwanamke kwa mara ya kwanza si rahisi. Kuna mambo ambayo lazima uyaangalie kabla kuchukua hatua yoyete. Kuna rafiki yangu mwingine anaitwa Sam alikuwa na mwanamke anampenda. Hakujua jinsi atamuaproach vipi. So baada ya kumkochi mara kadhaa akaweza kumuapproach na uzuri alifanikiwa na akakubaliwa.


So mambo yalikuwa shwari na baada ya wiki tano hivi nilimuuliza Sam uhusiano wake na huyo mwanamke ulikuwa vipi. Aliniambia yuko sawa lakini tatizo ni kuwa tangu ameet naye hajawahi kumkiss. Well, sikushangaa kwa kuwa jambo kama hilo hutokezea haswa iwapo hujapata kuelewa mbinu ya kutumia kumkiss mwanamke. Wengi huogopa kuanzisha mchakato wa kumkiss mwanamke kwa kuwa wanaogopa kupigwa kofi ama mbaya zaidi kukataliwa kabisa.

Najua watu kama Sam ni wengi huko nje. Kuna baadhi ya wanaume wanaweza kuongea na mwanamke lakini wanashindwa kufunga mchezo. Na kufaulu kuufunga mchezo kunaanza na kumkiss.

So leo tumeamua kumaliza tatizo kwa Sam yeyote ambaye anakumbwa na tatizo hili. Je, uko tayari kujua mbinu za kutumia kumkiss mwanamke? Zama nasi. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke akukiss wa kwanza]

#1 Tafuta sehemu ya faragha.

Ukitaka kumkiss mwanamke, lazima uanze na sehemu ya faragha. Huwezi kumkiss mwanamke mara ya kwanza hadharani. Si kawaida haswa katika tamaduni zetu za kiafrika. So mpeleke sehemu ambayo imetulia mkiwa nyinyi pekeenu. Kusikuwe na chochote ambacho kinaweza kuwasumbua ikiwemo simu ama watu kujitembelea ovyo. Sehemu ambayo ina mwangaza wa chini ni bora kwenu.

#2 Usimwambie akukiss.

Ijapokuwa kumwambia mwanamke akukiss ni ishara ya kudhihirisha ujuba, mara nyingi mbinu hii huwa haifanyi kazi. Wanawake hupenda kuwe na kemia ya kimapenzi na usisimuzi kwanza kabla ya kumkiss mwanaume. So hakikisha ya kuwa unamtamkia maneno haya iwapo tu tayari anataka kukukiss.

#3 Kaa karibu na yeye na umpe mahaba.

Kwa wale wanaoanza, kaa karibu na yeye. Na mwishowe tafuta kisababu cha kukaa na yeye karibu zaidi. Unaweza kutumia mbinu ya kujifanya unasoma kitabu na yeye ama kumuonyesha chapisho la udaku kutoka kwa mtandao.

Usianze mahaba kwanza. Ongea mambo matamu kumhusu, ama mambo mazuri ambayo nyinyi wawili mmepitia mkiwa pamoja. Halafu baada ya kumchangamsha, unaweza kuzungumza maswala ya undani ya mahabateni. [Download: Kitabu chetu cha maneno matamu ya Mahaba]

#4 Mguse mara kwa mara.

Tumia mikono yako kulisha vidole vyako kwa ngozi yake mara kwa mara. Unaweza kufanikisha mbinu hii kwa kumwambia kuwa ngozi yake ni laini huku ukiitomasa. Fanikisha haya kwa kumgusa kwa upole.

#5 Usilete ucheshi wala kucheka. 

Unaweza kuwa mtu mcheshi sana, lakini wakati huu uweke ucheshi wako mbali. Ucheshi huua moods za kimapenzi ambazo tayari zimejijenga. Cha kufanya hapa ni kuzungumza kwa mvuto na kwa sauti ya chini. Angalia mwenendo wake uone kama atarespond chenye wewe unafanya. Ukiona ameanza kuzungumza kwa upole huku anavuta sauti yake basi hapa uko karibu kumkiss huyu mwanamke bila wasiwasi.

#6 Muweke katika hisia zifaazo.

Iwapo huyu mwanamke anacheka, anaweka mizaha katika maswala muhimu, ama kuongea na sauti ya juu, basi huyu hajaingia katika hisia zifaazo za kumkiss. So la kufanya hapa ni kushika mikono yake na uanze kucheza na vidole vyake. Weka viganja vyake kwako na uanze kuvitomasa viganja au mkono wake. Hapa ijapokuwa anaweza kushangazwa na hatua yako, mwisho atatulia na atakuwa na hisia tulivu. [Soma: Dalili ya kuonyesha kuwa imefika wakati wa kumkiss mwanamke]

#7 Mpe busu kwa shavu lake.

Hapa ndipo kizungumkuti huanza, lakini pia huu ndio mlango wa kwanza kwa mwanamke kukukiss. Ukiona ametulia na amukuwa na moods kama zako, anza kuongea kuhusu mahusiano yenu huku ukitaja jinsi umefurahia tangu umjue. Na wakati umemaliza kumwambia maneno kama haya, kwa urahaka unaendea kwa shavu lake na unambusu. Ukishafanya hivyo tu, tabasamu. Pia yeye atabasamu.

Ukiwa unaogopa kumbusu kwa shavu, unaweza kuushika mkono wake na kuubusu. Hii inafanya kazi kama vile kumbusu kwa shavu.

#8 Soma reaction zake.

Je amefanyika nini baada ya kumkiss? Je ameingiwa na aibu ama ameshangazwa? Kwa vyovyote vile, wewe umembusu shavu so hawezi kukukasirikia.

Kama ameshikwa na aibu, basi amependezwa. Kama ameshangazwa usiwe na wasiwasi sababu utakuwa umeharakisha mambo. So rudi tena uanze mchakato mzima  wa kuanza kumtomasa ili aingie katika mood hadi aingiliane.

#9 Mkiss tena kwa shavu.

Kama amefurahia ulipomkiss awali, basi ni wakati wa kurudia tena. Wakati huu mbusu kwa shavu lake lakini pia ulete hadi karibu na kuugusa mdomo wake. Lisha kwa sekunde kadhaa sehemu hio. [Soma: Mfanye mwanamke akufukizie]

#10 Soma reaction zake kwa mara nyingine.

Sasa hapa umechukua hatua ya mbele zaidi. Je amependa? Macho yake ameyafunga huku akiskizia utamu ama ameyafungua macho yote akikuangalia kama kwamba umemkosea?

Kama anaonekana kuchanganyikiwa, mkiss kwa mara nyingine. Kama anaonekana kuwa umemkosea, basi rudi nyuma ujifanye kana kwamba ulikuwa tu unambusu kiurafiki. Ipo siku nyingine unaweza kufaulu.

Iwapo atashikwa na haya ama aibu na labda kukusongelea zaidi, basi hapa ushafaulu. Mkiss kwa midomo yake. Hapa lazima amependa na anataka zaidi.

Usivunje tenshen baada ya busu lenu la kwanza. Kaa karibu na midomo yake. Kama anakupenda na anataka umkiss tena, basi bila shaka atakupa ishara kuwa anataka busu jingine.

So ndio huu mpango mzima. Nilimuelekeza Sam kuifuata mbinu hii na baada ya kutoka deti na huyu mwanamke, alinipigia simu kuwa amemkiss na alifaulu. Je wewe utatoboa? [Soma: Zijue ishara za mwanamke mwenye kiu]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.