Majukumu Mjeuko- Mfanye Mwanamke Akufukuzie


Kila mwanaume anapenda kufukuziwa na mwanamke. Lakini tatizo ni kuwa ni baadhi tu ya wanaume wanaojua mchezo wa kuwafanya wanawake wawaandame mara kwa mara.
Ok. Najua kuna wakati flani ushawahi kujiuliza maswali ukitaka kujua ni kivipi yule rafiki yako ama yule jamaa unaemuona kila siku anapendwa kufukuziwa na wanawake anafaulu kuwavutia wanawake kiurahisi. 

Jibu tunalo.

Ujanja mzima wa kufanya wanawake wakufukuzie ni kitumia majukumu mjeuko. Zama nami.


Jinsi ya kumfanya mwanamke akufukuzie


1. Mfanye atake zaidi
Kumfanya mwanamke atake zaidi kutoka kwako ni rahisi sana. Mwanzo unafaa kitumia mbinu ya kumtawala kihisia ambayo nimeifafanua mbeleni. Baada ya kufanya hivyo, ujanja wa kumfanya mwanamke atake zaidi kutoka kwako ni unaweza kumweleza kuhusu issue flani lakini usimalize kumwelezea. Mfano kama unaongea naye, unaweza kumwambia kuwa kuna vitu vitatu ambavyo umependezwa navyo kutoka kwake. Mwelezee kuhusu vitu viwili halafu hio ya tatu mwambie ya kuwa utamwelezea siku nyingine. Ukitaka unaweza kumfafanulia kwa kumpa fununu kuhusu hilo jambo la tatu lakini usimweleze ni nini.
Kufanya hivi kutamfanya mwanamke kama huyu kuingiwa na hamu ya kutaka kujua zaidi ni kitu gani ambacho unataka kumwelezea lakini unamficha. [Soma: Mfanye mwanamke aathirike na penzi lako]

2. Usijibu simu zake
Hata kama unampenda kiasi gani, jifunze wakati mmoja au mwingine usipokee simu zake. Baada ya kupata namba yake, unafaa kujifunza kutopokea siku zake halafu baada ya hapo mtumie text ukimuuliza alikuwa ana tatizo gani. Kufanya hivi kutamfanya kuingiwa na mawazo kama ulikuwa buzy kiasi gani mpaka umekataa kupokea simu yake. Pia anaweza kujiuliza iwapo kuna wengine unaoongea nao.

3. Mfananishe na mhusika wa kubuni
Ok wakati umetoka kuangalia filamu flani, unaweza kumfananisha na mhusika mmoja katika filamu hio. Akikuuliza kwa nini umemfananisha na mhusika huyo usimpe jibu bali toa tabasamu. Kufanya hivi kutamfanya aanze kukuwaza zaidi. Utamfanya ajaribu kuangalia filamu hio kutaka kujua tabia zake na huyo mhusika ni zipi. Mwanzo utakuwa mkono wa mbele iwapo umemtajia filamu ambayo bado hajaiona. Mwishowe unaweza kumwambia tabia zake na mhusika huyo ni zipi iwapo ashaangalia filamu hio baadae. Unaweza kuangalia hilo chapisho kutoka Elitedaily.com.

5. Zuia migusano yenu
Hili ndilo laweza kuwa jambo gumu zaidi kwa mwanaume kufanya ili kumfanya mwanamke amfukuzie. Jambo muhimu hapa ni kuhakikisha ya kuwa unauteka moyo wa mwanamke. Kimsingi, kama ataingiliana na wewe na kuanza kukupa kiss ama vitu kuanza kushika moto, jizuie na kumwambia ya kuwa hauko tayari kwa jambo hilo, na kuwa unataka kufanya mambo polepole. Tofauti na hatua tulizozieleza hapo juu, hii haufai kumpatia sababu yeyote ya kwa nini umeamua kujizuia. Hii ni njia ya uhakika ambayo itampagawisha kukutaka zaidi. Lakini fahamu ukitumia mbinu hii kwa mwanamke utamfanya mchana na usiku asiwe na amani mpaka ile siku utampatia haki yake. Na akifaulu hatokuacha kirahisi. [Soma: Unajua kwa nini lazima ufanye mapenzi na rafiki yako?]


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.