Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akutambue Bila Hata Kuongea Na Yeye


Katika kitabu chetu cha Kutongoza Mwanamke Kuanzia Hadharani Hadi Kitandani tumeongea swala muhimu ambalo linahusu kumfanya mwanamke aone kama amekujua tangu zamani ilhali umekutana naye tu sahizi. Mbinu hii ya kisaikolojia inaitwa sanaa ya mazungumzo. Mbinu hii huwa na mafanikio ya asilimia mia iwapo utaifuata vile inavyotakikana.


Hata hivyo, kuna mbinu nyingine ambayo inafuata mfumo uo huo wa sanaa ya mazungumzo lakini hapa utatumia matendo ili mwanamke aweze kukutambua ama akunotice kiuharaka. Nayo katika sanaa ya mazungumzo utatumia matamshi kumfanya mwanamke akuone kana kwamba alikujua tangu zamani.

Uzuri wa kutambulika na mwanamke huwa kuna faida ya kuwa pindi utakapo muapproach na ufunguke kuwa unampenda, itakuwa rahisi kwake kukubali mwitiko wako.

Kutambulika na mwanamke ni rahisi. Unachohitajika ni kuhakikisha kuwa unafuata masharti ambayo tumeyaorodhesha hapo chini:

#1 Jitambulishe.

Umekuwa ukikutana naye mara kwa mara lakini bado hajakutambua. So wewe unafaa ujiletee atenshen ili akuone. Hapa itafanikishwa kirahisi wakati ambapo unakuwa kwa kikundi. Hakikisha wakati mwanamke huyu anapotokezea, kuwa mchangamfu katika kikundi chako. Ongea na marafiki zako huku mkienjoy muda wenu. Huu utakuwa mwanzo wa yeye kuanza kunotice uwepo wako.

#2 Valia vizuri.

Valia kistaarabu. Unaweza kuvalia nguo ambazo zinaweza kukutambulisha kama bilionea flani hivi. Usiogope kuwa tofauti na wengine. Lakini pia usipitishe kiwango cha kuvalia hadi ukaonekana kuwa lengo lako ni kutafuta atenshen kwa huyu mwanamke.

#3 Mwangalie machoni mara kwa mara.

Baada ya kutambua uwepo wako kwa muda, sasa una nafasi ya kuhakikisha ya kuwa unachukua hatua nyingine ya kumuonesha kuwa una interest na yeye. Na kutimiza haya ni kwa kutumia miondoko ya macho. Hapa Nesi Mapenzi tayari tushaeleza umuhimu wa kutumia macho na mbinu tofauti tofauti za kutumia macho kuhakikisha kuwa mwanamke anavutiwa na wewe.

#4 Kuwa na ujuba ndani yako.

Mwanaume mwenye tabia za ujuba huwa wanapendwa sana na wanawake. Wanaume aina hii hujiamini kwa kile ambacho wanafanya. Mfano ukijiamini, unaweza kufanya jambo lolote bila kuogopa kuwa utachekwa ama utafeli. So kwa mfano, ukimwona huyu mwanamke ameingia kwa baa, unaweza kuenda kuchukua mic na uanze kuimba karaoke, ama unaweza kuingia katika mashindano na marafiki zako. Mwanaume mwenye hulka za ujuba haogopi kufeli ama kuchekwa. [Soma: Jeuka mwanaume ujuba kwa kufuata hizi hatua]

#5 Wajue marafiki zake.

Kama hutaki kubahatisha kuongea naye moja kwa moja, unaweza kujitambulisha kwa marafiki zake wakujue. Hapa inaweza kuwa marafiki zake wa kiume ama wa kike. Haina tatizo. Ukiwavutia, wataweza kukusifia kwa huyu mwanamke unayemvizia.

#6 Jiamini. 

Kujiamini ni kila kitu kama unataka kuwavutia ama kuteka atenshen ya wanawake. Kujiamini ni dalili moja ya mwanaume alpha. So utajiamini vipi? Lazima uongee bila woga, kusimama wima, tembea kama mtu jasiri na kadhalika. Haya ni  baadhi ya mambo ambayo lazima uwe nayo. [Soma: Hatua za kujiamini]

#7 Tembea zile sehemu anazopenda. 

Kama mara kwa mara utakuwa unatokezea kwa zile sehemu ambazo anakuwa, mfano katika mkahawa, klabu, ufuoni nk, basi ni bora pia uwe unatangamana na marafiki zako katika hizo sehemu. Hii itamfanya azoee uwepo wako na pia atajihisi huru mbele yako kwa kuwa anakuona sehemu ambazo anazipenda.

#8 Kutana naye katika mazingara yasiyo ya kikazi/chuo

Kwa kuwa sahizi umetengeneza mazingara mazuri yako na yeye mkiwa katika shughli za kikazi ama chuoni, sasa ni wakati wa kukutana na uongee naye mkiwa nje ya kazi/chuo. So kufanya hivi jaribu kutafuta plan zake za wikendi atakuwa wapi. Unaweza kuwauliza marafiki zake upate kujua.  Hakikisha ya kuwa sehemu utakayoenda uwe na marafiki zako ama pekeako. Pia hakikisha ya kuwa hajui ya kwamba tayari umempangia kukutana naye hio siku.

So ukimwona katika hio sehemu aliyokuja, tumia mbinu ya kumwangalia kwa macho. Mwangalie kwa kwa sekunde halafu jifanye kwamba umechanganyikiwa hujui umwambie hi! ama ujipe shughli. Halafu rusha tabasamu  huku ukiwa unajifanya kuwa umeshangazwa na uwepo wake. Kama tayari ashakuona mara kwa mara awali, bila shaka atakuwa ashakunotice na atakutabasamia.

Pindi ukiona ametabasamu kwako, basi chukua nafasi hii ya kumuapproach na uongee naye. Mafanikio kwako.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.