Jinsi Ya Kumpata Mwanamke Kwa Njia Rahisi


Kila mwanaume ashawahi kupenda mwanamke spesho katika maisha yake. Unamjua wewe mwenyewe. Ana hulka ambayo ulipendezwa nayo, ana uso mzuri na nywele za kuvutia. Lakini tatizo ni kuwa anadeti wanaume bora mara nyingi, so utafanyaje mpaka akuone kuwa wewe ni bora pia na umfanye anotice uwepo wako?
Ok, kulingana na maumbile ya wanadamu ni kuwa wanaume huwa wananotice uwepo wa mwanamke kulingana na urembo wake ilhali wanawake wananotice uwepo wa mwanaume wakati hulka yake inang’aa. So, mwanaume bora kwa mwanamke ni Mwanaume Alpha – kiongozi anayejiamini na ambaye anapata kila kitu anachotaka wakati anapotaka. Kuwa Mwanaume Alpha ni njia rahisi kwa mwanamke kukupenda, kwa haraka sana.


Unapotaka kuchukua atenshen ya mwanamke, hakikisha kuwa hauonyeshi tabia ya uhitaji mwingi, bali mwonyeshe kuwa anapaswa kufanyia kazi ili aweze kupata time aspend na wewe. Yaani kwa njia rahisi ni kuwa unapaswa kuonyesha kuwa haujali kama yuko interested na wewe au la. Lakini pia usimfanye afikirie kuwa wewe ni changamoto kwake, bali kuwa changamoto wewe mwenyewe.

Kando na kuweka thamani yako mwenyewe, unapaswa kuipanua himaya yako ya kutangamana na wengine yaani ongeza idadi ya marafiki zako na pia wanawake wengi. Uzuri ni kuwa wanawake ni rahisi kuwa marafiki nao. So hakikisha ya kuwa unatangamana na wengine. Kufanya hivi hakutaongeza thamani yako mbele ya jamii pekee bali pia inakuwa kama kichocheo cha wewe kuweza kuwa na confidence mbele ya wanawake. Pia hakikisha unatoka deti na wanawake wengi kadri iwezavyo. Hii itakupa nafasi ya wewe kujifanyia zoezi ili ile siku utatoka deti na mwanamke unayempenda haitakuwa tatizo kubwa.

Kama mawazo yako yamejikita kwa maneno kama, “Nahitaji kumuwin huyu mwanamke”, “Huyu mwanamke anapaswa kuwa wangu pekeangu”, ama “Siwezi kuacha kumfikiria”, basi jizungushe na wanawake na matatizo ya fikra kama hizi zitakuepuka.

Tena, wakati wanawake wanapowaona wanawake wengine wakitangamana na mwanaume flani, watafanya bidii pia na wao watangamane na mwanaume yuyo huyo. Hii inajulikana kama ithibati ya kutangamana na huwa ina nguvu sana wakati inapotumiwa kwa wanawake. Kama umeshawahi kumuona mwanaume akiandamwa na wanawake wengi, basi hio itakuwa ithibati ya kutangamana kwako.
Sasa, kwa kuwa hakuna tatizo lolote la kuona mwanamke anayevutia na ambaye unahisia na yeye, unapaswa kujikumbusha kuwa kuna wanawake wengine wengi na warembo ambao wanaweza kuwa wazuri kama vile alivyo mwanamke wa ndotoni mwako. Kama utaendelea na kuwa na mawazo ya kuwa mwanamke wa ndotoni mwako hawezi kubadilishwa na mwingine, basi atashikilia nguvu juu yako na mwishowe atapoteza hamu na wewe. Kumbuka – kuwa Mwanaume Alpha. Chukua control katika hali kama hii na utampata bila kupoteza wakati.

Ok, ni vizuri kumwona kuwa ni mwanamke bora, lakini fahamu kuwa kuna wanawake bora zaidi kule nje. Hii itasaidia kuondoa uhitaji mwingi, na kukufanya kuonekana kuwa na thamani na kuweza kumpata mwanamke umemweka ndotoni mwako mwishowe.

1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.