Sababu 20 Zinazokufanya Usiwe Na Girlfriend


Tangu ujielewe umekuwa single. Huna girl friend ama mpenzi yeyote yule. Kuna yule mwanamke jirani yako kila siku unamwona. Unamtamani lakini hutaki kumuapproach. Kiufupi unaishi kiupweke ilhali marafiki zako kila wakati wanaonekana na wanawake tofauti tofauti.

Hii ni hali ambayo inatokea kwa wanaume wengi duniani. Usijione kama ni wewe pekeako. So shida huwa inatokea wapi? Nesi Mapenzi tumekuja na sababu ambazo zinakufanya wewe ubaki single milele.

#1 Hautaki kujaribu. Kuna wanaume wengi ambao wanalalamika kuwa hawana wachumba lakini hapo hapo hawatii bidii kuhakikisha kuwa wanatafuta mmoja. Usipojaribu kutongoza mwanamke basi utabaki hivyo hivyo single milele.

#2 Unatafuta mwanamke aliyekamilika. Wanaume wengine hufanya kosa la kutafuta wanawake warembo zaidi katika hii dunia. Hili ni jambo ambalo hutalipata. Kama utasema hutafuti mwanamke mpaka awe anafanana na Masogange ama Huddah Monroe basi utangojea sana.

#3 Hauko huru. Si jambo baya kuishi na wazazi wako. Wanaume wengi bado huishi na wazazi wao. Lakini kuna time ikifika, haswa miaka ya mwisho mwisho ya ishirini, unahitajika angalau ujitenge kiasi. Kwa nini? Hii ni ishara ya kuonyesha wanawake kuwa umekuwa mkubwa...unless uwe mswahili itakubalika.

#4 Kama umekataliwa, unakata tamaa. Kukataliwa ni hali ya maisha. Itakuwa labda hata umekataliwa kazi ama kujiunga na shule flani. Hio pia ni kukataliwa. Haina utofauti na kukataliwa na mwanamke. Lakini sasa shida yako ni kuichukulia binafsi. Yaani ukikataliwa na mwanamke mmoja basi wewe unaamua kujitenga kabisa na wanawake. Haifai.

#5 Bwana Mzuri. Kuwa mtu mzuri na karimu ni jambo zuri. Lakini pia ujue kuwa wanawake hawapendi mwanaume ambaye ni mzuri kupindukia. Kama hauko ngangari ama mkakamavu basi hufai. Wanawake wote utawaita mashemeji.

#6 Kila kitu ni wewe. Kuna wanaume ambao katika kila mazungumzo lazima waingilie kati. Wao ndio wanaanza mazungumzo na kumalizia.Wanapenda sana atenshen. Hii ni tabia ambayo wanawake wanaichukia na hawapendi aina hii ya wanaume. Kama unajijua uko na hii tabia basi ni vigumu kwako kuwa na girlfriend.

#7 Unahitaji kuoga. Tuseme kweli. Kuna wanaume wengine ni vigumu kwao kuoga. Kila wakipita sehemu yeyote unaskia harufu mbaya. Wanawake hawapendi aina hii ya wanaume. Kinachohitajika kufanya ni kuoga na sabuni. Nenda kinyozi unyoe nywele. Labda ilikuwa ni ishu ndogo ya usafi wa mwili ndio ilikuzuia usimpate mwanamke unayemtamani.

#8 Hujiamini. Wanaume wengi huwa hawajiamini ikija katika swala la kutongoza. Wasiwasi, kujishuku, woga kunafanya wengi wabaki single. Jeuka sasa ama itakuwa ngumu kwako.

#9 Unangojea akuaproach wa kwanza. Kama wanawake wangekuwa na uwezo wa kuapproach wanaume dunia ingekuwa sehemu nzuri yakuishi. Lakini sivyo. Ni wanawake kidogo sana ndio wanamoyo huo. So usingojee mwanamke akuapproach. Anza wewe ama utabaki hivyo hivyo.

#10 Unaona aibu katika kundi lako. Wanawake hawapendi wanaume wanaoona haya. Si vibaya kuwa na hulka ya kuona aibu, lakini usizidishe. Wanawake watakuona uko na tatizo. Itakuwa vigumu kwako kumuaproach na itakuwa vigumu kwake kukukubali.

#11 Hujui kusawazisha kati ya kazi na kujiburudisha. Mwanaume lazima ajipe time ya kujiburudisha. Kama utasema siku nzima wiki mfululizo utakuwa ukifanya kazi time ya kutangamana na wanawake itakuwa lini?

#12 Unakaa nyumbani na kuangalia movie wikendi nzima. Kuangalia movie ni jambo zuri. Lakini jua kwamba ukiwa unaangalia movie wikendi nzima basi nawe hutapata kumwona mwanamke unayempenda. Unapaswa kwenda kula bata ukajifurahishe na marafiki zako wakutambulishe kiumeni.

#13 Huonyeshi kuwa unampenda. Labda ni kweli unampenda lakini hujawahi kumuonyesha kuwa kweli unampenda. So nyinyi wawili ni marafiki wa dhati. Usipomuonyesha kuwa unampenda basi atakuingiza katika himaya ya urafiki akufungie huko milele.

#14 Umejenga ukuta wa hisia. Labda mbeleni kuna mwanamke alikutenda. Ama umeshuhudia rafiki yako akitendwa. So na wewe umeamua kuweka hisia zako mbele. Lakini kama unataka mwanamke basi lazima uubomoe ukuta huo na uanze kutangamana na wanawake hata kama unaogopa.

#15 Unataka maisha yaliyokamilika kabla hujatongoza mwanamke. Unataka nyumba, gari, kazi nzuri...naelewa. Lakini kama unangojea upate vitu hivi vyote kabla upate mwanamke, jua haitafanya kazi. Huwezi kupanga maisha kama yanaendelea.

#16 Unaenda katika sehemu zisizofaa. Kama unaenda gym ya wanaume, ama kwenda kilimanjaro kukwea milima huku ukitarajia ukutane na wanawake basi unaota. Wanawake hawapatikani sehemu hizo. Jaribu kwenda baharini, supermarket, klabu huko hukosi wanawake.

#17 Unafikiria sana bila matendo. Wewe ni yule ambaye tayari ushapanga jinsi utakavyomfanyia mwanamke ambaye bado hata huna namba yake. Changamka ujeuza fikra zako kuwa matendo.

#18 Unafanya mambo haraka haraka. Unampenda huyu mwanamke sana. Leo umetoka naye deti. Kesho na kesho kutwa unataka mtoke deti. Kila siku unataka utoke naye. Kufanya hivi kutamtishia na utamfanya akimbie.


#19 Unajiona spesho. Mbele ya mwanamke usijifanye spesho. Usianze kujigamba kuwa wewe ni hivi na hivi ama uko na hili na lile. Kama wewe ni spesho pia wanawake hujiona spesho zaidi yako.

#20 Hujui kutangamana. Kando na kujiona spesho unapenda kumdharau. Unamwonyesha kuwa yeye si lolole.  Hapa wanawake watakutenga na utajikuta pekeako.

Ok. Haya ni baadhi ya mambo ambayo yanakufanya uwe mpweke usiwe na mwanamke yeyote. Kama una moja wapo ya tabia hizi basi badilika sasa.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.
##valentine ##valentine