Dalili 7 Za Kuonyesha Mwanamke Anakupenda


Wanawake huwa tunatangamana nao kila siku, tunakutana nao kazini, shuleni, majumbani, hotelini na sehemu nyingine nyingi.


Wengine wetu hufikia level ya kuwa marafiki na wanawake hawa. Lakini je utatuaje kama mwanamke huyu anakupenda? Labda umekuwa ukiongea naye lakini interest kwake hauna kumbe kwa upande wake anakupenda. Ishara tunazo.


#1 Anapenda kushika nywele zake
Dalili moja ambayo wanawake hufanya bila wao kutambua kama wamemzimia mwanamume ni pale ambapo anakuwa anashika nywele zake ama kupitisha mkono wake kwa nywele zake bila kwa maksudi yeyote. Hii humfanya kuonekana mrembo zaidi na pia kumpa confidence ya kujitambua yeye mwenyewe. So kama mwanamke unamzimia kila wakati ukiwa na yeye anapenda kufanya huu mtindo basi fahamu kuwa hii ni dalili dhahiri. [Soma: Ishara za kuonyesha mwanamke anataka umpeleke chemba]

#2 Anapenda kutaka kuskiliza kila neno ambalo utaongea
Wanawake wanapenda kujiunganisha kimwili na kihisia. So ukiona kuwa anapenda kukuuliza maswali kukuhusu halafu anakuwa makini kwa kila kitu unachoongea, basi fahamu ya kwamba huyo mwanamke amekuzimia na angetaka kukufahamu zaidi na zaidi. Pia kama anakupenda, ile mizaha yako yote hata kama ni ile ya kijinga utamwona akicheka tu. Hii ni ishara ya wazi ya kuwa umegonga ndipo. Hakikisha kuwa unaitumia nafasi hii vile inavyotakikana.

#3 Atakupa namba yake ya simu bila tatizo
Kama mwanamke anakupenda, huwa kamawaida anajipendekeza yeye mwenyewe kwako. Atakurushia kuhusu dalili zote wakati ambapo yuko free au nafasi ya kuongea na pia atakwambia kuwa angetamani kukutana na wewe wakati mwingine muwe pamoja. Lakini tatizo ni kuwa kwa wanawake wengi si rahisi kumwambia mwanamume watoke out pamoja. So ijapokuwa mwanamke angetamani kutoka date ama out na wewe siku moja, atasalia kungojea maisha yake yote hio siku itimie bila mafanikio. So instead ya kumfanya angojee huu muda wote, wewe ndio unafaa uchukue hatua hio na kumwambia wazi kuwa umemzimia na unataka kutoka naye date ama kumtoa out kiasi.

#4 Anamaintain eye contact na wewe, yaani muda wake wote atakuwa akikuangalia machoni mnapoongea
Kukuangalia macho ni ishara kuu ya kuonyesha kuwa mwanamke amekuzimia. Kama kila wakati unapoongea na mwanamke atakuwa akikuangalia macho yako kwa umakini bila kuangalia pengine ni ishara kuwa anakupenda. Hii inamaanisha kuwa utakuwa umeiteka hisia yake na angetamani kukujua wewe mwenyewe binafsi zaidi. [Soma: Mambo ya kutarajia kama utadeti mpenzi aliyekupita kimiaka]

#5 Anapenda kusimama kando yako
Wanawake wanapenda kusimama karibu na wanaume wanaowapenda kwa sababu inawafanya wao kujiskia huru na kuwa bila wasiwasi. Wakati wowote mwanamke anaposimama kando yako hii kwa urahisi inamaanisha anajiskia yuko salama na huru akiwa na wewe. Hii ni ishara tosha ya kuonyesha kuwa mwanamke kama huyo amekuzimia kwani pia inatambulika ya kuwa wanawake hawapendi kukaa karibu na wanaume ambao wanawachukia na wasiowapenda.

#6 Anatafuta sababu ya kukushika
Wanawake wanapenda kuonyesha hisia zao na dhamira zao kwa jinsia ya wanaume kwa kutumia mtindo wa kuwashika mkono na viganja vyao.

#7 Anakusuka
Ukiona mwanamke anapenda sana kuongea na wewe kwa mitindo ambayo anajaribu kwa njia zozote kukufurahisha na ujiskie kumtamani ni dalili tosha kuwa anakuzimia. Anaweza kutumia maneno ya kukuchanganya akili ili mradi ucheke ama ufurahie.  Hii kwa kawaida huwa anajaribu kujiunganisha na wewe na ni dalili kuonyesha kuwa amekuzimia.

KUMBUKA: Ni muhimu kufahamu kuwa si lazima mwanamke aonyeshe dalili zote hapo juu tulizoziorodhesha ili uweze kudhihirisha kuwa anakupenda. Dalili mbili ama tatu hivi ni ishara tosha. Halafu ufahamu kuwa mwanamke yeyote anaweza kuonyesha baadhi ya dalili hizi so haimaanishi kuwa ukiingia kwa basi la abiria halafu mwanamke akusongelee karibu yako anamaanisha kuwa amekuzimia. [Soma: Jinsi ya kumtongoza mwanamke katika basi la abiria]No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.