Mambo 8 Ya Kutarajia Unapodeti Mwanaume Mzee Kukuliko


Si jambo lisilokuwa la kawaida. Tumekuwa tukiona wanawake wengi wakiingia katika mahusiano ya kimapenzi na wanaume ambao ni wakubwa kiumri kuwaliko. Kila mmoja huwa na sababu zake za kuamua kuingia katika mahusiano kama haya. Wengine wanaweza kusema wanaume wazee wanajua upendo zaidi, wengine wanaweza kuwa wamechoshwa na vijana na wengine labda wanaweza kujikuta katika mahusiano hayo kwa kuwa wanalenga hela.


Well, hayo ni mambo ambayo hufanyika. Kile kitu ambacho tunajua ni kuwa kila mtu anakuwa na maamuzi yake na hatuwezi kuamulia mtu. Kando na hilo, kama umejikuta ama unataka kuingia katika mahusiano na wanaume ambao wamekushinda umri, kuna mambo ambayo unatarajiwa kukumbana nayo.

Leo tumekuandikia mambo ambayo utakumbana nayo katika mahusiano haya na ni kama yafuatayo:

#1 Mawasiliano bora.
Wanaume wazee wako sawa ikija katika maswala ya kuwasiliana. Hii ni kwa sababu mtu mzee anachukulia mazungumzo katika hali ya kiubinafsi. Hawashindwi kueleza matatizo yao wala huwa hawafichi mambo.

So kama umeamua kudeti mwanaume mwenye umri mkubwa kukuliko, basi weka katika akili yako kuwa mahusiano yenu hayataathirika na mawasiliano.

#2 Atakuongoza.
Kwa kuwa mwanaume huyu amekuwa na maisha marefu na ameona mengi, atakuwa mstari wa mbele kukuongoza. Wakati wowote ambao utakuwa na changamoto, yeye atakuwa yuko na wewe kukuelezea jinsi ya kukabiliana na matatizo yako. [Soma: Mambo ya kufanya ili kiwaepuka wanaume wanakuchukiza]

#3 Unaweza kuwa huru.
Huu ndio ukweli, ukiwa unadeti mwanaume mzee kukuliko, utakuwa na nafasi nyingi ya kuwa huru. Kwa kuwa anayajua maisha, hatojaribu kubadilisha tabia zako ama mambo ambayo umeyazoea.

#4 Atakupa mahaba ya kutosha.
Hapa hakuhitaji maelezo ya kina. Tunajua kuwa umri humpa mtu hekima na ujanja. Hivyo ikija katika maswala ya mahaba, wanaume wazee waliokuzidi umri watakuwa wamekolea. Mwache akufundishe maujanja ambayo bado hujawahi kujua.

#5 Hakuna mashindano.
Ukiwa unadeti mwanaume ambaye mko sambamba kiumri ama mumepishana kidogo, kwa kawaida kunakuwa na mashindano na mara nyingi kunakuwa na wivu ndani yake.

Lakini kama unadeti mwanaume aliyekuzidi umri, hii huwa tofauti. Mara nyingi yeye huwa na maisha tofauti kabisa na yale yako. Hivyo inakuwa rahisi kwa nyinyi wawili kusikizana na pia kusaidiana sehemu ambazo kunakuwa na changamoto. [Soma: Jinsi ya kumpata mwanaume yeyote bila tatizo]

#6 Subra.
Tunajua wanawake jinsi walivyo. Wanapenda kujivuta kwa kila mambo. Pia wanakuwa si wasikivu wakati mwingine. Uzuri ni kuwa ukiwa unadeti mwanaume mzee kukuliko ni sahali kwako. Wanaume aina hii wanakuwa na subra zaidi ya wanaume wowote. So ukichelewa kidogo kwenda deti ataelewa. Ukichelewa kupika wakati wake pia atafahamu. Wanakuwa na ule msemo wa ‘yataka timing kumkata kobe kichwa’

#7 Anafuata utaratibu.
Wanawake hupenda wanaume ambao wanakuwa na utaratibu. Wanawake wangependa wanaume ambao kama ataonyesha upendo basi atauonyesha upendo huo bila kusita hata siku moja. Tatizo ni kuwa wanaume wengi hawawezi kuwa na huo utaratibu. Lakini si mwisho hapo, hili kundi la wanaume wazee ama waliokupita umri wanajua vyema kufuata utaratibu huu. [Soma: Jinsi ya kuongea na mwanaume aliyekupendeza]

#8 Wanayafanya maisha yako kuwa rahisi.
Kudeti mwanaume aliyekupita umri kuna raha, utakuwa na uhakika ya kuwa maisha yako yatakuwa rahisi. Kila kitu ambacho ungetamani akufanyie basi atakutimizia bila shida yeyote. Pia atakuwa mstari wa mbele kukulinda kutokana na tishio lolote lile ambalo litajitokeza.

Ok. Haya ni baadhi ya mambo ambayo unapaswa kutarajia iwapo utaamua kudeti mwanaume aliyekushinda umri.
Psss! Lakini pia uchunge usije ukashikwa katika fumanizi manake wanaume wengi kama hawa huwa wameoa na huongoza katika kuwa na michepuko. Tafuta ambaye yuko singo.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.