Jinsi Ya Kumpata Mwanaume Unayempenda Bila Kujisumbua


Wanaume wanajulikana kupenda vitu ambavyo hawawezi kuvipata. Na hii ndio siri kuu ambayo lazima uanze kuifahamu kuanzia sasa. Jaribu hizi mbinu ambazo tutakueleza na utampata mwanaume unayemtaka haraka sana.

Well, siri kuu ya kujua jinsi ya kumpata mwanaume unayempenda ni sahili lakini pia si rahisi kuifuatilia.


So tayari tushajua siri ya wanaume, huwa wanapenda vitu ambavyo hawawezi kuvipata.

So utafanyaje hadi uwe mwanamke aina hii?

Itakuwaje mwanamke ambaye anampemda mwanaume, aweze kumuona mwanamke huyu kiumbe bora zaidi ya yeyote yule?

Ni tricky lakini usijali. Hapa Nesi Mapenzi tuna suluhu la kila kitu ikija na maswala ya mahusiano. Zama nasi.

#1 Fikra za wanaume.

Wanaume wameumbwa kuteseka ili kupata kile ambacho wanahitaji. Na pia wanapenda kujihatarisha kupata kile wanachopenda. Hii ni kuanzia kutafuta sifa, ardhi, chakula ama wanawake.

Ijapokuwa wanaume wanasema kuwa wangependa kupata vitu kirahisi au kwa njia ya mteremko, kwa kawaida hawapendezwi ama kuthamini ubora wa kitu iwapo watakipata kwa njia iliyo rahisi. Haya ndio maumbile yao. So hapa namaanisha usiwahi kuwa mtu rahisi kamwe. Hii ni sheria ya kwanza ya viganja.

#2 Mpe atenshen

Wakati ambapo unaongea na yeye hakikisha ya kuwa unamwangalia machoni. Fanya hivi kwa kutumia madoido, si kama vile ambavyo unaangalia mtu kikawaida. Pia iwapo yuko na marafiki zake ama akiwa anafanya shughli zake unaweza kumuangalia mara kwa mara na akuone kuwa unamwangalia.

#3 Wapendeze marafiki zake

Wakati wowote ambao utakutana na marafiki zake hakikisha ya kuwa unakaa nao na unazungumza nao. Kuwa mtulivu na mwenye bashasha kila wakati. Waonyeshe marafiki zake upendo na wao pia watapendezwa na wewe.

Na pindi ambapo watakutana na yule mwanaume unapendezwa naye, lazima watafunguka na kumwambia jinsi ulivyo mzuri na mchangamfu. Kwa kuwajeuza marafiki zake kukupigia debe, bila shaka ataanza kuona jinsi ulivyo special zaidi ya wengine.

#4 Muulizie kumhusu

Wakati ambapo unakuwa na mazungumzo na marafiki zake, unamuulizia kumhusu. Lakini hapa lazima uwe mjanja kwa kuwa haupaswi kumtaja mara kwa mara. Unaweza tu kutaja jina lake kuuliza kitu kumhusu. Baada ya hapo, marafiki zake bila shaka wataenda wakamwambie kuwa ulikuwa unamuulizia. Hivyo utamwacha akichanganyikiwa na maswali yasiiyokuwa na majibu.

#5 Suka wanaume wengine

Unaweza kuwa umefall na yeye, lakini kama unamtaka mwanaume avutiwe na wewe, lazima ufuate sheria ambazo zinapaswa kuzingatiwa. Hupaswi kuwa ama kuonekana rahisi. Wakati anapokuwa na wewe, ongea naye, lakini usiwapuuzie wanawake wengine. Mkiwa mko pamoja, hakikisha ya kuwa unatangamana na wanaume wengine. Suka wanaume wengine na wala usikuwe na wasiwasi wowote ule. [Soma: Jinsi ya kuongea na mwanaume hadi apendezwe na wewe]

Kumbuka ya kuwa hapa unafuata sheria tuliyoielewa awali. Hapa utakuwa unamfanya mwanaume huyu kuwa na shauku ya kutaka kukujua zaidi. Kwa kusuka wanaume wengine kunampa changamoto mwanaume huyu ili awezenkuongeza gemu yake na ajaribu zaidi na zaidi kupata atenshen yako.

Utamwacha akijiuliza iwapo kweli unampenda au la. Na pia atachanganyikiwa kwa nini unamuulizia. Hapa ndio zile hisia za kiume zinapokuja na kutaka kukujua zaidi na kujaribu kuteka atenshen yako.

Kumbuka kuwa haupaswi kamwe kujiachilia na kuwa rahisi. Wanaume wako radhi kukufukuzia hata zaidi ya mwaka. Hivyo ni wewe wa kuamua ni muda gani umeona kuwa mtego wako umefaulu.

Mafanikio kwako!No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.