Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili


Je wewe ni miongoni mwa wale ambao wameshawahi kupendwa na mwanamke halafu baadae mwanamke huyo akapoteza interest na wewe? Ama ushawahi kumfukuzia mwanamke halafu ukaona kuwa unafaulu lakini baada ya masiku kadhaa mwanamke huyo akapoteza interest na wewe ghafla.


Hali hii hutokea wakati ambapo mwanamke huyu anaona tabia ambazo uko nazo sahizi ni tofauti na zile ambazo ulikuwa nazo awali, ama hakutarajia kukuona venye umebadilika.

Somo la leo tutakufundisha jinsi ya kurudisha interest ya huyu mwanamke na aanze kukupenda kwa mara nyingine.

Zama nasi!

#1 Tafuta chanzo kilichosababisha mambo kuharibika.

Jambo la kufanya kwanza ni kutambua mambo ambayo yalifanya hadi mwanamke huyu kuchoka na wewe. Inaweza kuwa labda mapenzi yako kwake yalikuwa yakupindukia akashindwa ama labda hakupendezwa na mwenendo ama approach yako kwake.

#2 Mpe nafasi.

Ameamua kukutenga. Hii ni kwa sababu amekuona huna manufaa kwake. So wewe pia lazima uheshimu maamuzi yake. So mpe nafasi yake akae kivyake. Hata ni bora zaidi kuhakikisha unampuuza kwa miezi kadhaa. Hii ni muhimu kwa kuwa ataona umeheshimu maamuzi yake ya kutaka kukutenga.

#3 Mpendeze kwa mbali.

Jeuka na uwe mwanaume bora. Mwonyeshe kuwa kukosekana kwake hakujakuathiri na chochote. Usionyeshe kama unasumbuliwa na misongo ya mawazo ama kutatizika maishani. Nyinyi si wapenzi so hakuna mahusiano yeyote kati yenu. Ukionyesha dalili ya kuwa unammiss basi atakuona wewe ni dhaifu. So unachotakiwa kufanya ni uishi maisha yako ya furaha. Si muda mrefu utaona akitafuta atenshen yako.

#4 Mwonyeshe kuwa una interest na yeye lakini kifioa.

Mwanamke huyu anajua kuwa unampenda sana. Hii ndio sababu anakuwa na confidence ya hali ya juu anapokuwa na wewe. Anaweza kuwa anakupenda pia lakini kwa kuwa anataka kukutumia ujumbe, ameachana na wewe. So wewe jifanye kana kwamba hauko interested na yeye kamwe. So mwangalie kwa dakika, na pindi anapokuona ukimwangalia tu, wewe angalia kando. Mbinu hii unapaswa kuitumia kifioa ili asiweze kudhania unafanya hivyo kimaksudi. Hii itamuacha na maswali ya kufikiria iwapo bado uko interested na yeye ama unapotezea tu. [Soma: Sanaa ya kutumia macho kumtongoza mwanamke]

#5 Jipende na jipe raha mwenyewe.

Usiwahi kumwambia mtoke deti baada ya yeye kukuonyesha madharau ya kukukataa. Usimwandikie jumbe za mahaba ama za kumuomba penzi lake. Usimuombe msamaha. Hakikisha hautangamani na yeye. Na kama itatokea kuwa anataka muongee basi ongea naye kama rafiki wa kawaida na wala usiongee kwa muda mrefu.

#6 Usimwonyeshe upendo.

Zile nyakati ambazo ulikuwa ukimbembeleza zinapaswa kuisha. Si alikutenga? Nawe mtenge. Mfanye aanze kuzitamani zile jumbe za usiku wa kiza ambazo ulikuwa ukimtumia mara kwa mara. Lengo lako kuu hapa ni kumuonyesha kuwa unaishi maisha yako ya kawaida ili umfanye ajutie uamuzi aliouchukua dhidi yako.

#7 Mfanye akumiss na kukutaka.

Mwishowe nyinyi wawili mtajeuka kuwa marafiki wa kawaida tu. Lakini jaribu kuhepa kuspend muda mwingi na yeye. Kama unakuwa na maongezi ya kuvutia na yeye unajiondoa na kumwambia kuwa uko busy na mambo mengine muhimu. Ataweza kuongea na wewe vile anavyotaka ilimradi tu akubali kukupenda kama vile zamani. [Soma: Mbinu za kumfanya mwanamke akumiss]

#8 Mfanye ashikwe na wivu.

Usiifanye ionekane wazi wazi. Anza kusuka na kutongoza wanawake wengine na uwapatie atenshen zaidi. Hapa bila shaka hata kama atajizuia kutoshikwa na wivu, ataudhika na wewe kwa kuwa unampuuza. Ukimwona anatongoza wanaume wengine usitishike. Hio  ni njia yake ya kukufanya uudhike. [Soma: Jinsi ya kumfanya mwanamke ashikwe na wivu]

#9 Anajiandaa kwako?

Je, baada ya haya yote unamshika akikuangalia? Ama ameanza kuonyesha interest kwako? Huwezi kuchukua hatua yeyote kabla kuhakikisha kuwa amekuwa interested na wewe. Ukifanya kosa la kuanza kumuapproach mara ya pili bila kujua kama amekuwa interested na wewe unaweza kuharibu kila kitu. [Soma: Jinsi ya kutambua kama mwanamke amevutiwa na wewe]

#10 Mwambie mtoke out tena.

Kama ushapata uhakikisho wa kuwa ameanza kukupenda kwa mara ya pili basi unaweza kuchukua hatua ya kujiandaa kuanza kuspend time zaidi na yeye. Usimzimie taa tena. Mwonyeshe upendo wako wote. Ukipata nafasi nzuri na yeye unaweza tena kumwomba mtoke out pamoja.

Tumeelewana? Kama unataka njia rahisi ya kuhakikisha ya kuwa unataka mwanamke arudiane na wewe kwa mara ya pili ama unataka kuiteka atenshen yake wakati ambapo umetatizika ulipokuwa unamtongoza basi hii ndio njia rahisi ya kumuwini.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.