Jinsi Ya Kuongea Na Mwanaume Na Umfanye Apendezwe Nawe


Tuanze. Je wajua jinsi ya kumfanya mwanaume apendezwe nawe? Wanawake wengi wanakuwa na maswali mengi ya kutaka kujua mambo ya kumwambia mwanaume wakati wanapokuwa wanaongea.


Kujua jinsi ya kuongea na mwanaume kunaweza kukutofautisha kati ya mwanamke anayeweza kuvutia attention na yule ambaye anaudhi wakati anapoongea na mwanaume.

Pia unapaswa kufahamu ya kuwa kufanya mwanaume apendezwe na wewe kunahitaji mambo mawili. Kwanza lazima ujue jinsi ya kuongea na pili lazima ujue jinsi ya kumfanya attention yake ije kwako.

jinsi ya kuongea na mwanaume.


Wakati ambapo utakuwa unazungumza na mwanaume, hakikisha unafuata mwongozo ambao tumekupatia na bila shaka utafaulu kuiteka atenshen yake na pia utaweza kumfanya apendezwe na wewe.

#1 Tabasamu mara kwa mara.

Next time ukiwa unaongea na mwanaume unayempenda, hakikisha unatabasamu zaidi. Cheka anapotoa mizaha yake, tabasamu mara kwa mara bila sababu ya maana na ulete hio nishati kwa macho yako. Hapa hakuna mwanaume yeyote ambaye anaweza kuistahimili jazba iliyoko ndani yako.

#2 Onyesha madoido.

Hii ni mbinu ambayo imekuwa ikitumika kwa maelfu ya miaka iliyopita. Na hadi wa leo inafanya kazi. Kuonyesha madoido ni tofauti na kuonyesha aibu kwa mwanamke. Na wanaume hupenda kuwaona wanawake ambao hupenda kuonyesha madoido. Wakati ambapo unaongea na mwanaume huyu, hakikisha ya kuwa unacheza na nywele zako, yazungushe macho yako wakati unapojaribu kupinga fikra zake, uma kucha, na kadhalika. Madoido huja automatic kwa mwanamke. Hivyo ni silaha nzuri ambayo unapaswa kuitumia wakati wowote ule.

#3 Mshike.

Wanaume wamejulikana kuwa huvutiwa zaidi pale ambapo wanapoguswa na wanawake. Pia utafiti umethibitisha swala hili kwa kudai kuwa wanaume huonyesha tabia za kutaka kuwatongoza wanawake pindi wanapoguswa wakati mazungumzo yanapoendelea.

So ile hatua ambayo unapaswa kuifuata ni kuhakikisha kuwa mara kwa mara unamgusa mkono, kuweka mkono wako kwa bega lake, ama sehemu nyingine yoyote ile ambayo haitaleta picha mbaya. Ukifanya hivyo utaona akionyesha interest zake kwako.

#4 Tafuta ulinzi wake.

Wanaume wanajulikana kama viumbe walinzi mbele ya wanawake. Hivyo utahitajika kuifufua hio taswira ambayo imekuwa ikijulikana tangu enzi za zamani. Na kufanikisha hivi ni rahisi sana. Mfano wakati ambapo mnavuka barabara pamoja, ushikilie mkono wake. Mshike kwa nguvu wakati utaona mbwa mkubwa akipita kando yenu, tabasamu halafu umwambie akushikilie mzigo mzito kwa dakika nk. Hizi ni baadhi ya mifano ambayo unaweza  kuitumia ikiwa lengo kuu ni kumfanya ajihisi kuwa yeye ndie mlinzi wako.

#5 Usitumie lugha chafu.

Wanawake wanatambulika kuwa wanapenda kusengenya na kutumia lugha za matusi wakiwa kikundini wakiongea. Well, ukiwa na huyu mwanaume hakikisha ya kuwa unatumia lugha ya heshima na pia unaacha kuongea kuhusu watu wengine. Wewe unachohitajika kufanya ni kumakinika na kusikiliza kile ambacho atakuwa anaongea.

#6 Usiwe mtu wa kutabirika.

Wanaume huwa wanachoshwa na wanawake ambao hawaeleweki. Lakini pia wanawake aina hii ndio wanawakula vichwa wanaume. Wanaweza kuzunguka kila mahali wakitaka kupewa majibu kuhusiana na wanawake hawa. So kwa upande wako, hakikisha kuwa mwanaume hapati kukuelewa kirahisi. Yaani asiweze kuisoma akili yake kwa vyovyote vile. La sivyo atakuona unaboesha.

#7 Kuwa mtundu.

Utundu ni jambo ambalo unapaswa kufanya mara moja au nyingine. Unaweza kumtesa, kumtatiza, kutoa mizaha kidogo ama kuyafanya yote. Wanaume hupenda wanawake wazuri, watulivu na wa amani. Lakini mambo hayo yanaweza kuboa baada ya muda flani so pia unahitajika kuonyesha ule upande wako mwingine.

#8 Kuwa na heshima.

Hii ni moja wapo ya tabia ya mwanamke ambayo kila mwanaume anatamani. Hivyo kama unataka kuongea na mwanaume ambaye unataka avutiwe na wewe, lazima uonyeshe heshima kwake. Lazima uwe unamakinika na maswali na majibu ambayo utakuwa unamwambia. Unaweza kufeki ama kujiteteza wakati ukiwa na yeye lakini pia ni vigumu na inahitaji ustadi wa hali ya juu. So badala yake hakikisha ya kuwa heshima yako inakuwa ya ukweli.

#9 Cheza mchezo usio rahisi.

Kama unataka mwanaume huyu avutiwe na wewe unahitajika kuwa mgumu. Usiwe mtu rahisi ambaye anaweza kukufanya vile anavyotaka yeye. Ongea na mwanaume kwa njia ya ukarimu lakini usimruhusu akuchukulie hivi hivi. Pia usiwe unapatikana kirahisi. Mtese kadri utakavyoweza. Afterall wanaume hawachoki kutafuta!

Upo!? Hizi ndizo mbinu ambazo unahitajika kufuata iwapo unataka mwanaume aweze kuvutiwa na wewe kirahisi. Tegea hapa hapa Nesi Mapenzi kwani kuna mengi ambayo yanakuja.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.