Jinsi Ya Kujichukua Baada Ya Mwanamke Kukukataa


Hali kama hii hutokea mara kwa mara kwa kila mwanaume. Hakuna mwanaume anaweza kusema kuwa hajawahi kukataliwa na mwanamke. Na iwapo kuna mtu anasema kuwa hajakataliwa na mwanamke, basi huyo ni mwanaume zege anayeogopa kutongoza wanawake kadhaa.
Tukirudi kwa mada, ni kuwa umekuwa ukimfukizia huyu mwanamke kila siku. Umetumia mbinu zote za kijanja tulizokupatia. Umejaribu kama mwanaume alpha lakini mwisho wa siku mwanamke huyu amekuambia, "Mimi siwezi toka na mwanaume kama wewe"


So utafanyaje?

Kama tulivyotangulia kusema awali ni kuwa hili ni jambo la kawaida kutokea kwa kila mwanaume. Pia hapa Nesi Mapenzi ni jambo la kawaida kwa paneli yetu kukumbana na jambo hili. So kukabiliana na hali kama hii tumekuandalia mambo kadhaa ambayo utahitaji kuzingatia ili uweze kunusurika usije ukajipata katika hali ya misongo ya mawazo.

#1 Si kila mtu atakupenda.

Jambo la kwanza unapaswa kufahamu ni kuwa si kila mtu katika ulimwengu huu atatamani kuwa na wewe. Ukishaliweka hili katika akili yako, basi hili jambo la kukataliwa linakuwa rahisi kwako. Najua inakuwa vigumu ukiwa unampenda fulani lakini pia unapaswa kujua kuwa ni jambo ambalo huwezi kulizuia. Itakubidi uvumilie hadi umpate yule ambaye atakupenda asilimia mia. [Soma: Mwongozo wa kutafuta mwanamke]

#2 Kuwa mtulivu.

Utakuwa umeudhika baada ya kukataliwa. Kama vile yeyote yule aliyekataliwa, la kwanza kufanyika ni kuwa atahisi uchungu, halafu kufuatiliwa na kukasirika. Lakini haya mambo yasikutatize. Huu ni mchakato mzima ambao huanza kwa hatua moja hadi nyingine. So ukiona kuna mabadiliko katika hisia zako, unapaswa kuwa mtulivu na wala hupaswi kukurupukwa ukafanya mambo ambayo yanaweza kukuletea shida.

#3 Usiichukulie binafsi.

Kila hatua umekuwa umeichukua kwa huyu mwanamke halafu akakukataa. Atakuwa amekukataa na sababu zake binafsi. Labda alikuwa hakujui, ama hujampendeza na approach yako. So lakufanya usiichukulie swala hili kuwa zito ukaanza kujiona hufai. La, naamini kama ungebahatika kumpata mwanamke ambaye analingana na wewe wakati huo basi ingekuwa rahisi kwako kuweza kumpata huyo mwanamke.

#4 Fahamu kuwa wanawake ni tofauti.

Wanawake wote si sawa. Unaweza ukatumia approach moja kwa mwanamke akakutaa, halafu ukaitumia approach hio hio kwa mwingine na akakukubali. So ukiona mwanamke wa kwanza amekukataa, hio haimaanishi kuwa kila mwanamke atakukataa. [Soma: Aina tofauti tofauti ya wanawake ambao hawakufai]

#5 Rudi nyuma ufikirie jambo ulilofanya.

Njia moja wapo nzuri ya kufanikiwa kwa wanawake ni kujua makosa ambayo umeyafanya awali. Ukiwa mtu ambaye unarudi nyuma kuangalia makosa ambayo umefanya basi itakuwa rahisi kwako kuweza kufanikiwa mbeleni. Pia utagundua makosa uliyoyafanya na badala ya kuwa na huzuni ya kukataliwa, unarudi kufanya mazoezi ili uwe bora zaidi.

#6 Weka umimi kando.

Usiruhusu umimi ukuingie kichwani. Kama umekataliwa na huyu mwanamke kubali tu na uendelee na maísha yako. Lakini ukianza kumtukana mwanamke kwa kuwa amekuacha, then mwisho itakuja na kukuathiri mwenyewe. Weka hisia hasi kando na ukubali matokeo. Hii itakupa fursa ya kupoza kidonda ambacho bado ni kibichi.

#7 Nenda zako.

Baada ya kukataliwa na huyu mwanamke, usipoteze muda wako ukingojea madakika. Unapaswa ujue ishara ambazo zinaonyesha kuwa uko karibu kukataliwa na mwanamke.

So ukigundua kuwa mwanamke huyu atakukataa baada ya dakika mbili zinazokuja, wewe hupaswi kungojea hadi akwambie kuwa hakutaki. La kufanya ni kujitoa na mapema ili ubadilishe mchezo uueke kwake. [Soma: Mbinu ya mjeuko ya kumfanya mwanamke akufukuzie]

#8 Usitumie maneno machafu.

Hili tayari tuligusia katika hoja ya 6. Mwanaume wa kawaida anafaa kuwa gentleman, hivyo akikataliwa asione kuwa ni ishu kubwa. Wanawake ní wengi sana. So tabia ya kumtukana mwanamke akikukataa ni ishara ya kutojiamini na uoga. Tabia hizi tuwaachie wenyewe.

#9 Usimuombe.

Hakuna kitu kinachosikitisha zaidi kama kumuona mwanaume akiomba penzi. Unapata mwanaume anampigia magoti mwanamke akimuomba asimuache. Hata kama ni mrembo kiasi gani, hupaswi kumuomba. Pindi mwanamke akiona kuwa yeye yuko juu yako basi anaweza kukufanyia chochote kile anachotaka ilimradhi akudharau. Hivyo epuka tabia hii.

#10 Usidhanie kuwa kila mwanamke yuko hivyo.

Kwa wale ambao ndio wameingia katika sekta ya kutongoza, unapaswa kufahamu ya kuwa si kila mwanamke atakukataa. Huyu ambaye umekutana naye mara ya kwanza na akakukataa, basi yule mwingine atakuwa tofauti na huyu wa kwanza. Kiufupi ni kuwa unapaswa kuelewa kuwa wanawake ni tofauti na tabia zao hazifanani.

Kumalizia ni kuwa kama umekataliwa ama unaogopa kukataliwa, lazima uelewe kuwa wanawake ni wengi. Unahitaji ukataliwe mara kwa mara hadi umpate yule ambaye atakukubali. Ni kama vile tu kutafuta kazi. Unaweza ukatuma makaratasi yako ukaitwa katika mahojiano na ukakataliwa mara kadhaa hadi mwishowe ukakubaliwa kirahisi. So usikate tamaa kamwe.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.