Mwongozo Wa Nesi Mapenzi Kuchagua Mwanamke


Wanaume wengi wanataka kujua kufanikiwa jinsi ya kuchagua wanawake. Ingawaje kuna baadhi ya wanaume wanaojua mchezo huu, wengi bado wamefunikwa na wingu jeusi la kutojua kuchagua wanawake, wanapojaribu kuapproach wanawake wanashindwa kiasi cha kuwa inabidi kuonekana kama wajinga wakati wanapokuwa wanachukua approach ya kwanza.

mwongozo wa kuchukua kuaproach mwanamke

Ok, ukweli ni kuwa hakuna kitu cha shangwe ama cha kuvutia kama kuapproach mwanamke.

Kuna wale ambao watapinga maoni haya kwa kudai kuwa approach kwa mwanamke kwa mara ya kwanza ni mfano wa kujaribu kuoga kwa maji ya barafu. Kama haya ndio maoni yako, hii post nimeiandika spesheli kwako. Nimeandaa mwongozo ambao lazima uutumie ili uondoe woga wa kuapproach mwanamke asilani.

Zama nami!

1. Maandalizi ndio ufunguo wa kila kitu
Wanawake warembo wako kila mahali - fahamu hilo. Hii inamaanisha ya kuwa katika ziara zako mahali popote pale, labda umeenda kununua bidaa supermarket, uko kituo cha mabasi, unafanya mazoezi, unakimbia, benki, ama sehemu yeyote ile ambayo unaijua wewe utawaona.

Amini usiamini, kuchagua na kuapproach mwanamke huwa kuna mafanikio ya juu wakati ambapo hautarajii. Hii ni kwa sababu pia mwanamke hatarajii jambo kama hilo. Hivi basi mahali popote utakapotembea hakikisha umejihami na angalia maneno mawili matatu ambayo mwishowe yatakufanya wewe utoke na kubadilishana namba ya simu ambayo mwishowe itazalisha deti. [Soma: Saikolojia kumfanya mwanamke akupende daima]

Hapa NesiMapenzi.com lengo letu kuu ni kukuhami wewe na zana zote ambazo unafaa kutumia kuhakikisha ya kuwa unaweza kuzitatua changamoto zote ambazo zinaweza kujitokeza wakati unaendelea na azma yako.

2. Michongo haina manufaa
Ijapokuwa ni muhimu kwako wakati wote uwe umejitayarisha, hii haimaanishi ya kuwa lazima kila wakati uwe umejiandaa kwa kuhifadhi baadhi ya michongo ulionayo. Ok sikatai ya kuwa kutumia michongo kuna asilimia 99 ya kuteka atenshen ya mwanamke (soma aina ya michongo hapa), lakini ninachomaanisha ni kuwa kutegemea sana matumizi ya michongo lazima ujitayarishe kusonywa na kuzungushiwa macho na wanawake ambao utawaaproach.

Kama utachagua kuhepa kuchekwa na kukataliwa na wanawake wakati unapowaomba utoke out nao, basi usitumie michongo na badala yake anza gumzo la kawaida ambalo linaweza kuwavutia. Kama ataingiliana na mtego wako na kuanza kuongea na wewe, sikiliza kila kitu ambacho ataongea nawe.

Kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia machapisho ya NesiMapenzi ya awali wanajua hatua za kufuata ikifikia sehemu ambapo umeshateka atenshen ya mwanamke.

3. Heshima ni muhimu
Wakati ambapo umechagua mwanamke, heshima ni jambo la muhimu la kufanya.

Kwa kuwa humjui wala kumfahamu huyu mwanamke, unachotaka kufanya ni kuhakikisha ya kuwa unatumia lugha ya heshima na kuhakikisha ya kuwa maneno utakayogusia hayataleta maudhi wala kumchosha. Kama unaweza kufanya hivi, basi tumia mbinu ya kumkeep buzy kwa kumletea mada ambazo zinavutia na kuchekesha. Ukifanikiwa kufanya hivi, fahamu ya kuwa siku yako itaisha ukiwa na furaha.

4. Epuka na lugha ya uongo
Ukishachagua mwanamke, hakikisha ya kuwa unaepukana na matumizi ya kutumia uongo kumvutia.

Makosa makubwa ambayo wanaume wengi wanafanya ni kutumia lugha ya uongo wakati wanapomtongoza mwanamke. Hii inafikia mahali flani unashindwa kufahamu kwa nini kila unapotongoza mwanamke unaachwa kwa mataa. Jambo la kufanya hapa ni uhakikishe ya kuwa unaongea ukweli kwa kuweka wazi madhumuni yako. Mfano iwapo hauko tayari kwa mahusiano marefu na mwanamke na upo tu kwake kujienjoy basi weka wazi. Kumshawishi mwanamke hakuendani sawia na udanganyifu, kiufupi usimwambie unataka kulala na yeye na bila chochote cha zaidi.

Hakikisha ya kuwa nia yako kwake haitamdhalilisha kwa njia yeyote ile.

5. Angalia mwonekano wako
Ingawaje mwonekano unaweza kuonekana ni wakujitweka, ni muhimu kwa kuwa kutachangia pakubwa kuteka moyo wa mwanamke.

Afterall, mwonekano wako ni kama kioo kinachomulika ndani ya mwili wako, hivyo ni muhimu kuhakikisha ya kuwa unajiweka nadhifu na vile utakavyovalia kutaleta shangwe kwa mwanamke.

6. Kutemwa ni hatua ya kawaida katika huu mchezo
Hata kama umesoma na kuhifadhi machapisho yote katika NesiMapenzi.com, kukataliwa na mwanamke mara moja au nyingine ni jambo ambalo kila mwanaume hupitia maishani mwake.

Sehemu ngumu ya kukataliwa ni kukubali kuwa umeshindwa na kuchukua hatua nyingine tofauti ya maisha bila kuingiwa na hisia za kuona aibu ya kuapproach tena.

Hata kama utakataliwa na wanawake mara ngapi, kila wakati unapokataliwa lifanye kama funzo kwako. Usikate tamaa kwani hatua za kuapproach mwanamke kuna asilimia 50 ya kukubaliwa na 50 ya kukataliwa.

Jifunze kukutana na wanawake mara kwa mara kwani utakuwa ukijipatia funzo ambalo utalishika na kutorudia makosa ya awali. [Soma: Jifunze jinsi ya kukutana na wanawake wapya]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.