Aina 12 Ya Wanawake Ambao Hawakufai


Kila mtu hapa ulimwenguni ameumbwa na sifa aina yake. Kuna wengine wameumbwa na tabia za kuridhisha na wengine wameumbwa na tabia ambazo haziridhishi. Hii pia inajitokeza katika wanawake. Katika mahusiano, utapata kuwa wanawake wanakuwa na tabia ambazo aidha zinawapendeza wanaume wao ama zinawachukiza.


Katika kuangalia tabia za wanawake, tumekuja na orodha ya wanawake ambao kama mwanaume unafaa kuwa chonjo nao kwani watayafanya maisha yako ya mahusiano kuwa ya balaa. Labda sahizi uko katika mahusiano ya muda mrefu na mpenzi wako ama sahizi uko mbioni unatafuta, kuwa macho na aina hii ya wanawake ambao wanaweza kukuharibia ama kukuletea shida
katika mahusiano yako nao mbeleni.

#1 Mwanamke anayekuganda nguoni.
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye amekupenda kiasi cha kuwa hawezi kufanya jambo lolote bila kukuhusisha. Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye amekuwa amezama kwa penzi lako kiasi cha kuwa hakupi nafasi ya kupumua. Kila kitu atakachofanya lazima uwe karibu yake.

Well, hii ni poa kwa mahusiano lakini itafikia mahali ambapo utachoshwa na tabia zake haraka. Na pia yeye kama mwanamke atakuwa na mawazo finyu kwani kila wakati anapokumbwa na jambo fulani hataweza kulitatua bila kukuhusisha. [Soma: Mambo za kuzingatia ili upate mpenzi wako wa dhati]

#2 Mwanamke aliyepagawa kimapenzi.
Nani hapendi mwanamke anayempenda kupindukia? Kila mtu angekuwa na mwanamke aina hii wanaume wangekuwa na furaha milele. Lakini kulingana na utafiti ni kuwa aina hii ya mwanamke ni miongoni mwa wanawake wabaya kabisa ambao wanaweza kufanya maisha yako kuwa ya taabu.

Mwanamke kama huyu utampenda siku za kwanza kwanza lakini tatizo ni kuwa kadri siku zitakavyopita mnapokuwa pamoja utagundua tatizo flani, mwanamke aina hii hangependa ufanye chochote bila yeye kuwa karibu yako. Hii ina maana kila mahali unapoenda lazima akuandame. Aidha ukiwa na marafiki zako, vilabuni, uwanjani...nk, yaani kiufupi kila uendapo anataka awe hapo hapo ili akuangalie na akupende zaidi. Utamweza kweli huyu?

#3 Mtumiaji.
Kuna aina ya wanawake ambao wanakuona wewe kama mwanaume mzuri ili wakutumie kama chambo kuwafanikisha kimaisha. Unaweza kuwa mwanaume ambaye una uunganishi na watu wengi, ama unaweza kuwa mwanaume ambaye unapendwa na wengi. Mwanamke aina hii ataona kuwa akiwa karibu na wewe itakuwa nafasi rahisi kwake kupata connection na marafiki zako kwa
urahisi. Hii inamaana kuwa pindi mwanamke aina hii akifanikiwa kupata kile ambacho amekuwa akitafuta, bila kupoteza wakati atakutema na kukuacha kwenye giza. [Soma: Ujanja wa kufanya uvutie wanawake haraka sana]

#4 Mwanamke asieomba msamaha.
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye hawezi kuomba msamaha kwa jambo lolote ambalo amefanya hata kama ni la makosa. Anaweza kuomba msamaha kwa shingo upande ama aamue kunyamaza kimya tu kwa jambo alilofanya la kukwaza ama kuudhi. Owk kwanza ni kuwa aina hii ya mwanamke anaogofya sana kwani mtu ambaye hakubali makosa yake si mtu mzuri wa kuishi naye hata mara moja.

#5 Mlalamishi.
Huyu ni aina ya mwanamke ambaye nyakati zote yeye hulalamikia kuhusu hili na lile. Yaani kwake hakuna jambo zuri ambalo limeshawahi kumfanyikia. Aidha atakuwa akilalamika kuhusu marafiki zake, maisha yake ya kila siku nk. Yeye siku zote hana amani. Aina hii ya mwanamke haifai kabisa kwani ulalamishi wake wa kila siku utakuchosha kwa haraka.

#6 Asiyejielewa.
Huyu ni mwanamke ambaye haelewi anachotaka maishani. Wakati wote yeye atakuwa anahangaika na uchaguzi wake na hajiamini na chochote ambacho anachagua. Aina hii ya mwanamke achana nayo kwa sababu wewe pia inamaana hayuko asilimia mia moja kama aendelee kuwa nawe au la. Aina hii ya mwanamke mara nyingi huwa na wanaume wengi na ni rahisi kwake kukuendea kinyume kimapenzi. So kama wewe una mahusiano na mwanamke aina hii aidha uachane naye fasta ama akuache wewe wa kwanza. [Soma: Jinsi ya kutongoza kwa wale wanaoanza]

#7 Anayetawala na kutotosheka.
Hii ni aina ya mwanamke ambaye anatarajia makuu kila wakati na hatosheki kile alicho nacho. Anapenda kutawala na kila kitu anataka kifanywe vile ambavyo anavyotaka yeye. Owk najua wanawake wanapenda wanaume ambao ni gentlemen, lakini baada ya muda mfupi utakuja kugundua kwamba aina hii ya mwanamke watakufanya bwege, yaani watakukalia kichwani na wao kujifanya mabosi.

#8 Mwenye maoni ya ukashifu wakati wote.
Kuwa na maoni na kukashifu si jambo baya kwani kukosoa mambo katika mahusiano ni jambo zuri katika maisha. Lakini usizidishe. Aina hii ya wanawake wanaokashifu kupita kiasi ni wale ambao wakisema jambo fulani basi litabakia hilo hilo na hata ufanyeje hawawezi kujeuza. Aina hii ya wanawake watafanya maisha yako kuwa balaa.

#9 Nusa Nusa.
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye haipiti siku bila kukuchunguza. Kila wakati anapopata mwanya anajaribu kukuchunguza mienendo yako. Unaweza kuwa mwaminifu kwake lakini yeye bila kutosheka lazima akuchunguze chunguze, mara aangalie simu yako, atake kujua umetoka wapi umeenda wapi, jana ulivaa nguo gani, anawauliza maswali marafiki zako kukuhusu nk. Aina hii ya mwanamke muogope sana kwani pia yeye haaminiki. Kila anachofanya yeye anashuku pia wewe utafanya. Hivyo mara nyingi ukiona mwanamke anashindwa kukuamini kwa uhusiano, inamaanisha kuwa pia yeye ana hilo tatizo, so ukiona mwanamke wako ana hizo tabia achana naye mara moja.

#10 Asiye na maono.
Aina hii ya mwanamke inafanana karibu na ile ya asiyejielewa lakini hii ni kuwa mwanamke aina hii hana maono kujihusu yeye mwenyewe. Ukimuuliza kitu chochote anakwambia kuwa hajui ama hana mtazamo wowote kuhusu jambo lolote. Mwanamke huyu anaweza kuonekana mwanamke mzuri mara ya kwanza kwa sababu hawezi kukupinga na chochote unachosema lakini pindi muda unaposongea utaona kuwa ataanza kuwa mzigo kwako. Aina hii ya mwanake iogope sana kwa sababu anaweza kuwa anafanya hivyo maksudi huku akiwe ameweka mtego ama malengo yake kibinafsi kutoka kwako. Mwanamke asiyetoa maoni kuhusu chochote unachosema ni umuogope sana. [Soma: Tabia zinazotofautisha kati ya wanaume wa kweli na wale wadhaifu]

#11 Mpenda vita.
Hii ni aina ya mwanamke ambaye huwa na hasira za haraka na akichukizwa na chochote kile ambacho kinakuja kwa akili yake. Aina hii ya mwanamke sitaigusia sababu kila mtu anajua matokeo yake.

#12 Mtoto wa mama.
Aina hii ya mwanamke ni yule ambaye hatofanya chochote bila kuingiza wazazi wake katika maongezi yake. Aina hii ya mwanamke ni mbaya kwa sababu hata ufanye nini lazima aingize wazazi wake ndani yake. Hii inamaanisha kuwa hawezi kuthamini maoni yako kabla kuwauliza wazazi wake.

Hii ni orodha ya baadhi ya tabia za wanawake ambazo mwanaume yeyote anafaa kuwa chonjo kwani mwishoni wanaweza kuleta taabu ambazo zitakuwa vigumu kutatua.


1 comment:

  1. nzuri wanawake sometym wanaboa uko wap, uko na nan. maswal gan haya

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.