Tabia Ambazo Zinamtofautisha Mwanaume Halisi Na Wanaume Wadhaifu


Mwanaume ambaye ni halisi kwa kawaida mambo yake yanakuwa rahisi maishani mwake. Mwanaume aina hii mara nyingi hupendwa na kila mtu, anakuwa rahisi kutambulika na jamii, akiongea mbele ya watu wanamsikiliza na pia hatatizwi na mambo ambayo watu wanaweza kuongea kumhusu.

Katika tasnia ya utongozaji, ni bora kila mwanaume kuwa mwanaume halisi. Mwanaume halisi si lazima awe mwanaume alpha ijapokuwa mwanaume alpha lazima awe mwanaume halisi. [Soma: Tabia za mwanaume alpha]


So labda ungetaka kujua iwapo una hulka ya mwanaume halisi au la. Hivyo leo tumekuja na tabia au sifa ambazo zinamtambulisha mwanaume kuwa mwanaume halisi.


Zama nasi…


Sifa za mwanaume halisi


#1 Anathamini wengine.

Sifa ya kwanza ya mwanaume halisi ni kuwa anathamini watu wengine. Vile ambayo anajithamini yeye ndivyo anavyothamini watu wengine. Anahakikisha kila mtu ambaye anatangamana naye anajiskia huru akiwa na yeye.


#2 Anawaheshimu wanawake.

Sifa nyingine ya mwanaume halisi ni kuwa anaheshimu wanawake. Kuheshimu wanawake ni swala pana ambalo linahushisha mambo kadha wakadha kama vile kuwaheshimu kitabia na kimaumbile.


#3 Anaongea kile ambacho ni cha haki.

Mwanaume halisi ni yule ambaye hafichi mambo kwa kuongea uongo. Mwanaume halisi huhakikisha ya kuwa anaongea yale ya ukweli bila kuogopa yeyote. Hakubali unyanyasaji ama dhulma kufanyika wakati anaangalia.


#4 Hurudi nyuma kama inahitajika.

Mambo mengine ambayo hufanyika hapa duniani hufikia kiwango ambacho mtu huweza kushindwa kuendelea kufuatilia. Hivyo mwanaume aina hii halazimishi mambo ambayo yanapita kiwango ambacho hawezi kukizuia. Mfano mwanaume halisi halazimishwi kupendwa na mwanamke ambaye hamtaki.


#5 Anaheshimu wakubwa wake.

Sifa za mwanaume halisi ni kuwa katika maisha yake anahakikisha ya kuwa anawaheshimu wakubwa zake. Hawezi kuwadharau wala kuongea mambo ambayo yatawakwaza.


#6 Yuko huru kupokea maoni kutoka kwa wengine.

Mwanaume halisi hawezi kukataa kuskiza maoni kutoka kwa watu wengine. Mwanaume aina hii yuko tayari kuskiza maoni ya wengine na hata anaweza kutumia maoni hayo kufanikisha ajenda ambazo anaweza kuwa nazo ili aweze kutimiza mambo yake. 


#7 Anakuwa na subra.

Mwanaume halisi anakuwa na subra ya kungojea mambo yafanyike bila ya kuharakisha. Mfano wakati anatongoza mwanamke, hawezi kuharakisha mwanamke ampende siku hio hio bali anachukua muda wake vizuri ili kuhakikisha kuwa mwisho wake utakuwa wa manufaa zaidi.


#8 Ni mwenye hekima.

Sifa nyingine ya mwanaume halisi ni kuwa anakuwa na hekima. Anajua kutofautisha kati ya baya na zuri, jema na ovu. Pia anakuwa na maamuzi ambayo hayatakinzana na upande wowote ule.


#9 Anajitambua.

Mwanaume halisi huwa anayatambua mazingira yake na pia anayatambua mazingira ambayo yanamzunguka. Hivyo hawezi kuingia na wasiwasi wa kutojiamini wakati wowote ule katika maisha yake.


#10 Anaeleza hisia zake.

Mwanaume halisi hafichi hisia zake. Akiwa na jambo ambalo linamsumbua moyoni mwake hawezi kuficha. Yuko tayari kueleza hisia zake bila woga. Akiwa anampenda mwanamke hawezi kuwa na woga wa kujieleza.


#11 Hadhalilishi wengine.

Mwanaume halisi hawezi kudhalilisha wengine. Hawezi kuleta utani ili kushusha hadhi ya wengine. Mwanaume halisi hayuko tayari kuidoresha sifa ya mtu mwingine kwa manufaa yake mwenyewe.

Upo!?


Ok. Hizi ni baadhi ya sifa zile muhimu ambazo zinaweza kumtofautisha mwanaume halisi na mwanaume dhaifu. Je, uko kitengo gani kati ya hawa watu wawili.




No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.