Mambo 6 Ambayo Mwanamke Hutamani Kutoka Kwa Mwanaume


Ushawahi kujiuliza ni mambo gani ambayo mwanamke angependa kutoka kwako? Labda umekuwa ukimvizia wiki nzima sasa au hata mwezi mzima lakini hupata mambo ambayo yanaweza kumpendeza?


Usitie shaka kwa kuwa wanawake huwa na tabia inayofanana kwa kila mmoja. Kuna mambo ambayo wanawake wote kwa umoja hupenda. Na uzuri ni kuwa pindi utakapofuata mambo hayo basi mwanamke yeyote ambaye umekuwa ukimwaproach ataanza kuvutiwa na wewe.

Haya hapo ni baadhi ambayo mwanamke hupenda kutoka kwa mwanaume yeyote yule:

#1 Kuwa gentleman ama mwanaume thabiti.
Wanawake siku hizi wamekuwa wa kisasa, lakini bado wangependa kuwa na mwanaume ambaye anawafungulia milango, wanawaletea zawadi mara kwa mara na kadhalika. Pia wanapenda mwanaume ambaye ni mkarimu na ambaye ni mpole. So kama wewe unatabia za ugentleman, basi una nafasi kubwa ya kumridhisha mwanamke yeyote. Na kama huna hizo tabia basi kazi ni kwako. [Soma: Jinsi ya kuwa na tabia za kijentleman]

#2 Kuwa mtu mwenye hisia na mambo yake.
Kama tulivyotangulia kueleza hapo juu ni kuwa mwanamke anapenda mtu mwenye tabia za kigentleman, so kama wataka kuyeyusha moyo wa mwanamke ni kuhakikisha kuwa unapenda kumfanyia saprize mara kwa mara huku ukimuonyesha ukarimu wako kwake. Hii itasaidia kumfurahisha na kutimiza ndoto zake. Kumfanya kuwa special ni dhahiri kuwa utamfanya akupende zaidi na zaidi.

#3 Kuwa na tabia za utu uzima.
Kulingana na utafiti ni kuwa wanawake wengi hupenda kudate na wanaume ambao ni wakubwa kuwaliko. So kama wewe unajiona unatabia za utu uzima na hauna mambo ya kifala basi bila shaka utatimiza ndoto yako na kuwa na yule umpendaye.

#4 Kujiamini.
Mwanaume ambaye anajiamini kuwa yeye ni yeye bila kujishuku ana nafasi kubwa ya kuteka hisia za mwanamke yeyote. Kujiamini hakumaanishi kutojali na mambo yeyote bali kujiamini kinafsia. Mwanaume anayejiamini anaweza kukabiliana na matatizo yeyote ambayo yanaweza kumkumba maishani mwake. So hio ni rahisi kwa mmoja kuiteka hisia ya mwanamke kiurahisi. [Soma: Mambo ya kufanya ili uongeze kujiamini kwako]

#5 Kuwa na uwezo wa kumshughulikia.
Wanawake wanafikiria maisha ya mbele, yaani maisha ya usoni mkiwa nyote wawili. So mwanaume ambaye anaonyesha dalili za kuwa anajielewa na ana uwezo wa kumtunza yeye kifedha maishani basi ana nafasi kubwa ya kumnasua mwanamke kiurahisi. Ujue kwamba hii haimaanishi kuwa lazima uwe tajiri kuweza kutimiza ndoto yako bali kile unachohitajika ni kumsaida kadri unavyoweza wewe na usipitishe kiwango ambacho kinaweza kukuathiri kisaikolojia.

#6 Uwe nadhifu.
Ingawa kuwa nadhifu haichangii sana kumfurahisha mwanamke kama ilivyo kwa wanaume, bado hii ni baadhi ya vitu ambavyo mwanamke angependa kuviona kwa mwanaume yeyote. So kufanya akupende lazima uhakikishe umetia bidii fulani katika sekta hio. [Soma: Sababu za kuwafanya masharobaro wapendwe na wanawake sana]

Sasa, hata kama kuna tabia flani hapa tulizozieleza ambazo hazifanani na wewe kabisa, haina haja ya kujistikia vibaya. Mradi una nia ya kujifundisha kuwa na tabia kama hizi ama unauhakika kuwa mbeleni utakuwa na tabia kama hizi, basi wewe una nafasi kubwa zaidi ya kukufanya kupendwa na wanawake ambao wako wengi wanatafuta wanaume ambao wanatabia kama hizi.


1 comment:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.