Kwa Nini Kila Mwanaume Anafaa Kuwa Na Tabia Za 'Alpha'


Neno 'alpha' si geni kwa wengi. Itakuwa ushawahi kuliskia mahali flani, kwa sinema ama kwa vitabu. Kwa lugha ya urahisi neno 'alpha' linamaanisha mwanzo ama wa kwanza. Pia linaweza kumaanisha mkubwa ama kiongozi wa kizazi fulani cha familia haswa katika wanyama.

Lakini hapa kwa blog ya NESIMAPENZI, ama katika nyanja ya mahusiano, neno alpha linatumika kuonyesha mwanaume ambaye yuko juu ya wanaume wengine kwa kila kitu, yaani ni mwanaume ambaye si wa kawaida na wanaume wengine haswa ikija maswala ya wanawake.


Wanaume aina hii huwa na uwezo wa kuchukua chochote ambacho wanajiskia nacho na wanaume wa kawaida huwaangalia bila kupinga.


Mfano ushawahi kumzimia mwanamke unayependa halafu ghafla akachukuliwa na mwanaume flani bila yeye hata kutoa jasho lolote? Inauma kweli kupatika katika situation kama hii.

Sasa waonaje uwe miongoni mwa wanaume ambao wanaitwa alpha? Habari njema ni kuwa kujeuka alpha si lazima uwe na kipawa chochote cha kuzaliwa nacho. Ukitia bidii na mkazo utafaulu kuwa mmoja wa alpha.

Hatua zifuatazo zitakufanya ujeuke mwanaume Alpha


1. Kujiamini -iige hadi ikuige

Mwanaume alpha ni mtu anayejiamini na huonyesha kupitia miondoko yake ya mwili. Anajiamini mahali popote kutoa maoni yake, bila kusitasita wala kubabaika. Najua umeshawi kuskia zaidi ya mara milioni moja kuwa kufanikiwa lazima uwe unajiamini. Na pia najua unazijua changamoto zinazotokana wakati unapojifunza kujiamini na kitu fulani. [Soma: Njia za kufanya ili uongeza kujiamini kwako]

Makinika na miondoko yako ya mwili. Wanaume wanaojiamini huwa wanaenda vizuri wakati wanapotoa mapozi yao. Usiingie sehemu flani haraka bila kujitambulisha ama kuongea na mtu. Tembea polepole na ukiwa kifua mbele, unapokaa hakikisha kuwa mikono yako umeipanua.

Mwanaume alpha anapokaa, huegemea nyuma, anaonekana mtulivu, na huchukua nafasi yote ile anayoitaka yeye. Huku marafiki zake wakichukua nafasi ndogo na kuingiwa na kibaridi, mwanaume alpha hana uoga wa kuangaliana ana kwa ana na yeyote yule. Usitoe kigugumizi wakati unapoongea. Ongea polepole na upange hoja zako kwa mpango nadhifu. Hakikisha unaongea kwa sauti ili yeyote yule apate kukuskia.

2. Jiheshimu -muhimu kati ya yote


Mwanaume alpha huwa anajiheshimu na maoni na vitu anavyoamini. Hababaikii kutaka kujua maoni ya wengine kumhusu ama kuhusu swala flani.  Hii inakuwa vigumu kwa yeyote kujaribu kuichezea akili yake. Tabia ya kuonyesha ubabe, na kumiliki himaya huwa kawaida kwake. Hawaingiwi na aibu kuhusu maswala tata yanayoibuka, kwa kawaida husimama na kujitetea. Tabia hii kawaida hufanya kazi kwa wanawake. Iwapo unaona ya kuwa mwanamke anajaribu kuichezea akili yako hapo hapo unaachana naye na unatafuta mwingine.

Mwanamke anayekubali kuingia katika himaya ya alpha lazima afuate masharti yake. Hatothubutu kubadilisha tabia ya mwanaume wakati wowote ule. Alpha anaishi na sheria zake bila kuskiliza za mwingine. Amini usimini wanawake hupenda tabia kama hizi kutoka kwa mwanaume.

3. Mbahili - jiweke mbele kwa kila kitu

Mwanaume alpha anajua ya kwamba yeye ndie wa kuchukua step ya kwanza wakati anapoapproach mwanamke. Ikija suala la kutimiza matamanio yake, haogopi kutemwa ama kufanya kazi. Kabla ya dunia kumuathiri, yeye ndiye anayeiathiri dunia. Haogopi kusimama na maoni yake.

Wanawake wanapenda wanaume ambao si waoga kuchukua uongozi wa swala fulani. Kuwa na maamuzi thabiti kunadhihirisha kuwa unajiamini. Wakati mwingine mnapotoka out usiwahi kumuuliza anataka kuenda wapi. Hakikisha tayari ushajipanga kitambo.[Soma: Maswali ya kumuuliza mwanamke kwa chat ambayo yatampagawisha]

4. Onyesha jinsia yako


Mwanaume alpha si muoga kuonyesha jinsia yake. Hahitaji kuambiwa kuwa amekubalika kuonyesha uume wake, hili ni swala ambalo kila mwanaume anafaa kujivunia nalo. Labda anaweza kumtomasa girlfriend wake ama kwa bahati mbaya kuupapasa mgongo wa mwanamke, hakuna maswali ya kuuliza kwa nini ameamua kufanya kitendo hicho.

Kuonyesha jinsia yako inaweza kuonekana jambo geni lakini ushawahi kujiuliza kwa nini John Travolta mpaka sasa anapendwa na wanawake na alioa tangu kitambo? Ukijifunza mara ya kwanza mwishowe utaona kama kawaida. Anza na kushika mikono, kiuno ama mgongo. Hakikisha usitumie nguvu ama kuonekana fisi. Ujanja ni kurelax na utumie mbinu ifaayo kumkeep mwanamke unayempenda kuwa buzy.

5. Fanya mazoezi binafsi kuikuza nafsi yako


Hauwezi kuamka kesho tayari ukajeuka kuwa mwanaume alpha. Lazima ufanye majaribio na muda mwingi wa kuipanga nafsi yako. Mwanaume alpha mara nyingi yeye huwa buzy na shughli zake hivyo ana muda mfupi sana wa kutangamana na wengine hivyo ni muhimu sana kuitumia dakika chache aliyo nayo.

Kitu kingine ufahamu kuwa usijitenge kuwa hauwezi kuwa alpha kwa kuwa unaopoga vile ulivyo, shepu yako na kadhalika. Rudia kusoma point ya kwanza ni kuwa mwanaume alpha anajiamini, hivyo wewe lazima ujiamini. Halafu fahamu ya kuwa kufanikiwa katika kumtongoza mwanamke kamwe hakuhusishwi na vile ulivyo bali vile ambavyo unajichukua.


Upo!? [Soma: Jinsi ya kumuaproach mwanamke mara ya kwanza]


1 comment:

  1. Howdy very ckol web site!! Man .. Beautiful .. Amazin ..
    I wikl bookmark yoiur site and take the feeds also? I aam satisfied to search out a lot of helpful information right here within the post, we
    want develop more teschniques in this regard,
    thanks for sharing. . . . . .

    ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.