Ishara 11 Kuonyesha Kuwa Ex Wako Hataki Kurudiana na Wewe Kamwe


Kuna wakati unaweza kukosana na mpenzi wako na mkaachana. Lakini baada ya kupitia hatua zile za huzuni za kuachwa,kuna wakati unatamani urudiane na mpenzi wako angalau kwa siku moja.

Hatua hii kila mtu hupitia na mara nyingi wengi huomba mbinu ama hatua za kufanya hadi kurudiana na mpenzi wake. [Soma: Hatua za kufanya urudiane na Ex wako]


Kuna baadhi hufaulu kurudiana na wapenzi wao lakini wengi huambulia patupu. Somo la leo hapa Nesi Mapenzi tumeamua kukuonyesha ishara ambazo zitakufanya utambue iwapo mpenzi wako amechoka na mahusiano yako na hataki kurudiana na wewe tena. Zama nasi.

#1 Anakuambia.
Unaweza usikubali kile ambacho anakwambia lakini mara nyingi mpenzi wako akisema amechoka na wewe basi anamaanisha ukweli. Anaweza kukusisitizia mara kwa mara ili uelewe. Ukiona kuwa hataki kusitisha msimamo wake basi fahamu hutafaulu.

#2 Hajibu meseji zako ama simu.
Mara za kwanza inaweza kueleweka kama hatajibu meseji zako. Lakini ukiona mtindo huu umeingia wiki hadi miezi basi msimamo wake wa kuwa hataki kurudiana na wewe uko pale pale.

#3 Amebadilisha namba ya simu.
Akiona ya kuwa mara kwa mara unamtatiza kwa kumtumia jumbe zisizoisha, basi hatua ambayo atachukua ni kubadilisha namba yake ya simu. Atafanya hivi ili kukatiza mawasiliano na wewe kabisa. [Soma: Sababu zinazokufanya umkumbuke Ex wako mara kwa mara]

#4 Amekuondoa kwa familia yake.
Wakati ulipokuwa na uhusiano wa kimapenzi pamoja mlikuwa mnaenda kuwatembelea wazazi wake ama kutangamana na marafiki zake. Lakini ukimwona kila ukijaribu kujileta kwao hataki uwasiliane na hata mmoja wa familia yake basi ni ishara ya kuwa hakuna matumaini ya kurudiana na yeye.

#5 Hataki kurudi nyuma na kuona makosa yaliyofanyika katika mahusiano yenu.
Mara nyingi wapenzi wawili wakikosana huwa kuna wakati hurudi nyuma na kuangalia makosa yaliyotokea. Lakini ukimwona mpenzi wako hajishughulishi wala hataki kujua chochote basi ni ishara ya kuwa ameamua kuendelea na maisha yake bila wewe.

#6 Anakwambia “Unahitaji mtu bora zaidi”
Tamko hili limetumika sana. Hii ni ishara anakupatia kukuambia kuwa hataweza kurudiana na wewe. Japo alikuwa na upendo mwema kwako lakini anajiona hatoshi. [Soma: Mfanye Ex wako atamani kurudiana na wewe]

#7 Amekurudishia vitu vyako.
Labda ulikuwa umeacha vitu kwa nyumba yake ili uweze kutumia kwa urahisi ukiwa kwake. Inaweza kuwa nguo, mafuta, marashi na kadhalika. Vitu hivi akikurudishia ni ishara ya kuonyesha kuwa hakuna matumaini ya kuwa kunaweza kuwa na uwezo wa nyinyi wawili kurudiana. Kumbukumbu zako kwake zinahusishwa na vitu hivyo.

#8 Anadeti na mwingine.
Kama Ex wako bado anakupenda basi hataharakisha mambo. Na wala hataanza kurusha picha za mpenzi mwingine kwa mitandao yake ya kijamii. Lakini ukiona ameanza kupost picha akiwa na mwingine basi fahamu wewe na yeye mambo yenu yamekwisha.

#9 Anajaribu kuhepa kukuona.
Anajua sehemu ambazo unakunywa kahawa na kujivinjari. Na mara kwa mara mumekuwa mkikutana katika sehemu hizo. Lakini ukiona Ex wako haonekani katika sehemu hizo basi ni ishara ya kuwa hataki mambo yako tena.

#10 Akikuona hana furaha.
Well, kwa mfano umekutana naye kwa ghafla na unamwona hana raha, si mchangamvu na anakaa kuchoka. Hii ni ishara ya kuwa hautaki uwepo wako na anajaribu mbinu zote kukutenga.

#11 Hataki kujua kama unadeti mwingine au la.
Mbinu hii hutumika kumfanya aone wivu la labda kutamfanya aanze kuzungumza na wewe kwa mara nyingine. Lakini akigundua unadeti mwingine na hashtushwi na chochote basi ni ishara ya kukuambia hana haja na wewe.

Najua ni vigumu kuamini kuwa mpenzi wako amekutoka. Labda ulipanga mengi na yeye na ulitamani muyatimize pamoja maishani. Lakini ukweli ndio huo. Ukiona Ex wako anaonyesha ishara hizi basi haina budi kukubali ya kuwa umekuwa single kwa mara nyingine! [Soma: Mitandao ya kutafuta wachumba kwa wale wako single]

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.