Jinsi Ya Kumfanya Mpenzi Wako Wa Zamani (Ex) Atamani Kurudiana Nawe -Ujanja 8 Wa Kisaikolojia


Kumfanya mpenzi wako wa zamani kurudiana na wewe si jambo la rahisi kutimiza, haswa kama iwapo ameshachukua hatua ya kusahau yaliyopita na kupata mchumba mpya ambaye wanadate.

jinsi ya kumvutia mpenzi wako wa zamani arudiane nawe

Wakati mwingine, inafaa ujipende wewe mwenyewe zaidi ili kufanya mtu mwingine naye akupende. Inafaa uwashe kitu fulani ndani yako; ili kufungua nishati ambayo inapatikana ndani ya mwili wako ili uweze kuwa mtu tofauti.

Wakati mwingine kama tumevunjwa moyo na kukata tamaa tunasahau kujipenda sisi wenyewe. Dunia yako haifai kuzunguka kwa mtu mmoja pekee. Kumbuka marafiki zako wapya na wa zamani sababu hao wanaweza kukusaidia.

Kuwa jasiri kufanya mambo ambayo hujawahi kufanya mbeleni. Kufanya hivyo kutakupa wewe nafasi ya rahisi kumpata na kurudiana na mpenzi wako wa zamani. Jaribu kuvumbua upande mwingine wa nafsi yako, na ukigundua kuwa unaweza kufanya mambo kama hayo, unaweza kujiamini kufuata maagizo haya ya kutumia saikolojia ili uweze kumfanya mpenzi wako atake kurudiana na wewe. [Soma: Hatua za kufanya ili mwanaume akupende]

1. Tumia saikolojia mjeuko

Mfano
Mpenzi wako wa zamani Ex ameamua kuachana na mambo yenu ya zamani. Hajibu texts zako wala hataki kupokea simu zako.

Kitu cha kufanya
Bila shaka itakuwa wamezoea ya kuwa kila wakati unamfukuzia ama kutaka kujihusisha na kumbabaikia. Lile ambalo utahitaji kufanya ni usijisumbue kuwatext wala kuwapigia simu.

Kama itatokea mkipishana hata usijisumbue kumuangalia machoni. Akikusalimia mambo wewe mjibu tu poa. Hivi hivi unafaa kuwafanyia marafiki zake. Hakikisha ya kuwa unawafanya kana kwamba huwatambui kabisa katika maisha yako. Wewe jifanye mtu wa kawaida kabisa.

Ukifanya hivyo wataanza kushangaa kwa nini umeanza kuwapuuza kwa ughafla. Wataanza kujiuliza kwa nini umeacha kuwatumia jumbe fupi ama kukuona kwa nini siku hizi umeacha kuwa mtu wa kujamiiana. Mwishowe itafikia wataanza kuuliza marafiki wengine kutaka kujua kama umepata mchumba mwingine ama umeanza kudate mtu mwingine.

Owk. Kama unafanya haya yote kumbuka usivuke mipaka. Wakikusalimia jibu salamu zao lakini usiwe wewe wa kwanza kutoa salamu. Muda si mrefu watagundua ya kuwa mchezo umewajeukia wao bila hata wao kutambua.

2. Jipe shughli kwa kuwa buzy
Hakikisha kuwa unajipa shughli zako kila muda. Mwanzo kama mnafanya kazi katika jengo moja ama mnasoma darasa moja hakikisha ya kuwa unafanya shughli zako kama kawaida ili uonekane huna muda na mambo ambayo anafanya...yaani humtambui kama yuko hapo.

Kwa bahati mbaya iwapo itatokea umekuwa na yeye katika sehemu moja jifanye unatext mtu ili mradi usiongee na yeye. Hii itamfanya yeye kujiona mjinga akiwa kando yako sababu wewe upo buzy na shughli nyingine. Kama ni hali mko shuleni, unaweza kumpuuza kwa kujikeep buzy ukiongea na rafiki yako mwingine [Soma: Hatua wanawake hutumia kutongoza wanaume bila kujulikana]

3. Usijifanye uonekane mwenye wivu
Mfano
Umemuona mpenzi wako wa zamani akiandamana na mwanamume/mwanamke anayevutia kama vile Justin Bieber/Beyonce wakitembea wakija upande wako.

Kitu cha kufanya
Usionekane mwenye wivu. Jiweke asili yako vile ulivyo.

Unaweza fikiria unapishana tu na wapenzi wawili ambayo huwajui kamwe. Usijaribu kuwakimbia.

Ukijaribu kuwahepa utakuwa unatuma ujumbe kwa mpenzi wako wa zamani ukiashiria ya kuwa bado unawapenda na kumwona yeye na mwanamume/mwanamke mwengine kumekufanya uvunjike moyo. Huku kutawafanya wao kujiskia wako juu na kujiskia raha. Badala ya wewe kuwafanya wajiskie hivi, hakikisha ya kuwa unawapuuza kabisa. Jambo hili litawafanya kuwa na maswali mengi iwapo kama tatizo liko wapi. Kile unachofaa kufanya nikuwapuuza.

4. Badilisha muonekano wako. Kuwa mtu tofauti
Owk najua ushawahi kuskia zaidi ya mara elfu moja kuwa unafaa kubadilisha muonekano wako ili kujionyesha. Well, kufanya hivi kuna umuhimu gani?


 • Kujibadilisha kunakupa mwonekano mpya na kunakufanya ujiskia vizuri kuhusu wewe mwenyewe. Kufanya hivi kunakupa confidence na kuweza kujiamini kila mahali utakapokwenda.
 • Kama unaonekana vizuri, kwa kawaida inakuwa kama ni kioo kinachokumulika ndani yako. Hii itatuma meseji kwa mpenzi wako wa zamani kuashiria kuwa maisha yako hayazunguki kwa mtu mmoja pekee ambaye ni yeye.
 • Iwapo umejibadilisha kabisa, watagundua ya kuwa kuna nafasi ya haraka kwako kuweza kupata mchumba mwingine. Hii inaweza kumfanya Ex wako kuingiwa na hisia za woga wa kukupoteza asilani. Hivyo kuna uwezekano wa yeye kujipendekeza kwako ili mrudiane.
5. Kuwa mtu usiyejali na ujiburudishe
Tumia muda wako ulionao kujiinjoy na marafiki zako. Jumuika na marafiki zako sehemu tofauti, cheka zaidi, enjoy maisha hadi kilele chako. Iwapo ulikuwa na stress ama mkazo wa maisha wakati ulipokuwa ndani ya mahusiano naye na sahizi umekuwa tofauti itaashiria kuwa umekuwa na utofauti mkubwa na kuwa ndani ya mahusiano naye ilikuwa ni balaa tupu. [Soma: Jinsi ya kuipendua akili ya mwanamke]

6. Jifunze kukataa
Ukionyesha kuwa bado unampenda mpenzi wako wa zamani, basi wanaweza kuutumia huu mwanya kukutumia vibaya kwa kuwa hauna uwezo wa kukataa chochote ambacho wanaweza kusema.

Acha kuwa mtu wa aina hii kwa kujikeep buzy na mambo tofauti ya muhimu. Jiheshimu wewe mwenyewe kwa kukataa kutumiwa ovyo. Usikubali kamwe kufanywa mtumwa na mpenzi wako wa zamani. Mwonyeshe kuwa umekuwa tofauti kabisa na mtu ambaye ulikuwa zamani.

Jipe shughli na vitu vyako ili usiweze kutumiwa na ex wako. Hata kama ni kumsaidia na kitu ambacho kinaweza kuchukua dakika 15 unahaki ya kumwambia usoni mwake kuwa haujiskii na kile anachotaka umfanyie.

7. Ingia gym, boresha umbo lako
Kuingia gym ni mbinu moja wapo ambayo unaweza kuitumia kusahau mambo yako ya zamani. Pia kuingia gym kunakupa nafasi kwako kujishepu mwili wako ili uwe na toni ya kuvutia. Pia gym inakusaidia kukupa confidence na kujiamini. Pia gym inakufanya uwe na nguvu zaidi.

Mpenzi wako wa zamani aka ex wako akiona mabadiliko yako ya kimwili, kujiamini na nguvu bila shaka atavutiwa nawe. Labda wakati mwingine anaweza kukuomba kama unaenda gym muende pamoja. [Soma: Aina ya wanawake ambao watayafanya maisha yako ya kimapenzi kuwa ya shida]

8. Usiwahi kumsifia
Mfano
Wewe na ex wako mmekutana katika birthday party ya rafiki yenu halafu akakusifu kwa mtindo wako uliovalia kwa kusema "Umependeza". Wewe ni lazima umjibu pia.

Vile unavyotakiwa kusema
Mjibu kwa kumsifia lakini usiingie sana. Unaweza kumwambia "Pia wewe umependeza lakini mtindo wa nywele zako umekaa vibaya na nguo" ama "Hio nguo uliyovaa inaweza kufanya kila mwanamke akuangalie lakini marashi uliopaka yananuka vibaya"

Ok hii itawachanganya kabisa kwa sababu hawakutarajia kamwe kuskia neno 'lakini' katika kuwasifia.

Unaweza kuonekana mchoyo lakini hio ni muhimu katika kutimiza lengo lako la kutumia mbinu ya kisaikolojia ili kurudisha akili yake kwako.


Mwisho nikuwa ukitumia mbinu hizi zote kuna uwezekano mkuu wa ex wako kukutizama na sura mpya. Kurudiana na ex wako kutategemea na chanzo chenu cha kwa nini mliachana mara ya kwanza. Labda ilikuwa ni sababu ya kuboeka na mahusiano yenu ama sababu tofauti kabisa.


7 comments:

 1. Kwa upande wangu mi nadhani kuhangaika kufanya vyote hivyo ulivyoorodhesha ili tu umfanye mpenzi wako wa zamani atamani kuwa nawe ni sawa na kupoteza muda wako, yani ni kama unajitesa bure tu kufanya vyote hivyo ili upate attention ya ex wako wakati yeye tayari yupo na mtu mwingine.

  Ila kama unafanya vyote hivyo ulivyoorodhesha kwa manufaa yako wewe mwenyewe na kuendelea na maisha bila ya kujali kama ex wako anataka kuwa nawe au hataki, basi ni sawa kabisa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Mimi wangu alikua hapokei simu zangu lakin kwa sasa ananitafta yeye tena anasema ananipenda
   Nashindwa kumwamini koz ako na mwingine

   Delete
 2. Nilikuwa kwenye hatihati ya kumpoteza mke wangu wa miaka sita kwa sababu alisema hakuwa na hamu tena na ndoa yetu, ambayo inalea binti mzuri kwa sababu kama dereva wa lori huwa nikienda barabarani, lakini nampenda sana na namjali mke wangu. Nilimuuliza yeye na binti yangu shida ni nini, lakini hakutoa ufafanuzi mzuri, akisema alikuwa amechoka na umoja wetu, ilikuwa ya ajabu kwangu kwa sababu mke wangu alikuwa mwanamke mwenye upendo, ghafla kila kitu hubadilika tu. na mtazamo wake kwangu haukuwa mzuri, nilijua ilikuwa mbaya mahali pengine, kwa hivyo nilielezea mambo kwa rafiki yangu mzuri Micheal, ambaye alinitambulisha kwa jina la mwandishi wa spell Dr.Pellar, nilielezea hali yangu kwa mwandishi, ilifanya ninatambua kuwa mpenzi wa zamani alikuwa akimdanganya mke wangu kuniacha, lakini akaniambia nisiwe na wasiwasi. Nilifuata maagizo yote na mke wangu alirudi kwa ustawi wake wa kawaida na ninashukuru sana kwa kile msaidizi wa Dr.Pellar amenifanyia, kwa hivyo nashiriki shuhuda zangu ikiwa unakabiliwa na shida yoyote maishani na unahitaji suluhisho kuwasiliana na daktari huko DrPellar kwenye barua pepe yake drpelar@gmail.com

  ReplyDelete
 3. This comment has been removed by a blog administrator.

  ReplyDelete
 4. Sikuamini kuwa ningeweza kuungana tena na mpenzi wangu wa zamani, nilipatwa na kiwewe cha kusimama peke yangu bila mwili wa kusimama na kuwa nami, lakini nilipata bahati sana siku moja nilikutana na Dk DAWN, baada ya kumwambia. kuhusu hali yangu alifanya kila liwezekanalo kumuona mpenzi wangu anarudi kwangu, kiukweli baada ya kunifanyia uchawi mpenzi wangu wa zamani alirudi kwangu chini ya masaa 48, mpenzi wangu wa zamani alirudi huku akiniomba kuwa hatoniacha kamwe. tena. Miezi 3 baadaye tulioana na kuoana, ikiwa una hali sawa. Ana nguvu nyingi katika mambo yake;
  * upendo
  inaelezea * inaelezea kivutio
  * kama unataka ex wako nyuma
  *acha talaka
  *kuvunja mawazo
  * huponya viharusi na magonjwa yote
  * uchawi wa kinga
  *Ugumba na matatizo ya ujauzito
  * bahati nasibu
  * bahati nzuri
  Wasiliana na Dk Ediomo kwenye barua pepe yake: dawnacuna314@gmail.com
  Whatsapp:+2349046229159

  ReplyDelete
 5. Baada ya kuona chapisho kwenye mtandao la Jenna kutoka USA akisema jinsi alivyosaidiwa na Dk. DAWN, niliamua pia kuwasiliana naye kwa msaada kwa sababu sikuwa na chaguo nilichotaka ni kumrudisha mpenzi wangu na furaha. Kwa mshangao mkubwa mpenzi wangu alifika nyumbani akiwa amepiga magoti kwamba nitafute nafasi moyoni mwangu kumsamehe, hakika nilistaajabu na kushtuka mpenzi wangu alipopiga magoti akiomba msamaha na mimi nimkubalie tena. Kweli nimepungukiwa na maneno, na sijui ni kiasi gani cha kukushukuru wewe Dr. DAWN. Wewe ni Mungu aliyetumwa kurejesha uhusiano uliovunjika, Na sasa mimi ni mwanamke mwenye furaha. mawasiliano yake ni Whatsapp +2349046229159
  dawnacuna314@gmail.com

  ReplyDelete

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.