Jinsi Ya Kumfanya Mwanaume Akupende


Unampenda mwanaume flani lakini hajaonyesha dalili zozote za kukupenda? Umejaribu kutumia maujanja yako uliobarikiwa nayo kama mwanamke lakini bado unashindwa kuinasua akili yake? Kumfanya mwanaume akupende si jambo gumu la kufanya, kile unachohitaji ni kutumia mbinu hakika ambayo imefanyiwa utafiti na kuonyesha kuwa inafanya kazi mia kwa mia.


Tukirudia kutumia mbinu hakika ni kuwa kama team ya Nesi Mapenzi, tumekuja na miongozo ambayo ikitumiwa vizuri basi bila shaka unaweza kumfanya mwanaume yeyote akupende.

1. Kuwa machoni mwake
Kumfanya mtu akupende ni rahisi. Iwapo mara kwa mara utakuwa machoni mwake itafikia wakati flani kuwa amekuzoea kiasi cha kuwa akienda mahali asipokuona basi hasikii raha. Hii unafaa kuitumia kwa mwanaume unayemzimia kwa kuwa karibu na yeye mara kwa mara. Mfano akienda library kusoma, wewe unafaa uwe uko karibu naye, akiwa ameenda kula lunch katika hoteli flani unaweza kupata kisababu cha kuenda naye nk ilimradi muda wake mwingi awe anakutia machoni.

2. Jeuza mtindo
Baada ya kuona ya kuwa amekuzoea ama mmezoeana, kile unachotakiwa kufanya ni kubadilisha mtindo mzima. Usipokee simu zake kwa muda wa siku tatu, akikutext mjibu baada ya masaa matatu huku ukimwambia uko buzy. Zile sehemu ambazo amekuzoea mnakutana pamoja usiwe ukienda mara kwa mara.  Kufanya hivi kutamfanya mwanaume kuvutiwa zaidi na wewe kwani tayari ulikuwa ushamzoesha yeye kukuona mara kwa mara. Iwapo kama mwanauume ataonyesha interest na wewe hapa basi fahamu kuwa umepiga hatua kubwa kumfanya mwanaume huyu akupende. [Soma: Hatua za kufanya iwapo unataka mpenzi wako wa zamani arudiane nawe]

3. Mfanye specially kwako
Mfanye ajiskie maalum wako. Njia moja wapo ya kumfanya mwanaume azuzuike kwako ni kumchukulia kwa njia ambayo kunamfanya yeye kujiskia ama kujiona mtu maalum sana kwa maisha yako. Kama uko na marafiki ama katika gumzo la watu, makinika kwake peke yake na kujihusisha na yale ambayo ataongea. Mwangalie machoni bila kupesa huku ukimuuliza maswali ya kepekee ambayo yanamlenga yeye.
Pia unaweza kujaribu maji mapya kwa kuonyesha azma ya kutaka kuyajua maisha yake, vitu anavyovipenda na kutaka kujua urafiki wenu nk.

4. Kutana naye 'kibahati mbaya'
Kutana naye kibahati mbaya. Hii kutamfanya kufikia kana kwamba kuna uunganisho kati yenu. Mfano kama umegudua ya kuwa anapenda kusoma gazeti katika mkahawa flani mjini, unaweza kujipeleka hapo kimakusudi ilimradi aone kuwa makutano yenu yalikuwa ni sadfa. Mfanyie saprize kwa kushangaa kukutana naye hapo. Mwangalie vile atakavyofanyika wakati ambapo amekuona. [Soma: Mambo wanawake hufanya ambayo huwachukiza wanaume]

5. Jirembeshe uonekane
Kujirembesha haimaanishi kujibadilisha vile ulivyo. La! Vile unavyotakiwa ni kuhakikisha ya kuwa unakuwa nadhifu na msafi. Hakikisha kuwa unavalia nguo zako za kawaida lakini zitie nakshi kiasi flani. Mfano unaweza kuvaa bangili,shanga, vipuli nk. Pia jipulize marashi mazuri (wanaume huwa wanyonge ikija maswala ya marashi ya wanawake). Hakikisha haubadilishi tabia zako ili uweze kumfanya mwanaume akupende.

6. Onyesha uhuru wako
Jambo ambalo wanawake hukosea kwa wanaume ni ile tabia ya kutojitegemea wao wenyewe. Tabia ambayo inachukiza mwanaume ni kuona mwanamke anapenda kumtegemea mwanaume kama kupe.
Vile unavyotakiwa kufanya ni kuhakikisha kuwa unajitegemea wewe mwenyewe. Muonyeshe kuwa wewe una maisha yako, vitu unavyopenda kufanya, una marafiki zako na kuwa hutegemei yeyote katika maisha yako. Usiogope kutoa maoni yako kuhusu maswala fulani. Amini usiamini, mwanaume akikuona unatabia kama hizi atavutiwa nawe bila yeye kujielewa. [Soma: Tabia chafu za wanawake ambazo zinapendwa na wanaume]

NB: Hakikisha kuwa hauigi tabia za mtu yeyote. Kama unaona baadhi ya kufanya mambo haya ni magumu, chukua muda wako wote wa kufanya mazoezi ili mwishowe uweze kushika. Ukiiga tabia ambazo si zako ni rahisi kugunduliwa na mwishowe utajiharibia mwenyewe kwa kuitwa feki.


No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.