Mambo Ambayo Wanawake Hufanya Na Huchukiza Wanaume


Ok najua haiwezekani kukusanya wanawake wote pamoja kwa kuwa kila mwanamke ana tabia tofauti kabisa na mwengine. Na pia si wanaume wote wanaudhiwa na kitu kimoja. Lakini kwa kawaida wanaume wakati mwingine huweza kuwa na tabia za ujumla, yaani kuna mambo ambayo wanaume wa kawaida huwa nayo kwa pamoja. Hivyo tumeamua kuja na baadhi ya mambo kwa ujumla ambayo huwaudhi wanaume kutoka kwa wanawake.

Hivyo kama mwanamke unapenda baadhi ya tabia hizi basi fahamu ya kuwa unamchukiza mpenzi wako.


Kuwa na hisia nyingi
Wanaume wanaweza kupandwa na mori iwapo wapenzi wao wanakuwa na hisia za kupindukia, sana sana kama wanaanza kulia halafu wanatarajia wanaume kutatua matatizo yao. Wanaume wanajua kuwa wanawake huwa na hisia nyingi kuanzia kuvunjika kucha zao ama kusongwa nywele vibaya. Wanaume wengi hukiri ya kuwa ni vigumu kwao kuweza kutatua baadhi ya matatizo kama haya.

Kuwa mzuri kuliko mwengine
Wanawake wanapenda sana kuwasifia wapenzi wao kuwa ni wazuri na eti ni tofauti kuliko wapenzi wake wa zamani. Mara ya kwanza kwanza mwanaume atapenda kusikia maneno kama hayo na kuona kama ulipitia pabaya wakati wa mahusiano yako na wengine lakini baada ya muda ataanza kufikiria kuwa wewe utamwingiza katika moja wapo la kundi ambalo atakuwa ukimuita 'mwanamume fala'. Njia nzuri ya kutatua jambo hili ni kusema ya kuwa hujawahi kuwa katika mahusiano yeyote na mwanaume hivyo mtakuwa na wakati mzuri pamoja. [Soma: Sheria za kutumia wakati unapomtext umpendae]

Kuongea bila kikomo
Wanawake wanapenda sana kuongea kuhusu mahusiano yao ya kimapenzi na marafiki zao wanawake. Lakini hio ni tofauti  kwani wanaume hawapendi sana kuzungumza mengi so kama una maneno mengi yasiyokuwa na mwisho basi itakubidi uachane na hio tabia.

Shopping isioisha
Ukweli usemwe ni kuwa wanawake hupenda sana kufanya shopping kiasi cha kuwa inafikia wakati fulani inaudhi. Sasa kama wewe ni mwanamke unayependa kufanya shopping usijaribu kuenda shopping na mpenzi wako. Tabia ya kuingia kwa duka kwa masaa mawili kununua dress na mpenzi wako kutakutia taabani. Hii ni kwa sababu ya kuwa muda mwingi mwanaume hatakuwa na kitu cha kufanya ila kukuangalia tu wewe. Pia tabia ya kuvaa nguo kisha unamuuliza kama imependeza au la.


Hizi ni baadhi tu ya mambo ambayo huchukiza wanaume hivyo ni bora kama utaacha tabia kama hizi kabisa.No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.