Njia 9 Za Kutambua Kama Mwanaume Ana Uume Mkubwa


Kujua ukubwa wa uume wa mwanaume ni swala kubwa ambalo linatatiza wanawake wengi hadi siku ya leo. Wakiwa katika vikao vyao wako tayari kujadiliana na kuwaza ukubwa wa uume wa wanaume. Kuna dhahania tofauti tofauti ambazo wanawake hubuni kufananisha mwili wa mwanaume na uume wake. Wengine husema mtu mrefu ana uume mkubwa, wengine husema mtu mwenye vidole virefu ana uume mkubwa na dhahania nyingi zisizokuwa na mwisho.


Ok, kabla hatujaingia katika mada hii, swali ni; Je uume mkubwa una manufaa yeyote? Wanawake wengi husema ukubwa wa uume si kigezo muhimu, wengine nao husema ukubwa wa uume ni lazima kwa mwanaume yeyote.

Swala hili linanikumbusha mwaka wa 2018 Disemba jijini Nairobi kulipokuwa na Wasafi Festivals. Msanii Lava Lava alipopanda jukwaani wanawake wa jiji hilo walianza kumshambulia kila mmoja akijaribu kuuangalia ukubwa wa uume wake. Hii inaashiria nini? Hii ni ishara ya kuwa uume ni kigezo muhimu ambacho kinaangaliwa katika mwanaume. Wewe jiulize kwa nini dawa za kuongeza uume zinakuwa na soko kubwa kuliko dawa nyingine duniani! Na mbona mara kwa mara unakumbana na matangazo ya aina hii! Hii ni ishara kuwa uume mkubwa una umuhimu wake.

So, kama uume mkubwa una umuhimu wake, je unajua ni vigezo gani ambavyo vinatumika kutambua kama mwanaume ana uume mkubwa?

Zama nasi!

#1 Hakuna njia hakika ya kusema.
Huu ndio ukweli wa mambo. Hakuna njia thabiti ya kudhihirisha kuwa mtu ana uume mkubwa au la. Unaweza kudhani mtu flani ana uume mkubwa na mwisho ukagundua kuwa hana. So huwa mara nyingi ni kubahatisha. Huwezi kuwa na uhakika asilimia 100. [Soma: Ishara kuonyesha mpenzi wako ana mchepuko]

#2 Anakuwa na confidence.
Mwanaume mwenye uume mkubwa utamtambua na confidence yake. Mwanaume kama huyu haogopi kujitokeza mbele ya wanawake wengi. Yuko tayari kukabiliana na changamoto ambazo zinaweza kujitokeza. Mfano mzuri unajitokeza pale msanii Lava Lava aliposimama mbele na kujiachilia wanawake wauguse uume wake. Kama angekuwa hajiamini basi ingekuwa ni ishara ya kuwa ana kiume kidogo. Angalia video yenyewe alivyodhihirisha confidence:


#3 Hulka yake.
Hulka ni tabia ya mtu binafsi. Ukiona mwanaume ana majisifu na anapenda kujisifu kwa mambo kama vile; mimi nina hiki na kile, hakuna mtu ananishinda, na kadhalika basi huyo hana kitu. Mwanaume mwenye uume mkubwa ni yule ambaye ni mnyenyekevu, hana mambo mengi na mtulivu.

#4 Mikono yake.
Hii ni moja wapo ya dhahania ambayo wanawake hupenda kuitumia. Mwanaume mwenye mikono mirefu ni ishara ya kuwa huko chini bia ni kukubwa. Hiki ni kigezo ambacho hutumika na wanawake wengi. [Soma: Ishara za kuonyesha kuwa anacheza na moyo wako tu]

#5 Miguu yake.
Wanawake wengine wamedhibitisha kuwa mwanaume mwenye miguu mikubwa ni ishara ya uume mkubwa. Lakini mara nyingi kigezo kama hiki hakitumiki sana kwa kuwa miguu hufichika na viatu.

#6 Mfuro.
Hii ndio njia rahisi ya kutambua kama mwanaume ana uume mkubwa au la. Kama amekaa kwa kiti na ukaona kwa suruali yake imefura basi ni ishara. Pia jinsi anavyotembea utagundua. Huwa atakuwa anatembea utofauti kana kwamba ana miguu mitatu.

#7 Sehemu anayotoka.
Pia hiki ni kigezo kikubwa cha kuangalia. Je, huyu mwanaume ni wa mkoa upi ama ni wa kabila lipi. Kuna makabila mengine inasifika kwa miume mikubwa ilihali wengine hawana sifa za maana. [Soma: Jinsi ya kuwa na mahusiano marefu na mpenzi wako]

#8 Pua kubwa.
Ni tamaduni ambayo imeaminika ya kuwa wanaume wenye pua kubwa au ndefu wanakuwa na uume mkubwa.

#9 Haongei sana.
Mwanaume aina hii hajisumbui kuongea sana akiwa na marafiki zake. Haswa hutamuona akiongea maneno mengi akiwa na marafiki zake wakiwa na wanawake. Hii ni sababu hataki kujidhihirisha mbele ya wanawake. Tayari anajua ana uume mkubwa so swala la kujipendekeza mbele ya wanawake hana. [Soma: Sababu wanawake huwaplay waume zao]

Kumjua mtu ambaye ana uume mdogo utamjua na mambo mawili makuu. Kwanza ni kuwa atakuwa na majisifu. Atajisifu kuhusu uume wake jinsi ulivyo mkubwa na jinsi wanawake hupiga kelele wakiwa mchezoni. Mwanaume kama huyu hana lolote. Pili ni wale ambao wanakuwa na misuli mingi na wenye miraba minane. Huyu hana lolote. Kuingia kwake gym anajaribu kujitosheleza kwa kuwa anakosa kitu muhimu hapo chini.

Upo!?


2 comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.