Ishara 11 Za Kuonyesha Kuwa Anacheza Na Moyo Na Hisia Zako


Kitu cha kwanza ambacho unafaa kujua ni kwamba kuwa katika uhusiano wa kimapenzi si rahisi. Na pindi wakati ambapo utapenda inakuwa vigumu zaidi. Hapa simaanishi kuwa haupaswi kutafuta mapenzi, la. Mapenzi huwa na hisia nzuri sana katika zote.


Lakini pia unafaa ujue kuwa katika mapenzi kuna changamoto zake. Unaweza kuwa unampenda mpenzi wako ila yeye hakuthamini. Ama unaweza kuwa uko katika uhusiano na mpenzi wako lakini kumbe yeye anakuchezea tu na mipango yake ni tofauti na yale ambayo unapanga wewe.

So leo tumekuja na ishara ambazo zitakusaidia ujue iwapo mpenzi ulienae anakupenda ama anachezea hisia zako na mbaya zaidi anakuumiza moyo bila wewe kufahamu.

Ishara 11 za kutambua iwapo anakuchezea kihisia.


#1 Unahisi kuwa kuna kitu ambacho hakiko sawa. Hii ni hisia ambayo mara nyingi inakuja yenyewe bila kuambiwa na yeyote. Unaanza kujiuliza maswali mengi kumhusu mpenzi wako na mwishowe unakuja kujipatia jawabu. So ikiwa umeanza kuhisi kuwa kuna kitu ambacho hakiendani sawa basi ni wakati wako wa kuchukua hatua ya mbele. Usikubali kubahatisha kamwe kwa kuwa mwishowe itakuwa mbaya kwako.

#2 Hajihusishi na agenda ambazo ni za kudumu. Agenda za kudumu zinaweza kuwa wiki mbili, miezi, hata mwaka. Hoja hapa ni kuwa mpenzi wako huyu hajihusishi na chochote. Ukimuuliza miezi mitatu unatuona wapi mimi na wewe anakujibu hajui. Ama unamwambia wiki inayokuja kuna harusi nataka tutoke deti pamoja halafu anakujibu bila jazba, “Nitaangalia” halafu hashughuliki zaidi hapo unapaswa utie shaka.[Soma: Tambua iwapo mwanamke anakupenda kwa kuiangalia miguu yake]

#3 Anapenda vile vitu vizuri katika maisha. Kila mtu anapenda maisha mazuri, so sikatai. Lakini kila kitu pia kina kiasi. Ukiona kila siku ukitoka deti ama out na mpenzi wako anataka umpeleke zile sehemu nzuri nzuri pekee, anataka umnunulie vitu ghali vya bei ya juu na umtunze hapo unapaswa uanze kujiuliza maswali. Huyu bila shaka hayuko nawe kujenga hisia bali anakutumia halafu akutupe kama vocha. Ukiona mpenzi wako anakutumia kama kitega uchumi jua huyo hakupendi.

#4 Mazungumzo yenu si ya undani. Wewe na huyu mpenzi wako hakuna cha maana mnachoongea. Cha zaidi atakuuliza ni kazini, shuleni, marafiki zako ama sehemu ulizokuwa. Hatawahi kuzungumza vitu ambavyo vinagusa hisia yake kama mambo aliyopitia utotoni, mambo yake ya ndani ama jinsi anavyohisi anavyokuwa na wewe.[Soma: Mbinu ambazo wanawake huwrza kutongozea bila wao kujua]

#5 Anachukua muda mwingi kukujibu. Hapa namaanisha kuanzia kujibu sms zako hadi kujibu calls zako. Ok, nafahamu kuwa wengine wanakuwa busy siku nzima so hawawezi kujibu simu zako haraka lakini hauwezi kukosa dakika hata moja kureply mtu unayempenda.

#6 Hakumbuki yale mambo madogo madogo. Yale mambo madogo madogo huwa ndio yanafanya mahusiano ya wawili yashike kasi. Lakini ukimwona mpenzi wako hata hakumbuki kuwa asubuhi ulimwambia umeenda mkutano sehemu flani jua hapo kuna tatizo. Ama hakuulizi siku yako ilienda vipi basi kuna tatizo kubwa hapo.

#7 Haujihisi salama ukiwa naye. Najua hawezi kukumwagilia maji ya moto ukiwa umelala usiku, la. Hapa namaanisha kuwa katika hisia zako kuna kitu ambacho kinakwambia kuwa huyu umpendae anaweza kukuacha saa yoyete. Akipata kwingine ambapo kuna manufaa zaidi kuliko kwako atajitoa.

#8 Anamtaja ex wake mara kwa mara. Kumtaja ex wako huwa ni kawaida kwa kuwa wengi wetu wamekuwa na mahusiano marefu na ma ex wao. Lakini ukiona huyu mpenzi wako haipiti siku lazima amtaje ex wake then ujue anacheza na hisia zako. [Soma: Zimwi mtu ambalo hutesa wanaume wengi]

#9 Hana upendo. Upendo hapa anauonyesha mkiwa faraghani na wakati ambapo mnafanya mapenzi. Lakini pindi mnapotoka nje hadharani unaona anajeuka baridi. Mawasiliano yenu yanapungua kiasi cha kuwa anakuwa mwoga umshike mkono. Ukiona anakufanyia hivyo jua anakupa ishara ya kuwa hataki mahusiano yenu yavuke mipaka fulani.

#10 Umeonywa. Ushaambiwa na watu kuwa huyu mpenzi wako hakufai. Na si mara ya kwanza. Lakini kwa kuwa wewe unaona anakupa tunda ambalo unakula na kushiba unapuuza. Ama unamuona ni mrembo kupindukia hivyo hutaki kuskiliza ya watu. Well, hapo atakuwa tayari ashakufunga akili na anakuchezea akili yako. Ukiona imefikia hatua kama hii lazima urudi nyuma utathmini maisha yako na yeye.

#11 Hayuko ule wakati ambao unamhitaji. Labda umekuwa na tatizo kazini ama ulipigana na rafiki yako. Huu ndio ule wakati ambao unamhitaji mpenzi wako akuliwaze na kukupa sapoti. Lakini wakati huo ndio hapatikani kabisa. Labda hata anakwambia anaenda kuwatembelea marafiki zake,

So kama unaona kuwa mpenzi wako anakuonyesha ishara hizi ambazo tumezitaja basi jua leo anauchezea moyo wako. Akishapata kile kitu ambacho alikuwa anatafuta atakuacha kwa giza.

No comments:

Jiunge na jamii yetu ya Facebook/App yetu ili uweze kutangamana na members na readers wetu wa Nesi Mapenzi ama ujitafutie mpenzi HAPA

Powered by Blogger.